Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 3, 2018

Godbless Lema Ataka Naibu Spika Tulia Ackson Ashughulikiwe Kwa Kuimba Wimbo wa Nyegezi Mwanza Uliofungiwa

Video inayosambaa mtandaoni ikimuonyesha Naibu Spika wa Bunge, Dr. Tulia Ackson Mwansasu akiwa na Wabunge wanzake wakiimba wimbo ‘Mwanza’ wa muimbaji Rayvanny ambao umefungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), imezua gumzo mtandaoni.

Wabunge hao walikuwa nchini Burundi kwenye michuano ya wabunge na baada ya kuibuka na ushindi wakaanza kushangilia kwa style ya kuimba wimbo huo ambao upo kifungoni.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kwa kudai kwamba, Mhe Spika Tulia anatakiwa kuhojiwa na kamati ya maadili ya Bunge kuhusiana na tukio hilo.

“Nina muomba Mh Spika Ndugai aitishe kamati ya maadili ya Bunge juu ya kitendo cha Naibu Spika Mh Tulia kuimba na kucheza wimbo uliopigwa marufuku na Basata unaoitwa Nyege,Nyege ,Nyegezi /Mwanza akiwa Nchini Burundi.Mimi na Mke wangu tume huzunika sana".
Video hiyo ipo kwenye mtandao wa Instagram wa meneja wa Diamond, Babu Tale.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )