Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, December 28, 2018

Picha Ya Lemutuz Akiwa na Gari la Serikali Yaibua Gumzo Mtandaoni

Picha aliyoipiga Wiliam Malecela maarufu kama Lemutuz na kuposti katika mtandao wake wa kijamii ikimuonesha ameegemea gari la Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro na kuandika maneno ya kumshukuru kwa kumpatia usafiri huo, imeibua mijadala mbalimbali katika mitandao ya kijamii.
 
Jana Lemutuz aliposti picha mbili tofauti katika ukurasa wake
wa kijamii wa Instagram, moja ikimuonyesha akiwa amesimama na mdada aliyevaa koti la rangi ya kaki na nyingine ikimuonesha ameegemea gari la DC Muro.

Baada ya kuposti picha hiyo ambayo ilikuwa na maneno yafuatayo; “Thanks to God hatimaye nimefika salama at Masailand Safari Lodge...downtown Sakina/Arusha...I mean thank u ndugu yangu sana DC wa Arumeru JerryMuro kwa
kunipatia usafiri toka nilipofika mpaka hapa...I mean I am Super Humbled u know,” aliandika Lemutuz.
 Aidha baada ya picha hiyo na maneno hayo uliibuka mjadala katika mitandao ya kijamii ambapo watu mbalimbali walihoji sababu ya Lemutuz kuumia gari la Serikali kwa safari zake binafsi.
 
Hata hivyo muda mfupi baada ya kuibuka kwa mjadala huo, Lemutuz alidaiwa kubadilisha picha hiyo na kuweka picha ile ile lakini ikiwa na maneno mengine tofauti.
 
Katika posti ya pili Lemutuz aliandika;  “Thank God hatimaye
nimefika at Masailand Safariandlodge...I mean happy to meet you bro Jerrymuro1980...na thank u Masailand Safariandlodge kwa ukarimu wa ajabu sana...I am home here u know and I lov it,” aliandika.
Alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo, Muro alisema Lemutuz ni rafiki yake aliyekwenda jijini Arusha kwa ajili ya kutalii na yeye kama mwenyeji wake alikwenda hoteli aliyofikia kumsalimia.

“Masailand Hotel iko Sakina, Ngaramtoni ambayo ni wilaya yangu ya Arumeru na alikuja kwa ajili ya kutalii kama mtalii wa ndani na mimi nilikwenda pale kumsalimia na alipiga picha kwenye gari la umma yeye ni mwananchi na ana haki ya kupiga picha nalo,” alisema.

“Msifuate yanayoandikwa kwenye mitandao, wale ni wageni wangu nilikwenda kuwatembelea hotelini wakapiga picha na gari la serikali sasa si mali ya Muro. Lile ni gari la umma ni mali ya wananchi wanahaki nalo,” alisema.

Baadhi ya wachangiaji kwenye mitandao hiyo ya kijamii walihoji kubadilishwa maneno na picha ya awali iliyokuwa ikionyesha namba za STK na bendera ya taifa na kuwekwa picha mpya.

“Yaani unapata ujasiri wa kumpa rafiki yako gari la serikali tena bendera inapepea duu,” alihoji mmoja wa wachangiaji kwenye picha hiyo.
Advertisement
Loading...
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
==

taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Loading...