Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 2, 2018

Joshua Nassary "Apewa Makavu" Mbele ya Rais Magufuli

Mbunge wa Viti Maalum CCM, Amina Mollel amedai tangu Joshua Nassari alipochaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki kwa tiketi ya Chadema, ametokomea kusikojulikana na hajui shida za wananchi waliomchagua.

Mollel ametoa madai hayo leo Jumapili Desemba 2, 2018 katika uzinduzi wa mradi wa uboreshaji huduma za maji safi na maji taka katika jimbo la Arumeru Mashariki uliofanywa na Rais Magufuli.

"Naamini walifanya makosa na hawatarudia tena 2020 na mimi niko hapa kwa ajili ya kuwasemea ili kuhakikisha shida zao zinatatuliwa," amesema Mollel. Katika uzinduzi huo Nassari hakuwepo.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema Nassari yupo na wananchi wake na anafanya shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwamo katika sekta ya elimu na afya.

“Kuna kipindi Nasari alikuwa anasoma ila kwa sasa amemaliza na anaendelea na shughuli zake za Kibunge, Amina si msemaji wa wananchi wa Arumeru kazi hiyo ni ya wananchi wa Arumeru na kama alitaka kushitaki angewashitaki kwa Rais, mawaziri waliotajwa kutohudhuria vikao vya Bunge. 

Kwa upande wake mbunge wa Monduli, Julius Kalanga amemuomba Rais kuwasaidia kuondokana na shida ya maji kwa sababu wananchi wake wana hali mbaya.

Amesema hata akipewa nafasi kadhaa za kutoa maombi yake ili aweze kusaidiwa katika utekelezaji mara zote angetaja maji.

"Kama ulivyowakumbuka wenzetu wa Arumeru, tunaomba na sisi utukumbuke katika ufalme wako kwa sababu tuna shida kubwa ya maji," amesema Kalanga.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )