Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

Rais Magufuli Asema Tanzania Itaendelea kushirikiana na Wadau wa Maendeleo

adv1
Na. Immaculate Makilika- MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli anasema kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wa maendeleo katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo  barabara na madaraja hatua inayolenga kuboresha maisha ya watanzania.

Akizungumza leo jijini Dar es salaam, Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa daraja jipya la Selander lenye urefu  wa kilomita 1.03 na barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 5.2, upana wa mita 20 na njia nne za magari pamoja na njia ya waenda kwa miguu yenye upana wa mita 2.5, alisema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau  wa maendeleo katika kuwaletea watanzania maendeleo.

“Tanzania itaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo ili kuwaletea maendeleo watanzania sambamba na kuhakikisha malengo na matumaini ya watanzania ya kuleta maendeleo tunayafikia kikamilifu” alisema Rais Magufuli

Pia, Rais Magufuli aliwataka watanzania kufanyakazi kwa bidii ili kufikia kiwango cha maendeleo cha nchi ya Korea ya kusini ambayo, katika miaka ya 1960 kiwango cha maendeleo kilikuwa sawa kati ya nchi hizo mbili.

“Tulikuwa tunalingana kiuchumi na nchi ya Korea ya kusini ambayo ina idadi ya watu milioni 51 na Tanzania  milioni 55,huku Tanzania ikiwa na eneo kubwa zaidi ya nchi ya Korea ya Kusini, lakini wao walijifunga mkanda na mpaka sasa wameweza kujitegemea kiuchumi kwa kufanyakazi kwa bidii na kujiletea maendeleo makubwa” alisema Rais Magufuli

Aidha, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale alisema kuwa daraja hilo  jipya la Selander litajengwa kwa fedha za mkopo nafuu kutoka nchi ya Korea kusini pamoja na fedha za ndani, ambapo litagharimu dola za kimarekani milioni 112.8 ambapo Korea ya kusini  itachangia dola za kimarekani milioni 91.03 na Tanzania itachangia dola za kimarekani milioni 21.822.

Vilevile, daraja hilo  litakuwa na urefu wa kilomita 1.03 na  barabara unganishi zenye urefu wa kilometa 5.2, upana wa mita 20 na njia nne za magari pamoja na njia ya waenda kwa miguu yenye upana wa mita 2.5, lengo likiwa ni kupunguza  msongamano wa magari katika barabara ya Ally Hassan Mwinyi.

Mhandisi Mfugale aliongeza kuwa daraja hilo litaweza kudumu kwa zaidi ya miaka 100 na linaweza kubeba uzito wa tani 180 kwa wakati mmoja.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkuu wa Benki ya Exim  nchini Tanzania, Hyon –Jong Lee alisema kuwa uhusiano wa Tanzania na Korea ya Kusini ulioanza miaka 26 iliyopita umezidi kuimarika, na kupitia Mfuko wa Shirika la Maendeleo la Korea kusini (ECDF), Korea imefadhili miradi ya Ujenzi wa chuo cha Mloganzila, daraja la Kikwete pamoja na Kituo cha kuchakata data cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).

Naye, Balozi wa Japan nchini Tanzania Cho Tae-ick alisema kuwa nchi ya Korea kusini inafurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kujiletea maendeleo

“Serikali ya Korea ya kusini inaangalia kwa makini fursa zilizopo Tanzania ikiwa ni nchi yenye uchumi unaokuwa kwa asilimia 7 na yenye sera kuelekea nchi ya viwanda, na hivyo Serikali Korea ya Kusini ina  nia ya dhati ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )