Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 18, 2018

Lowassa, Maalim Seif, Zitto Kabwe Wajichimbia Zanzibar

adv1
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa vya upinzani  nchini wamejichimbia visiwani Zanzibar kwa ajili ya kupatiana mafunzo mbalimbali juu ya mwenendo wa siasa na demokrasia.
 
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria ni Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamadi, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa na Kiongozi wa ACT - Wazalendo Zitto Kabwe.

Mbali na hao, viongozi wengine walionekana na Rais wa Chama Cha Mawakili Tanzania, (TLS) Fatma Karume pamoja viongozi wengine mashuhuri nchini ambapo imeelezwa walijadili juu ya mwenendo wa hali ya kisiasa nchini.

Kaimu Msemaji wa chama cha CUF, Mbarara Mahagande amesema kikao hicho kimeandaliwa na taasisi ya marekani IRI kupitia kwa Katibu wa CUF, Maalim Seif.

"Ni kweli kuna semina inafanyika ya viongozi wa vyama inafanyika Zanzibar ambayo inafanyika kwa siku tatu, na aliyewaalika ni Katibu Mkuu wetu Maalim Seif na imeandaliwa na taasisi ya IRSA, watu wa democratic ya America," amesema Maharagande.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter Maalim Seif aliandika; "Ni heshima kubwa kwangu na kwa CUF kuandaa na kuwa mwenyeji wa kikao cha kutathmini demokrasia yetu na kujitathmini sisi wenyewe kama vyama vya upinzani na mwelekeo wetu."
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )