Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, December 12, 2018

Gwajima, Lusekelo Wamwaga Maombi IKULU

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo leo Jumatano Desemba 12, 2018 wameungana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Leo Rais Magufuli anasaini mkataba wa ujenzi wa mradi wa kuzalisha umeme katika Pori la Akiba la Selous wa Stiegler’s Gorge na viongozi hao wa dini wamekuwa miongoni wa viongozi mbalimbali wa dini waliohudhuria hafla hiyo.

Kabla ya kuanza kwa hafla hiyo, viongozi hao wa dini walianza kwa kufanya maombi kila mmoja.

Gwajima amemuomba Mungu awawezeshe  nguvu wote wanaofanya kazi na Rais John Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu,  Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri na watumishi wote wa serikali.

“Nafunga kila kazi zenye kukwamisha mradi wa Stiegler’s Gorge, ukiwemo wizi, rushwa, maneno ya kuvunja moyo; nayazuia katika jina la Yesu na kila mmoja katika nafasi yake atiwe nguvu,” ameomba Gwajima
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )