Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 15, 2018

Kamishna wa zamani TRA Harry Kitilya na wenzake Kuendelea Kusota Rumande

adv1
Mwenyekiti wa kampuni ya Egma inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na dhamana, Harry Kitilya na maofisa wa zamani wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na Sioi Solomon watamaliza mwaka wa 2018 bila ya shauri lao kuanza kusikilizwa baada ya mahakama kuambiwa jana kuwa upelelezi haujakamilika.

Kitilya, ambaye alikuwa kamishna mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA), Shose, ambaye alikuwa Miss Tanzania wa mwaka 1996 na Sioi, walifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza Aprili mosi 2016 na kusomewa mashtaka manane, likiwemo utakatishaji ambalo halina dhamana.

Wakili wa Serikali, Wankyo Saimon alisema jana kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kumuomba Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kupanga tarehe nyingine.

Washtakiwa hao, ambao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutakatisha fedha, wamerejeshwa rumande ambako wameshaishi kwa takribani miaka miwili sasa tangu wakamatwe.

Hakimu Shaidi alihirisha kesi hiyo hadi Desemba 28, 2018.

Washtakiwa wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola 550 milioni za Kimarekani kwa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )