Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 23, 2018

Ndege ya Tanzania Air-Bus A220 Kutua Nchini Leo Saa nane Mchana

Ndege ya kwanza kati ndege mbili aina ya Air-Bus A220 zilizonunuliwa na Serikali ya Tanzania jana ilitua  Mjini Accra nchini Ghana ikiwa safarini kuja hapa nchini.

Ndege hiyo itawasili leo Jumapili Disemba 23,2018 majira ya saa 8:30 mchana na kupokelewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.

Balozi wa Tanzania nchini Nigeria ambaye pia anahudumia nchini Ghana Mhe. Muhidin Mboweto amesema ndege hiyo ilitua salama Mjini Accra Ghana na kuwa gumzo kwa kila aliyeiona ikiwa uwanja wa ndege.

“Wafanyakazi wa hapa uwanja wa ndege na baadhi ya abiria baada ya kutangaziwa kuwasili kwa ndege hii aina ya A220 wamekuwa na shauku kubwa ya kuiona na kwa kweli ni ndege nzuri inapendeza na inawavutia zaidi kumuona Twiga na jina la nchi yetu Tanzania ambalo lina sifa kubwa duniani” amesema Balozi Mboweto.

Balozi amesema Watanzania waishio Nigeria na Ghana wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano na Mhe. Rais Magufuli kwa mafanikio haya makubwa ambayo yatasaidia kukuza uchumi kupitia usafiri wa anga, utalii na uwekezaji.

Ndege hiyo A220 iliondoka Montreal Canada juzi saa 1:00 Jioni kwa saa za Canada na ikatua visiwa vya Santa Maria saa 5:00 usiku kwa saa za huko.

Jana imetua Accra Ghana majira ya saa 4:00 kwa saa za Ghana na kupokelewa na Balozi Muhidin Mboweto wa Nigeria anayehudumia na Ghana.

Pamoja na marubani wa kampuni ya Air-Bus na Marubani wa Tanzania walioongoza katika safari ya ndege hiyo kuja nchini Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Mhandisi Ladislaus Matindi ndiye anaongoza safari ya ndege hiyo kutoka Canada hadi itakapowasili katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam leo   saa 8:30 mchana.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...