Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 27, 2018

Mawakili Waomba Kesi ya Vigogo Rahco Ifutwe

adv1
Upande wa utetezi katika kesi ya kuisababishia Serikali hasara ya Dola 527, 540 za Marekani (zaidi ya Sh1 bilioni) inayowakabili vigogo wawili wa Kampuni Hodhi ya Mali za Reli (Rahco), umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuifuta kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Jeremiah Mtobesya ameieleza mahakama hiyo leo Alhamisi Desemba 27, 2018, baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika.

Washtakiwa katika kesi hiyo ni aliyekuwa mkurugenzi mtendaji wa Rahco, Benhardard Tito; mwanasheria wa zamani wa kampuni hiyo, Emmanuel Massawe na mwakilishi wa kampuni ya Rothschild (South Africa) Proprietary Limited, Kanji Mwinyijuma.

Washtakiwa hao wanaendelea kusota rumande takribani miaka miwili na miezi tisa sasa, kutokana na upelelezi wa shauri hilo kutokamilika.

Tito na wenzake walifikishwa kwa mara  ya kwanza, Kisutu  Machi 14, 2016 kujibu mashtaka manane likiwemo la matumizi mabaya ya madaraka.

Awali, wakili wa Serikali, Neema Mbwana akishirikiana na Nickson Shayo amedai mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa na kwamba jalada halisi la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini(DPP) kwa ajili ya kulifanyia maamuzi.

Baada ya maelezo hayo, Mtobesya amedai kuwa kesi hiyo imekuwa ikiahirishwa kila siku kutokana upelelezi kutokamilika na kisha akaomba kesi hiyo ifutwe.

“Wenzetu upande wa mashtaka wamekuwa wakiahirisha kesi hii kwa muda mrefu zaidi ya miaka miwili sasa kwa madai upelelezi bado haujakamilika, “ amesema Mtobesya.

“Hivyo tunaiomba mahakama hii kuwafutia mashtaka wateja wetu wanaoendelea kuteseka rumande, mpaka pale upande wa mashtaka watakapokamilisha upelelezi.”

Akijibu hoja hizo, Wakili Mbwana amedai kuwa kesi ya uhujumu uchumi ina vitu vingi ambayo vinatakiwa kufanyiwa uchunguzi na hivyo kuiomba mahakama kupanga terehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Mtega baada ya kusikiliza hoja za pande zote, aliahirisha kesi hiyo hadi Januari 7, 2019 itakapotajwa tena.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )