Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 18, 2018

Manchester United Yamfukuza Kazi Mourinho

Klabu ya Manchester United imetangaza kuachana na kocha wake mkuu, Jose Mourinho,  kuanzia leo Desemba 18, 2018 ikiwa ni siku mbili tangu alipopokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa mahasimu wao, Liverpool, Jumapili iliyopita.

Taarifa ya klabu hiyo iliyochapishwa kwenye tovuti yake imesomeka kuwa, “Manchester United inatangaza kuwa imevunja mkataba na kocha Jose Mourinho”.

“Klabu ingependa kumshukuru Jose kwa kazi yake nzuri katika kipindi chote alichokuwa na Manchester United na tunamtakia maisha mema huko aendako.”

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 katika kikosi cha Manchester United amefanikiwa kutwaa taji la Kombe la Ligi na Ligi ya Europa katika miaka miwili na nusu aliyokaa ndani ya timu hiyo.

Lakini kwa sasa Man United iko katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa nyuma kwa pointi 19 dhidi ya vinara Liverpool ambao waliwafunga mashetani hao wekundu kwa mabao 3-1.

"Kocha atakayechukua jukumu hilo kwa muda anategemewa kutangazwa hivi karibuni, huku tukiendelea na utaratibu wa kusaka kocha mpya," imesema taarifa ya Man United.

Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )