Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 30, 2018

CHADEMA Yapigwa 'Marufuku' Jimboni Kwa Mbowe

adv1
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimezuiwa kufanya mkutano pamoja na ziara ya viongozi wa chama hicho kitaifa, wilayani Hai mkoani Kilimanjaro.

Hayo yamebainishwa kupitia barua iliyotumwa kwa Katibu wa CHADEMA wilayani Hai, ambayo imesainiwa na Katibu tawala wa wilaya hiyo, Said Omary iliyoelekeza kusitisha kibali cha kufanya mkutano wilayani humo.

"Nimeagizwa na Mkuu wa Wilaya ambae ni mwenyekiti wa kamati ya usalama ya Hai. Nikuandikie kukutaka kusitisha mkutano na ziara ya viongozi wako kitaifa, tarehe 29/12/2018 na kuendelea", imesema barua hiyo.

Baada ya zuio hilo, Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya jana  aliamuru kukamatwa kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dkt. Vincent Mashinji pamoja na viongozi wengine kwa makosa ya kufanya kusanyiko bila kibali.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )