Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

CHADEMA Waendelea na Msimamo Wao wa Kususia Uchaguzi

adv1
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimeendelea na msimamo wake wa kutoshiriki chaguzi mbalimbali za marudio hapa nchini, kwa kile walichokidai kutofanyiwa haki, pamoja na kuminywa kwa demokrasia.

Msimamo huo wa CHADEMA umedhihirishwa kwenye chaguzi mbalimbali za marudio za hivi karibuni, ikiwemo uchaguzi katika jimbo la Singida Kaskazini, ambako alijiuzulu mwanachama wao wa sasa Lazaro Nyalandu.

Chaguzi nyingine ambazo CHADEMA ilitangaza kutoshiriki ni majimbo ya Ukerewe, Serengeti, Babati Mjini, Simanjiro, Liwale ambapo kwa sasa pia wametangaza kutoshiriki tena uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Temeke.

Akizungumza Jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Mambo ya nje CHADEMA, John Mrema amebainisha kuwa msimamo wao ni ulele na haujabadilika.

"Msimamo wetu haujabadilika na tulishatangaza kutoshiriki uchaguzi mdogo kwa sababu tume ya uchaguzi haitutendei haki lakini leo tuna kikao ili kujua kwa mtu ambaye atashiriki uchaguzi huo tumchukulie hatua gani," amesema John Mrema.

Juzi Desmemba 18 kupitia Katibu Mkuu, Dkt Bashiru Ally, Chama Cha Mapinduzi CCM kilipitisha jina la Abdallah Mtolea kuwa mgombea Ubunge wa jimbo la Temeke.

Jana Disemba 19, 2018 mgombea huyo alichukua fomu ya kuwania ubunge wa Jimbo hilo na leo Desemba 20, 2018 ndiyo mwisho wa kurejesha fomu hizo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )