Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 3, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 40

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
             
Wakatuamrisha kushuka kwenye gari huku mikono yetu ikiwa ipo juu. Nikamkonyeza Camila nikimuashiria tufanye kama tulivyo agizwa, kwa haraka Camila akaninyonya lipsi zangu huku machozi yakimwagika usoni mwake, taratibu na mimi machozi yakaanza kunimwagika. Nikazitoa lipsi zangu kwa Camila kisha nikafungua mlango wa gari hili na nikawa wa kwanza kushuka huku watu hawa wakianza kunisogelea kwa ukaribu sana, akafwatia Camila naye akashuka huku akitetemeka sana. Jamaa hawa wakatunyooshea mitutu yao ya bunduki, wakazikoki vizuri tayaru kwa kutuua jambo lilizo tufanya tuzidi kujawa na hofu kubwa sana.

ENDELEA
Mmoja wa watu hawa akanisogelea na kunipokonya bastola niliyo ishika huku mikono yangu ikiwa juu. Akanipiga kwa kutumia kitako cha bunduki kifuani mwangu na kujikuta nikianguka chini mzima mzima huku nikihisi maumivu makali sana. 

Wakamvisha Camila kigunia cheusi kichwani mwake huku wakimfunga mikono yake na pingua, japo Camila alijitahidi kurusha rusha miguu na mikono yake, ila hakuweza kuzuia watekaji hawa kutimiza azima yao. 

Wakaninyanyua na mimi, jamaa mmoja akanipiga ngumi ya kifuani mwangu na kujikuta nikigugumia kwa maumivu makali sana. Wakanifunga mikono yangu kwa nyuma kwa kutumia pingu, kisha nami wakanivisha kigunia cheusi ambacho kikanizuia kuweza kuona ni kitu gani ambacho kinaendelea. Nikasukumiwa ndani ya gari ambalo sifahamu ni gari gani.
 
“Camila, Camila”
Niliita ila nikastukia nikipigwa teke la kifuani mwangu.
“Kaaa kimya pumbavu wewe”
Niliisikia sauti ya kiume ikifoka, sikuhitaji kuendelea kupata matatizo zaidi ya kuendelea kukaa kimya kwa maana watu hawa sihitaji waendele kunidhuru zaidi.
‘Ethna upo wapi rafiki yangu’
 
Nililamama huku nikiwa nimelala chini kwa kujikunja ndani ya gari hili ambalo inaonyesha ni lori kubwa sana. Baada ya kama ya saa moja na nusu, nikasikia breki za lori hili, likasimama, watu hawa walio tuteka wakanikamata mikono yangu, wakaninyanyua na kunishusha ndani ya lori hili. 

Nikaanza kutembezwa mkuku mkuku, nikakalishwa kwenye moja ya kiti kisha kigunia nilicho vishwa kichwani mwangu nikavuliwa. Mwanga mkali wa taa yenye mwanga mweupe ikanipiga machoni mwangu, jambo lililo sababisha niyafumbe macho yangu kwani ni maaumivu makali sana ninayo yapata yatokanayo na mwanga huo. Baada ya kumulikwa na taa hizi zenye mwanga mkali kama dakika tano hivi, wakazizima na kuyafanya macho yangu kujaa mawenge mawenge mengi kidogo.
 
Nikamuona Camila akiwa amekalishwa kwenye kiti cha mbele yangu huku akimwagikwa na machozi mengi sana usoni mwake. Mdomoni mwake wamamfunga kitambaa cheusi ambacho sio rahi kwa yeye kuweza kutoa sauti. Pembeni yake wamesimama watu wawili walio shika mitutu ya bunduki.
“Halooo Ethan”
Nilisikia sauti mbaya na nzito ikizungumza huku ikitokea kwenye kipaza sauti kidogo kilicho fungwa pembeni yetu.
“Munataka nini nyinyi wana haramu?”
 Nilizungumza kwa hasira huku nikijitahidi kujitoa mikono yangu kwenye pingu hii.
“Hahaaaa……ni jambo dogo sana tunataka kutoka kwako”
“Zungumzeni basi nipo tayari kuwapatia, ila mke wangu awe salama”
“Hahaaaa…..mke wako hausiani na kile ambacho tunakihitaji kutoka kwako”
 
“Tunahitaji boksi jeusi na Camila tunahitaji baba yako asigombanie uraisi wa hii nchi, ahakikishe anajitoa kwenye kinyang’anyiro hichi mara moja la sivyo tutaikata shingo yako”
Sauti hii iliendelea kutoa kauli ambazo hakika zinatisha.
“Niueni ila sifahamu ni wapi lilipo boksi jeusi”
“Ohoo tukuue”
“Ndio”
Camila akaanza kutingisha kichwa huku akigugumia kwa kulia, maamuzi nilio amua kuyachukua ni magumu sana. Maamuzi ambayo hakika yatamuacha na upweke katika kipindi chote cha maisha yake.
 
“Mpigeni risasi afe”
Sauti hiyo ilizungumza na watu wawili wakasimama mbele yangu huku wakiwa wameshika mitutu yao ya bunduki.
‘Nimekuja’
Niliisikia sauti ya Ethan ndani yangu, mwili wangu ukapata msisimko mmoja wa ajabu, pingu nilizo fungwa mikono mwangu zote zikakatika, nikasimama kwa haraka sana, nikawawahi watu hawa wawili, kwenye shingo zao, nikawanyanyua juu kwa mikoano yangu, kisha nikawarusha walipo simama watu walio mzingira Camila na kusababisha watu wengine kuanza kunishambulia kwa risasi. Kasi iliomo mwilini mwangu na uwezo alio nipatia Ethan, ukanifanya niweze kukwepa risasi zote ambazo wananishambulia.
 
Nikazivunja pingu za Camila za mikononi na nikaifungua miguu yake kisha yeye akamalizia kufujifungua kitambaa cha mdomoni mwake. Camila hakuhitaji kuwa mzembe, akaokota moja ya bunduki na kuanza kuwashambulia watu wengine huku nami nikiwa na kazi ya kutumia nguvu nilizo pewa na Ethan kuwanja vunja viuongo vyao watu hawa. Ndani ya dakika tano watu wote waliomo ndani ya holi hili, tukawabadilisha majina na kuwa ni marehemu. Camila akanikumbatia kwa haraka huku akiwa analia.
 
“Imekwisha baby”
Nilizungumza huku nikiendelea kumkumbatia Camila kwa nguvu sana.
‘Muhusika ana kimbia toka nje’
Niliisikia sauti ya Ethan, nikamuachia Camila na kwa haraka nikaanza kukimbia kueleekea nje, nikakuta gari moja nyeusi aina ya Lexus ikioandoka kwa kasi eneo hili, nikaangza huku na huku na nikaona moja ya pikipiki. Nikaifwata na kwa bahati nzuri nikakuta ikiwa na funguo, nikaiwasha kabla ya sijaondoka, nikamuona Camila akitoka katika holi huku akiwa na bastola mbili mikononi mwake.
 
“Njoo upande”
Nilimuambia huku nikitazama gari hii jisni inavyo timua vumbi. Camila kwa haraka akaokota heliment mbili za pikipiki, akanirushia moja kisha naye akavaa jengine, na kupanda kwenye hii pikipiki. Nikatia gia na kuanza kufukuzia gari hili. Uzuri wa pikipiki hii ina ina spidi mita mia mbili na ijini yake ni kubwa kiasi cha kuifanya iweze kushindana mwendo kasi na gari hili linalo zidi kwenda kwa kasi katika barabara hii ya vumbi.
“Ongeza mwendo”
Camila alizungumza huku akiwa ameizungusha mikono yake kiunoni mwangu.
“Poa poa”
Nilizungumza huku nikiongeza mwendo kasi wa pikipiki  hii kutoka mia moja na stini hadi kuanza kukaribia spidi mita mia mbil, jambo lililo sababisha taa ndogo nyekundu kuanzza kuwaka pembeni ya dashbod ya spidimita.
 
Tukaanza kulikaribia gari hili, Camila akanishika mkono mmoja kiuno changu, huku mkono wake mwengine akiuweka begani mwangu huku akiielekezea bastola aliyo  ishika kwenye gari hilo. Akaanza kufyatua risasi kadhaa kueleke kwenye gari hilo, baadhi ya risasi zikazipiga  gari hili kwa nyuma na kusababisha lianze kuyumba na likapoteza dira na kuvamia miti iliyopo pembezoni mwa eneo hili ambalo ni nje kabisa ya mjini. Nikaanza kupunguka mwendo mara baara ya kulishuhudia gari hili likipinduka matairi juu kichwa chini. Nikasisimamisha pikipiki hii mita chache kutoka eneo la ajali, tukashuka huku tukivua heliment za pikipiki hii.
 
“Nisubirie hapa”
Nilimuambia Camila huku akinikabidhi bastola moja.
“Etha…..”
Nikamtazama kwa macho makali ambayo yaliweza kumpa ishara ya kunyamaza kimya. Nikaanza kutembea kwa umakini sana kuelekea kwenye gari hili, nikamuona dereva akijivuta pembeni akitokea kwenye gari hili huku akiwa analalamika maumivu ya kuvujika mguu. Nikachungulia siti ya nyuma napo nikaona kuna mtu, nikamfungua mlango wa gari hili na kuanza kuivuta miguu ya mtu huyu ambaye sura yake bado sijaiona.
 
Nikastuka sana mara baada ya kuiona sura ya mwanasheria wa kampuni zangu. Mtu ambaye nimemuamini kwa maisha yangu. Mtu ambaye anafahamu siri zangu nyingi sana na hata baadhi ya makampuni yangu anayaongoza yeye.
“Nilikuambia utulie utaona, umejionea sasa?”
Ethan alizungumza huku akiwa amekaa pembeni yangu. Mwili mzima nikaihisi ukinyon’onyea sana. Camila uvumilivu ukamshinda na nikaanza kumuona akija katika eneo hili.
“Camila atakuona”
“Yaa inabidi anione, bila mimi musinge kuwepo hapa. Naamini leo ndio mara yake ya pili ataniona”
Ethan alizungumza huku tukimtazama Camila aliye karibia kufika hapa. Camila alipo muona Ethana, kwa haraka akamnyooshea bastola.
 
“Ondoka pembeni ya mume wangu”
Camila alizungumza kwa ukali sana na kumfanya Ethan kuangua kicheko kikubwa kilicho jaa kejeli ndani yake.
“Nimesema ondoka nitakuua”
“Camila tulia”
“Siwezi kutulia huyo ndio muuaji. Aliwaua walinzi wangu siku ile”
“Ndio niliwaua, unataka kuniua na mimi si ndio”
“Nimesema usinijaribu, nitakuua”
Ethan kwa haraka akasimama mbele ya Camila jambo lililo nifanya nihitaji kupiga hatua moja mbele ila nikagundua adui yangu hadi sasa hivi sijajua amepoteza maisha au amezimia.
“Camila acha, huyu ni fariki yangu na yeye ndio aliye nipatia msaada kwenye maisha yangu”
 
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Camila usoni mwake. Uso nzima wa Camila umebadilika na kuwa mwekundu kwa hasira.
“Tafadhali mke wangu, sikikilize basi achana na Ethan njoo ushuhudie hili hapa”
“Msikilize mume wako, kwa maana mimi huwezi kuniua kwa maana si binadamu.”
“Si binadamu?”
“Wote acheni ujinga”
Ilinibidi nizungumze kwa kufoka na kuwafanya Camila na Ethan kunitazama.
“Tuna kazi ya kufanya, nahitaji kujua huyu mshenzi kama yupo hai au amekufa. Nyinyi mumekalia upuuzi sitaki ujinga”
Niliendelea kuzungumza kwa kufaka na kumfanya Camila kuishusha bastola yak echini taratibu. Nikakitazama kifua cha mwana sheria na nikakiona kikihema taratibu.
 
“Mpuuzi yupo hai huyu”
Nilizungumza huku nikimalizia kumvuta kutoka ndani ya gari. Nikamtazama dereva anaye endelea kulia kwa maumivu makali anayo yahisi. Nikamsogelea na kuchuchumaa pembeni yake.
“Unahisi maumivu si ndio?”
“Ehee….nisaidie….nisaidie tafadhali”
Nikasokomeza bastola yangu mdomoni mwake, akanitolea macho ya woga sana huku akinitazama usoni mwake. Nikafyatua risasi mbili mfululizo na kumfanya kichwa chake kichanguke kwa nyuma na damu zikaanza kutapakaa kwenye mchanga. Taratibu nikaichomo bastola yangu na kurudi eneo alipo mwana sheria ambaye amezungukwa na Ethan pamoja na Camila ambaye anashanga uwepo wa mwana sheria huyu  katika eneo hili.
 
“Ethan huyu si mwana sheria wako?”
“Ndio”
“Mbona yupo hapa?”
“Yeye ndio anahusika kwa kila kitu ulicho kiona leo”
“Ohoo Mungu wangu!!”
“Ethan unaweza kumuamsha?”
“Mmmmm nina weza”
“Muamshe”
Ethan akamshika mwana sheria eneo la shingoni mwake. Taratibu mwanasheria akafumbua macho yake. Ethan akamshika shat lake eneo la kufuani mwake na kumkalisha kitako huku akimuegemeza kwenye gari hili lililo pata ajali. Mwanasheria woga mwingi sana ukamtazama, hakutegemea kutuona hapa sisi watatu, kwa hasira niliyo nayo hadi nikajikuta nikikosa cha kuzungumza na mkono nilio shika bastola ukaanza kutetemeka.
 
“Kwa nini umefanya hivi?”
Nilijikaza kuzungumza ila mwana sheria akakosa cha kunijibu zaidi ya machozi kuendelea kumwagika.
“Haya ndio aliyo  kuagiza baba yangu uyafanye juu yangu si ndio?”
“N…..i…nii same….he…..Ethan”
Mwanasheria alizungumza huku akimwagikwa na machozi usoni mwake.
“Ethna nimefanya hivi kwa ajili ya familia yangu, kwa ajili ya mke wangu na mwanangu”
“Mke wako na mwanao ndio walio kuagiza kuniteka mimi na Camila na kunishinikiza vitu vya kijinga si ndio?”
“A….a…..!!”
Mwanasheria kigugumizi kikaendelea kumbana kifuani mwake.
“Nakuuliza mke wako ndio aliye kuagiza kufanya ujinga huu si ndio?”
“Nd….ndi….ooo”
“Mke wako ndio aliye taka utuue sisi na mume wangu, jamani mbona hana huruma. Tumemfanyia nini jamani ehee?”
Camila alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake.
 
 “Mke wangu anagombania kiti cha uraisi hawa pia ni watu wake aio nikabidhi kufanya nao kazi. Alinishawishi sana nikushawishi umuunge mkono, ila nikakataa  ndio maana akatumia nguvu hii.”
“Ina maana bi Magnalena Schoss ni mke wako?”
Camila aliuliza huku akimtazama mwana sheria usoni mwake.
“Ndio ni mke wangu  na tuna miaka thelethini sasa katika ndoa”
“Boksi jeusi alilihitaji la nini kwangu?”
“Eheeeee!!!”
Mwanasheri alijifanya kama hajasikia, nikampiga na kitako cha bastola kwenye ugoko wa mguu wake wa kushoto na kumfanya alie kwa uchungu sana huku akinitazama usoni mwangu.
 
“Alihitaji boski jeusi  kwa ajili gani?”
“Ni kwa ajili ya kujiimarisha kiusalama zaidi”
“Ahaa…..sawa sawa”
Nilizungumza huku nikiikoki bastola yangu na kumuelekezea kichwani, kama alitoa amri ya mimi kupigwa risasi basi na yeye hana nafasi ya kuishi hapa duniani.
“Ethan ngoja kwanza usimuue”
Ethan alizungumza huku akinitazama.
“Kwa nini?”           
“Kwa kumtumia huyu basi tutahakikisha huyo mwana mama anaenguliwa katika kasi za kugombania uraisi na itazidi kumpa nguvu baba mkwe wako kushinda uchaguzi wa uraisi”
Ethna alizungumza kwa upole, kabla sijafanya chochote simu ya mwanasheria huyu iliyopo kwenye koti lake la suti ikaanza kuita, nikampasa kwa haraka na nikaitoa. Nikakuta namba hiyo ni ya mke wake, nikamuonyesha kisha nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
“Mume fiki wapi mume wangu. Nipe habari njema”
“SIO HABARI NJEMA, NI HABARI MBAYA MUME WAKO AMEFARIKI DUNIANI”
Nilizungumza kwa sauti nzito na iliyo jaa mikwaruzo mingi sana na kumfanya mwana mama huyo kukaa kimya kwa sekunde kadhaa akisikilizia sauti yangu.

==>>ITAENDELEA KESHO
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )