Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, December 1, 2018

Polisi Yaonya Wizi Mafuta Ujenzi Reli Ya Kisasa...."Tutakaye Mkamata Hatasahau Maisha Yake Yote"

Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi nchini limetangaza kuanza kwa Operesheni kali ya kuwabaini na kuwasaka watu wote wanaojihusisha na wizi wa mafuta katika mradi wa  ujenzi wa reli ya kisasa (SGR)unaoendelea kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Operesheni Maalum za Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi DCP Liberatus Sabas wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi wa reli hiyo katika kambi ya ujenzi ya Soga mkoani Pwani  na Ngerengere wakati wa ziara yake katika mradi huo  kufuatia kuwepo kwa vitendo vya wizi wa mafuta.

Sabas amesema Operesheni hiyo haitamwacha salama yeyote atakayekutwa akishiriki na kufanikisha vitendo vya wizi katika mradi huo na kuwataka wafanyakazi hao kuwa wa kwanza kutoa taarifa pindi waonapo viashiria vya wizi katika maeneo yao ili mradi huo uwe salama.

“Polisi tutatumia kila aina ya nguvu zetu kuhakikisha kuwa mradi huu unakuwa salama na tukikamata mwizi wa mafuta katika mradi huu hatasahau maisha yake yote kwa kuwa kuhujumu mradi huu muhimu kwa taifa ni kosa kubwa hasa ukizingatia gharama kubwa ambazo Serikali inatua kufanikisha jambo hili” Alisema Sabas.
 
Katika hatua nyingine DCP Sabas amewaelekeza Makamanda wa Polisi wa mikoa ya Pwani na Morogoro kuweka mikakati kabambe kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi Reli ili kufanya doria za mara kwa mara katika vijiji vinavyozunguka mradi huo kwa kuwa ndipo kulikobainika kuuzwa mafuta ya wizi wa mradi huo.
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )