Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, December 1, 2018

Magufuli, Kenyatta kufungua kituo cha pamoja cha forodha

Rais wa Tanzania, John Magufuli na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta wanatarajiwa kufungua Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP) eneo la Namanga upande Kenya na Tanzania kisha kufuatiwa na sherehe ya uzinduzi huo zitakazofanyika upande wa Tanzania.

Viongozi mbalimbali wakiwemo mawaziri, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, wabunge na viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wapo upande wa Kenya kwa ajili ya uzinduzi huo unaofanyika leo Jumamosi Desemba 1, 2018.

Lengo la kuanzisha OSBP ni kurahisisha huduma na watu kuchukua muda mfupi kupata huduma za Forodha mpakani.

Kituo cha Forodha cha Namanga ni moja ya vituo vinavyotumika kutoka na kuingia Kenya mkoa wa Arusha, kituo kingine kidogo ni Osmolo kilichopo wilayani Ngorongoro.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )