Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 18, 2018

Hukumu Ya Tido Muhando Kusomwa January 25

adv1
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imepanga Januari 25, 2019 kutoa hukumu ya kesi ya matumizi mabaya ya madaraka inayomkabili  aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Tido Mhando.

Hukumu hiyo ilipangwa kusomwa leo Jumanne Desemba 18, 2018 lakini Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Huruma Shaidi amesema hajakamilisha kuandaa hukumu kwa sababu kuna vitu bado anavifanyia utafiti kabla ya kutoa hukumu hiyo.

"Hukumu yako Tido bado haijakamilika, kuna vitu bado navifanyia utafiti. Januari 25 nitatoa hukumu, utaendelea kuwa nje kwa dhamana hadi siku hiyo,” amesema Hakimu Shaidi.

Tido anakabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )