Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 17, 2018

FastJet Yatangaza Kusitisha Safari za Ndege Disemba na January 2019

adv1
Kampuni ya Ndege ya Fastjet Tanzania imesitisha safari zake za Desemba 2018 na Januari 2019  kutokana  na sababu za utendaji.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 17, 2018, menejimenti ya kampuni hiyo imesema wateja wote watarudishiwa nauli zao Desemba 20 mwaka huu kwa utaratibu uliotumika katika manunuzi ya tiketi.
 
“Fastjet inaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza. Tunawaomba abiria pamoja na mawakala wa safari za anga kuwasiliana nasi kupitia namba za simu za mkononi au barua pepe ili kupata ufafanuzi zaidi,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.
 
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, pia imeagiza kampuni na mashirika mbalimbali yaliyokuwa yanafanya biashara na Fastjet yawasiliane kwa njia ya barua pepe au maofisa husika.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )