Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, December 1, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 39

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
           
“Unaikumbuka sura ya mama yako vizuri?”
Swali la Ethan likanifanya nikae kimya kwa muda huku nikimtazama mama huyu.
“Hapana”
“Kwa nini umeamini kwamba huyu ni mama yako?”
“Ethan, moyoni mwangu, ninahisi kabisa sura ya mama yangu”
“Acha ujinga Ethan, ni watu wangapi weusi ambao una fanana nao, unataka kusema kwamba ni ndugu zako. Hapa umechezewa mchezo wa ajabu. Sasa ni hivi huyu sio mama yako, mumepumbazwa na unapo pelekwa ni kufilisiwa kila kitu chako na utabambikiwa kesi ya mauaji umenielewa”
Maneno ya Ethan kidogo yakanifanya nishikwe na bumbuwazi huku nikimtazama usoni mwake, kwani haya anayo nieleza sijawahi kuyafikiria kabisa kwenye akili yangu.

ENDELEA   
“Nani amepanga kunibambikia kesi?”
“Utajua, ila ukweli ni kwamba huyu si mama yako. Kitu kingine ninacho kihitaji Ethan sasa hivi usifanye maamuzi makubwa pasipo kunishirikisha. Muda mwengine ninakuja kukusaidia kwa sababu wewe ni rafiki yangu, ila nikiama kukaa mbali nawe basi nitakaa na utashindwa kwneye kila jambo. Umenielewa?”
 
Ethan alizungumza kwa msisitizo huku  akinitazama usoni mwangu.
“Nimekuelewa kabisa sinto rudia makosa”
“Yaa napenda kusikia hivyo. Sasa hivi nenda katafute hoteli, lala kesho urudi kambini”
“Sawa”
Ethana akapotea na kuniacha peke yangu katika chumba hichi. Nikamtazama mwana mama huyu kwa macho makali sana, nikatoka ndani humu na nikakutana na Camila mlangoni.
 
“Vipi mume wangu”
“Twende zetu hotelini”
“Hotelini tena?”
“Ndio, nahitaji kwenda kupumzika”
“Ila mbona kama unaonekana kama umekasirika”
“Twende nyumbani”
Nilizungumza kwa msisitozo mkali sana na kumfanya Camila kukubaliana na kile nilicho mueleza. Tukatoka katika eneo hili na walinzi wawili wakatangulia mbele yetu huku walinzi wengine wawili wakiwa nyuma yetu. Wakatufunguli mlango wa gari na  tukaingia ndani kisha taratibu tukaanza kuondoka katika eneo hili.
 
“Ethana mbona sijakuelewa kabisa, kwa nini umetaka tumuache mama pake yake kule hospitalini?”
“Sio mama yangu”
“Samahani, sijakuelewa?”
“Si mama yangu, hujanielewa nini?”
Nilizungumza kwa hasira kidogo na kumfanya Camila kukaa kimya. Camila akawaelekeza walinzi watupeleke katika hoteli nzuri na yenye ulinzi. Tukafika katika hoteli yenye hadthi ya nyota tano, Camila akatumia kadi yake maalumu ya malipo kulipia moja ya chumba cha kisasa kisha tukaelekea ndani.
“Ethan muda ule nilishindwa kuliongelea hili swala kwa urefu. Hembu niambie yule si mama yako kivipi, ikiwa ulisha sema ni mama yako?”
 
“Kuna mchezo ambao unachezwa hapa na wajinga”
“Mchezo gani?”
“Hadi hivi sasa mimi siukumbuki. Nimeweze kumtazama yule mama na kutafuta alama ambazo nilikuwa ninamuona nazo mama yangu, ila sijafanikiwa kuweza kuziona, hivyo wana nidanganya”
Ilibidi nimuongopee Camila.
“Mmmm ni kina nani hao lakini?”
“Si wale jamaa?”
“Jamaa wapi?”
“Mmoja wao ni yule mzee amabaye alinionyesha picha za huyu mwana mama akiniaminisha kwamba ni mama yangu ila ukweli ni kwamba si mama yangu”
 
“Mmmmm”
“Ndio Camila, kuna watu wana mpango wa kunifilisi na kunibamikia makesi ya ajabu. Endapo nitawajua haki ya Mungu nitafanya jambo moja baya snaa kwao”
“Mume wangu usiipe hasira nafasi ya kutawala moyo wako. Tafadhali na nakuomba uwe mvumilivu. Naamini huko mbeleni tutajua ni nani mbaya kwako na nani ni mzuri kwako. Ila tafadhali nakuomba uwe makini na kila mtu wa karibu yako”
 
“Ikiwemo wewe”
Jibu langu likamduwaza Camila, nikavua viatu na kujitupa kitandani. Mwili wangu kwa namna moja ama nyingine umechoka sana, toka asubuhi sikuweza kupata hata muda mzuri wa kupumzika. Camila taratibu akapanda kitandani huku akiwa mnyonge sana.
“Ethan”
“Mmmmm”
“Natambua ya kwamba una huzuni kubwa sana moyoni mwako. Natambua kwamba kitendo nilicho kufanyia hadi  sasa hivi bado hakijafutika akilini mwako. Ila tambua kwamba kila jambo nililo kuwa nimelifanya kwako kwa kipindi cha nyuma hazikuwa akili zangu. Nakuomba unisamehe Ethan”
“Nimekusamehe. Tule tulale”
 
Camilaakaandaa chakula huku akionyesha dhairi kwamba hana furaha kabisa. Tukapata chakula, tukaingia bafuni kwa pamoja, tukaoga kisha tukarudi chumbani na kulala pasipo hata mmoja kudhubutu kunyanyua hisia za mwezake.
    Asubuhi na mapema tukaanza safari ya urudi kambini. Msafara wa gari hizi tatu huku gari letu likiwa katikati, ukazidi kusonga mbele. Meseji ikaingia kwenye simu yangu. Nikaifungua na kukuta ikiwa imetoka kwa mwanasheria.
‘NIPO HOSPITALINI MADAKTARI WANADAI HAUPO MKUU, UPO WAPI?’
Nikaitazama meseji hii kwa muda, kisha nikampigia mwana sheria.
“Ndio mkuu za asubuhi?”
“Salama, sasa ni hivi”
“Ndio”
 
“Hakikisha unasimamia matibabu ya mwana mama huyo hadi anapona. Kisha arudishwe nchini Tanzania akaendelee na maisha yake”
“Ahaa….samahani mkuu, kwa nini umechukua maamuzi hayo?”
“Ni maamuzi yangu binafsi nahitaji akipona. Umpatie dola elfu hamsini, akaanzie maisha Tanzania. Mambo mengine nitakueleza muda ukifika wa kuyazungumza”
“Sawa mkuu nimekuelewa”
“Nashukuru”
Nikakata simu na kuirudisha mfukoni.
“Ethan”
“Mmmm”
“Haya maisha yetu ya kukaa kimya ya kuto kuzungumza, kununiana hakika mimi siyapendi mume wangu”
“Kwani Camila nimekununia?”
 
“Ndio, jana usiku, tumelala kila mtu amegeukia kwake. Leo asubuhi, tumeamka hata busu la hasubuhi hatukupeana, kila mmoja ameamua kufanya anacho taka kwa nini lakini”
Camila alizungumza kwa sauti iliyo jaa malalamiko, nikawatazama walinzi wawili walio kaa siti ya mbele huku mmoja akiwa ni dereva.
“Sijakukasirikia mke wangu, ila ninakasirika huu mchezo unao endelea”
“Sawa, ila tambua kwamba mimi ni mke wako”
“Natambua hilo na nitazidi kulitambua, ila na wewe unatakiwa kunibembeleza ukiniona nikiwa katka hali kama hii”
“Nitakubembeleza vipi ikiwa mwenyewe unanijibu vibaya”
“Sa…..”
 
Hata kabla sijaimalizia kauli yangu, dereva akayumbisha gari letu, huku akilikwepa gari la mbele lililo tutatungulia ambali, tunalishuhudia jinsi lilivyo paishwa angani kwa kulipuliwa na bomu moja kubwa na likatua chini na kusambaratika. Dereva wa gari letu akajitahidi kwa kadri ya uwezo wako kuliweka gari sawa, huku dereva wa gari la nyuma, akitutipa kwa kasi sana na kutangulia mbele yetu. Gari hizi mbili zilizo salia zikasimama, huku eneo hili tulilopo ni eneo la barabara za juu, katikati na chini. Ubaya wa barabara yuliyopo ni katikati, eneo ambalo huwezi kujirusha kwenda sehemu yoyote.
Watu walio valia nguo nyeusi, huku wakiwa na pikipiki kubwa, wakasimama mita kadha kutoka gari hizi zilipo na wakaanza kuzishambulia.
 
Walinzi kama jukumu lao la kutulinda, wakaanza kushuka kwenye magari haya na kujibu mashambulizi. Mimi na Camila miili yetu ina tetemeka kupita maelezo.
“Ohoo Mungu wangu”
Nilizungumza huku nikiendelea kushuhudia jinsi walinzi wanavyo zidi kupungua. Kwa haraka nikafungua mkanda wa siti niliyo kalia na kuahamia siti ya mbele ambayo mlinzi wake ameshuka kupambana na wavamizi hawa.
“Unafanyaje Ethan?”
Camila alizungumza huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.
“Kaa hapo hapo”
Nilizungumza, huku nikikaa kwenye siti ya dereva ambaye tayari amepigwa risasi ya kichwa na kufa. Wavamizi wakazidi kutusogelea huku wakizidi kuwapukutisha walinzi wetu. Mlinzi aliye salia naye akapigwa risasi na kutufanya tubaki sisi kama sisi.
 
‘Lazima nifanye jambo hapa’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikifunga mlango ambao alishuka mlinzi. Nikaokota bastola moja ya dereva, kisha nikaufunga mlango kwa nguvu. Risasi zinazo pigwa kwenye kuelekea lilipo gari letu haziingii ndani ya gari kutokana gari hili limetengenezwa kwa mfumo wa kuto kuingiza risasi.
“Ethan unafanya nini mume wangu”
 
“Lala kwenye siti”
Nilizungumza huku nikilirudisha gari hili nyuma, mnikaligeuza kwa kasi sana hadi likakaribia kuanguka. Nikaingiza gia namba moja gari likanza kusonga mbele taratibu, nikazidi kuongeza gia za garihili na kulifanya lizidi kuongezeka mwendo. Kupitia kioo cha pembeni, nikashuhudia kuona wavamizi hawa wenye pikipiki zipatazo saba wakituandama huku kwenye kila pikipiki wakiwa wamepanda wawili wawili. Camila akajaribu kuchungulia ila kwa jinsi kioo cha nyuma kinavyo shabuliwa kwa risasi na kusababisha alama nyingi nyingi, nikajikuta nikimfokea Camila na kumuomba alale chini. Sikuwa na budi ya kukwepa magari ninayo kutana nayo, kwani barabara hii inaruhusu magari ya kwenda upande mmoja tu ambao tulikuwa tunauelekea.
“Ni kina nani Ethan?”
“Sifahamu Camila”
Risasi zikazidi kumiminika na mbaya zaidi watu hawa ni wataalamu wa kuendesha pikipiki, kisha cha kunifanya hata niendeshe gari vipi, wana zidi kunisogelea.
‘Ethan naomba msaada wako’
Nilizungumza kimoyo moyo, ila sikuweza kupata msaada wowote wa Ethan. Nikafika katika barabara ya kugeza ambayo inapita eneo la chini, nikakanyaga breki kidogo, huku nikikunja kona hii kali na kulifanya gari liserereke, na kujibamiza kwenye vymba vikubwa vilivyo jengewa pembezoni mwa barabara hii kisha likaa sawa na tukaondoka katika eneo hili kwa mwendo wa kasi.
“Ethan”
“Mmmm”
“Naomba bastola”
“Bastola ya nini?”
“Kuna hawa wanatusogelea?”
Camila alizungumza huku akijipangusa machozi usoni mwake. Nikatazama kioo cha pembeni yangu nan ikawaona wavamizi wawili wakiwa wanatukaribia kabisa. Nikafunga breki za gafla na kuwafanya mmoja wao kugonga pipiki hii kwa nyuma na kusababisha ajali moja mbaya sana.
 
“Njoo uendeshe”
Nilizungumza huku nikuhamia siti ya nyuma kwa haraka, tukapishana na Camila kama upepo kwani hapa tunapigania maisha yetu kama wapenzi. Akaka kwenye siti ya dereva kisha akaliondoa gari hili kwa kasi sana. Nikaikoki bastola hii vizuri huku nikitazama pikipiki zinazo kuja. Kioo hichi cha nyuma hakika kimejaa alama nyingi za risasi hadi zinasababisha kuto kuweza kuona vizuri nyuma na kimebakisha asilimia ndogo sana kitoboke na kuruhusu risasi kuweza kuingia ndani ya gari hili.
“Ongeza mwendo Camila”   
“Najitahidi”
 
Nikafungua kioo kidogo kisha nikautoa mkono wnagu wa kushoto ulio shika bastola na nikaanza kufyatua risasi kadhaa kuelekea nyuma.
“Ethana una fanya nini!?”
“Nawazui wasitukaribie”
“Ohoo Mungu wangu”
Camila alizungumza huku akijitahidi kufunga breki za gari hili hadi nikarumbishwa na kujipigiza katika siti pembeni yangu. Nikatazama mbele na kushuhudia lori moja kubwa sana likiwa limeziba njia na mbaya sana zaidi tupo kwenye barabara aina ya karabati na eneo hili linawashwa taa masaa ishirini na la sivyo kuna kuwa na giza moja zito sana.
“Ni mtego mpenzi wangu”
 
Nilizungumza huki nikikaa sawa, nikafunga kioo nilicho kuwa nimekifungua kidogo. Juu ya lori hili tukaona watu wawili nao wakiwa wamevalia nguo nyeusi huku mikononi mwao wakiwa wameshika mabomu aina ya bazooka ambayo laiti wakiyafyatulia kwenye gari letu basi, gari litanyanyuliwa kama vile lilivyo nyanyuliwa gari la walinzi wetu lililo kuwa limetangulia mbele.
 
“Camila”
“Mmmm”
“Usifanye kitu chochote hawa watu wanahitaji sisi tukiwa wazima”
“Ethan tuna kufa mume wangu”
“Hatuwezi kufa, niamini mimi na tutoke kwenye gari”
Nilizungumza huku nikishuhudia wavamizi wenye pikipiki wakisimamisha pikipiki zao nyuma yetu. Ubaya watu hawa wamejifunika sura zao jambo la kushindwa kumtambua nani ni nani. Wakatuamrisha kushuka kwenye gari huku mikono yetu ikiwa ipo juu. 

Nikamkonyeza Camila nikimuashiria tufanye kama tulivyo agizwa, kwa haraka Camila akaninyonya lipsi zangu huku machozi yakimwagika usoni mwake, taratibu na mimi machozi yakaanza kunimwagika. Nikazitoa lipsi zangu kwa Camila kisha nikafungua mlango wa gari hili na nikawa wa kwanza kushuka huku watu hawa wakianza kunisogelea kwa ukaribu sana, akafwatia Camila naye akashuka huku akitetemeka sana. Jamaa hawa wakatunyooshea mitutu yao ya bunduki, wakazikoki vizuri tayar kwa kutuua jambo lilizo tufanya tuzidi kujawa na hofu kubwa sana.

==>>ITAENDELEA
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

taboola apo chini
Loading...
....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )