Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 19, 2018

Fastjet Wajipanga Kuingiza Ndege Mbili....Moja Itatua Nchini Jumamosi Hii

adv1
Mwenyekiti mtendaji wa Shirika la Ndege la Fastjet Tanzania, Lawrance Masha amesema wamejipanga kuingiza ndege aina ya Boeing 737 na Bombardier. Amesema Boeing itaingia  Tanzania Jumamosi Desemba 22, 2018.

Akizungumza leo Jumatano Desemba 19, 2018 katika kipindi cha 360 kinachorushwa na Clouds Televisheni, Masha amesema  ndege ya shirika hilo aina ya Boeing 737 ambayo ilizuiliwa kuruka na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kutokana na hitilafu za kiufundi, sasa iko imara.

“Kuanzia Jumamosi tukakuwa na ndege mbili aina ya Boeing 737 (pamoja na iliyopo sasa) ambazo zitakuwa tayari kufanya kazi. Hii  itasaidia kuondoa kero ya kusitishwa kwa safari,” amesema Masha.

“Ndege zote zitakuwa na usajili wa Tanzania na kutokana na mahitaji na msimu,  hivi karibuni tunaweza kuongeza ndege nyingine moja au mbili aina ya Bombardier.”

Amesema ana imani shirika litainuka na kuwa imara zaidi na juhudi zinazofanyika sasa ni kuzungumza na mamlaka ili kuwaruhusu kuanza kuuza tiketi.

Amesema tayari baadhi ya matakwa ya mamlaka hiyo yametimizwa au kujibiwa ingawa bado mazungumzo yanaendelea.

“Tunatarajia kurejesha safari zetu za Nairobi na Afrika Kusini kuanzia Februari 2018 na kuanza kwenda Songea, Dodoma, Bukoba na Arusha mjini endapo TCAA wataturuhusu kwakuwa tutakuwa na ndege ndogo ambazo zina uwezo wa kutua katika viwanja hivyo,” amesema Masha.

Juzi, TCAA ilitangaza kuwa Fastjet imepoteza sifa ya kufanya biashara nchini na ndege yao moja imezuiwa kuruka kutokana na matatizo iliyonayo na kukosekana kwa meneja mwajibikaji wa shirika. Ilitoa notisi ya siku 28 ikikusudia kuifuta leseni ya shirika hilo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )