Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 1, 2018

CCM Yatoa ONYO Kwa Wakuu wa Mikoa Wanaosaka Ubunge 2020

adv1
Katibu Mkuu wa CCM, Dk Bashiru Ally ametoa onyo la mwisho kwa wakuu wa mikoa  nchini Tanzania kuacha kuvuruga chama hicho kwa kufanya kampeni kimyakimya ya kusaka majimbo huku wakitumia rasilimali za Serikali.

Dk Bashiru ametoa onyo hilo jana Ijumaa Novemba 30, 2018 wakati akizungumza na wanachama wa CCM Mkoa wa Geita katika ziara mkoani humo.

Amesema wakuu hao wa mikoa, wameshindwa kutumia nafasi zao kutekeleza majukumu waliyokabidhiwa na Rais John Magufuli na kubaki kujiimarisha wao jambo ambalo hataki kuliona likiendelea.

Amewataka wateule hao wa Rais  kufanya kazi ya heshima na ya kikatiba ya ukuu wa mkoa, badala ya kuanza kuvuruga chama katika maeneo mengine.

“Nitawapeleka kwa aliyewateua, nimwambie awatafutie kazi nyingine waache kuvuruga chama, kwa sababu katika hatua za kutafuta ubunge, wanasababisha chuki na fitina katika majimbo, waache hapakaliki, sasa waache kumdharau aliyewateua.”

“Huwezi kujenga uongozi wa pamoja kama wateule wa rais na viongozi wa kisiasa hawana mtazamo wa pamoja,” amesema Dk Bashiru.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )