Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 2, 2018

Rais Magufuli awaonya wanaotaka kuzichonganisha Tanzania na Kenya

Rais wa Tanzania, John Magufuli amewataka wananchi wa Tanzania na Kenya kuendelea kushikamana na wasikubali kuchonganishwa katika masuala yanayolenga kuwatenganisha.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jana Jumamosi Desemba 1, 2018 wakati wa uzinduzi wa kituo cha huduma za forodha kilichopo katika mpaka wa Namanga mkoani Arusha.

Alisema wananchi wa mataifa hayo wanapaswa kuungana na kuwa kitu kimoja wakishirikiana katika harakati za kuleta maendeleo kwenye nchi zao.

“Sisi ni wamoja hata mimi na (Rais wa Kenya, Uhuru) Kenyatta ni marafiki hivyo hakuna sababu ya kuchukiana endeleeni kupendana, kusaidiana na kushikamana.”

“Asitokee mtu wa kuwachonganisha ipo siku viongozi tutaondoka au kubadilika lakini nyinyi mtaendelea kuwepo,” alisema Rais Magufuli.

“Najua kuna watu wanachomoka na kusema vineno vya ajabuajabu ila nawaambia washindwe na walegee Afrika Mashariki ni moja,” aliongeza.

Kwa upande wake, Rais Kenyatta alisema ipo haja kwa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki kuungana na kuweka mazingira bora ya kufanya biashara kinyume na hapo zitaendelea kuwa maskini.

“Tusipoungana nchi zetu zitaendelea kuwa maskini. Tuungane kwa kuwa na soko la pamoja litakalowezesha kuleta wawekezaji wakubwa ambao watakuwa kiini cha uwekezaji utakaozalisha ajira kwa vijana,” alisema.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )