Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, December 26, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Aagiza Ng'ombe Waliovamilia Mashamba Ekari 4 Wapigwe Mnada Kufidia Uharibifu Huo

Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira, ameagiza kukamatwa na kupigwa mnada kundi la mifugo inayodaiwa kuvamia mashamba ya wakulima katika kijiji cha Chemchem, Wilaya ya Moshi, baada ya kuharibu zaidi ya ekari 400 za mazao ya chakula.

Dk. Mghwira ametoa agizo hilo jana katika salamu zake za sikukuu za krismasi na mwaka mpya, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkoa ulivyojipanga kuimarisha ulinzi kila kona.

“Nimeshaagiza vyombo vyetu vya usalama kwa maana ya Jeshi la Polisi likamate mifugo ya wafugaji ambayo ilikula mazao ya wakulima wa kijiji cha chemchem na ipigwe mnada ili fedha zitakazopatikana ziwafidie wakulima waliopata hasara ya kupoteza mazao yao.

“Pia nimewaagiza Wakuu wa Wilaya za Moshi na Mwanga wasimamie utekelezaji wa agizo hili. Hatuwezi kaucha mchezo huu ukaendelea kila mwaka, lazima kuwe na heshima dhidi ya dola.”

Siku nne zilizopita, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji, Kadiria Mmari, alitoa taarifa kuwa moja ya mazao yaliyoharibiwa vibaya ni pamoja na mahindi, nyanya, kabichi, bamia na tikitiki maji.

Mifugo kutoka Wilaya hiyo ya Simanjiro imekuwa ikifanya uharibifu mkubwa wa mazao yao kwa miaka minane mfululizo, bila kupatiwa ufumbuzi. 

Mifugo hiyo inadaiwa kutokea vijiji vya Magadini, Kiruwani, Msitu wa Tembo na kambi ya chokaa vilivyopo mkoa wa Manyara.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )