Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 1, 2018

Diwani CCM Atupwa Ndani Saa 48

adv1
Diwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kata ya Okaoni amejikuta akilala rumande kwa saa 48 kwa amri ya Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya baada ya kiongozi huyo kulalamikiwa na wananchi, kuwa amemiliki shamba lenye ukubwa wa heka 500  kwa muda mrefu bila kuliendeleza.

Akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika Kijiji cha Nkwansira, DC huyo amesema mwekezaji huyo ambaye ni Diwani ameshindwa kuendeleza shamba hilo na kusababishia serikali hasara kwa kutokulipa kodi.

Aidha amesema mwekezaji huyo amekua akiwanyanyasa wafanyakazi katika shamba hilo na kuwanyima mishahara.


"Kuanzia leo nimetengua maamuzi ya kikao cha wajumbe 31 waliopitisha na kummilikisha shamba hili mwekezaji huyu hivyo, simtambui pamoja na shughuli zake zote ndani ya wilaya hii,"amesema Mkuu huyo.


Mkuu huyo amechukua hatua hiyo, baada ya kupata malalamiko kutoka kwa wananchi wa Kijiji hicho wakimlalamikia mwekezaji huyo kutokana na matumizi mabaya ya shamba hilo ambalo ameshindwa kuliendeleza na badala yake kulibadilisha matumizi.


Pia, amesema amekua akikwepa kodi na hajawahi kuona kumbukumbu zozote za kulipa kodi kwa mwekezaji huyo na kwamba hamtambui.


"Sina kumbukumbu zozote za mwekezaji huyu na simtambui katika wilaya hi,"amesema Sabaya.


"Haiwezekani shamba hili ambalo amepewa na serikali kulima kahawa alitumie kulishia mifugo na kuotesha maharage,"amesema.

Hali ya kukamatwa kwa viongozi kwa upande CCM imekuwa mara chache kutokea kwa baadhi ya viongozi wa chama hicho, lakini imekuwa ni tukio la mara kwa mara kwa baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani ambao mara kwa mara wamekuwa wakituhumiwa kuvunja sheria.

Machi 2018 Mbunge wa Jimbo la Hanang, mkoani Manyara Dkt Mary Nagu (CCM) na Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo walishikiliwa na Jeshi la Polisi wilayani humo kwa amri ya Mkuu wa wilaya.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )