Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 9, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 42

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
“Ni watu wa huyu mzee”
“Ohoo samahani mume wangu kwa kukuamisha kwamba ni watu wa serikali. Tukashuhudia helicopter nyingine nayo ikilipuka mlipuko mmoja mkali sana. Wanajeshi wanao tushambulia tukawashuhudia jinsi wanavyo anguka mmoja baada ya mwengine.
“Nilikuambia Ethan, hii vita si ndog….”
“Nyamaza nguruwe wewe”
Nilizungumza huku niligeuza gari hili kwa kasi sana, likayumba kidogo ila nikafanikiwa kuliweka sawa.
“Tupa hiyo simu ya huyo mzee”
Tuliisikia sauti ya Ethan akizungumza nasi, tukatazamana na Camila usoni mwetu. Nikaanza kujipapasa mifukoni mwangu na kuipata simu ya mzee huyu, nikashusha kioo kidogo na kuitupa dirishani na kuanza safari ya kutokomea sehemu ambayo kwa kweli hatuifahamu na hatujui ni nini hatima yetu na mwanasheria wangu huyu.

ENDELEA
“Tunakwenda wapi huku mume wangu?”
Camila alizungumza huku tukiendelea kufwatisha barabara ndogo iliyopo katikati ya msitu huu wenye miti mirefu kwenda juu na iliyo fungamana sana.
“Twende tu mke wangu, hatuwezi kurudi mjini kwa hali hii”
Meneja akakurupuka na kujikuta nikitazama nyuma alipo kaa. Nikamuona Ethan akiwa amekaa pembeni yake.
“Unaniogopa ehee?”
Ethan alizungumza huku akimshika meneja shati lake. Ethan akaniomba nisimamishe gari na nikafanya hivyo. Kwa ishara akaniomba nishuke kwenye gari ili tuweze kzungumza.
“Muangualie huyu”
 
Nilizungumza huku nikimtazama Camila, akanijibu kwa kutingisha kichwa huku akiwa ameishika bastola yake vizuri. Nikafunga mlango na tukazunguka nyuma ya gari hili.
“Hali ya usalama wenu sio nzuri rafiki yangu. Hali ni mbaya na munawindwa kuuwawa”
Ethan alizungumza kwa sauti ya upole sana
“Duuu na inakuwaje watu wa serikalini ndio wanahitaji kutuangamiza?”
“Raisi wa sasa hivi haitaji kuachia madaraka kwenye chama cha baba yako mkwe. Kumbuka kwamba huyu raisi chama chake ndio hicho anacho gombania huyo mke wa mwanasheria wako. Wewe kwa kumpa msaada wa kipesa wa asilimia hamsini, umewafanya wajenge uadui mkubwa sana. Hivyo wakiwaua wewe na Camila basi baba yake atajitoa kwenye kinyang’anyiro cha kugombani uraisi”
 
“Hii taarifa inabidi Camila aweze kuifahamu”
“Sawa”
Nikarudi upande wa siti ya Camila, nikamuomba ashuke kwenye gari huku akichomoa funguo za gari hili na tukaifunga milango. Tukasimama nyuma ya gari hili huku tukimtazama Ethan.
“Shemeji kuna swala hapa nahitai kukueleza, nilianza kumueleza Ethan kidogo akaona sio mbaya akakushirikisha na wewe”
“Swala gani?”
“Vita ambayo mupo nayo hivi sasa imeanzia serikalini. Lengo lao ni kuwaua nyinyi wawili ili kuhakikisha kwamba baba yenu anatoka kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi wa raisi”
“Ohoo Mungu wangu, kwa hiyo haya yanayo tokea hivi sasa ni kwasababu ya raisi huyu wa sasa?”
 
“Ndio”
“Sasa tutafanyaje jamani”
“Popote ambapo mutakuwa ndani ya hii nchi ni lazima muta uwawa kwa maana adui yetu anakuja kwa sura nyingi, mara wanajeshi mara hivi, hivyo hata mimi japo nina uwezo mkubwa, ila wananizidi akili sana na laiti ningekuwa mbali nanyi hawa wanejeshi wangewaua”
Nikashusha pumzi huku nikimtazama Ethan.
“Nina rafiki yangu mmoja yupo nchini Tanzania. Nitawasiliana naye kwa sasa ili aweze kuwasaidia kuwaficha huko. Naamini kwamba mashambulizi ya kumuangusha huyu mama kutoka madarakani itaanzia huko huko Tanzania sawa”
 
“Sawa shemeji ila uchaguzi umebakisha siku ishirini na hivi sasa baba tupo kwenye kampeni kweli si wanaweza kumdhuru”
“Hadi kumfikia baba yako ni kazi ngumu sana na ukumbuke kwamba baba yako anasaidiwa na babu yako ambaye naye alikuwa ni raisi wa hii nchi. Hivyo bado kuna nguvu ambayo aimeicha ndani ya serikali”
“Sawa nimekuelewa shemeji”
Ethan akatoa simu yake na kusogea pembeni.
“Sasa mume wangu kama tukielekea Tanzania, itakuwaje mama na dada yako?”
“Nina imani atawalinda kama anavyo tulinda nasi”
“Kweli?”
“Ndio”
Ethan mara baada ya kumaliza kuzungumza na simu akarejea sehemu tulipo.
 
“Nimesha zungumza naye. Mutaondoka hapa na helicopter hadi nchini Ufaransa. Kuanzia hapo mutaiaza safari ya kuelekea nchini Tanzania na huko mutapokelewa na mwana dada huyo”
“Sawa, sasa dada yangu na mama nina waacha huku itakuwaje rafiki yangu?”
“Nitakuwa nao pamoja na nimeweza kuweka hali ya wao kusahulika, hakuna adui ambaye anaweza kuwakumbuka hata mmoja”
“Ahaa, sawa.”
“Ila nitahitaji kuzungumza na mama pamoja na baba ili tuwatoe wasiwasi?”
“Kwa sasa si rahisi na salama kuzungumza nao. Mutazungumza nao kipindi mukifika nchini Tanzani, sawa”
“Sawa”
 
“Ingieni kwenye gari, sasa hivi nitawaendesha”
Nikamkabibidhi Ethan funguo, kisha mimi nikapanda siti ya nyuma na kukaa na mwanasheria huku Ethan na Camila wakikaa siti ya mbele.
Safari ikaendelea huku tukizidi kukatiza kwenye msitu huu. Mwanasheria mwili wake unamtetemeka kila anapo mtazama Ethan mwenzangu.
“Yaani sikuamini kama wewe unaweza kuja kuwa mtu ambye unaweza kuja kuniharibia maisha yangu na nimekuwa mkimbizi wa kukimbia kimbia katika nchi ambayo nimekuwa toka nilipo kuwa mtoto mdogo”
“Haya yote nimefnya kwa shinikizo, sio mimi, laiti kama ningekuwa ni mimi nisinge fanya hivi”
 
“Hiyo sio pointi ya kujitetea”
“Ethan huyo nitabaki naye mimi hapa Ujerumani”
“Sawa nashukuru, ila hakikisha anakuwa hai hadi pale anapo mshuhudia mke wake anavyo anguka na ikiwezekana anakwenda jela kwa kosa hili”
“Sawa”
Tukafika kwenye moja ya kiwanja kidogo ambacho kimezungukwa na miti. Tukakuta helicopter moja ya kifahari ikiwa katika eneo hili. Tukashuka ndani ya gari na kumuacha mwanasheria peke yake.
“Huyu mzee anatawapeleka hadi Ufaransa, mutapanda ndege na maelezo yote nimemueleza na tutawasiliana mukiwa ndani ya ndege”
“Sawa”
 
“Shem ni nani ambaye atatupokea huko?”
“Ohoo usijali shemeji, mukiwa kwenye ndege mutakabidhiwa kila kitu chenye melezo sawa”
“Sawa nashukuru shemeji yangu, ninaweza kukumbatia?”
Macho yakanitoka kidogo kwa ombi hilo la Camila kwa Ethan.
“Acha wivu. Unaweza kunikumbatia”
Ethan akapanua mikono yake kidogo na Camila akamkumbatia kwa nguvu sana.
“Imetosha sasa, kukumbatiana gani huko”
“Haahaaa haya”
Ethan alizungumza huku akimuachia Camila taratibu. Tukaanza kutembea na Ethan hadi  kwenye helicopter hii. Tukakuna na mzee mmoja wa kifaransa kwenye ndefu nyingi nyeupe.
“Anaitwa mzee Fransico. Mzee Fransico huyu ni Ethan wajina wangu na huyu ni Camila ni mpenzi wake”
“Nashukuru kwa kuwafahamu”
“Karibuni sana nimewajia na nguo za kubadilisha”
“Tunashukuru”
“Munaweza kuingia ndani ya helicopter mukabadilishia humo humo ndani”
 
“Sawa”
Mimi na Camila tukaingia ndani ya helicopter hii, tukakuta nguo kadhaa, nikavaa suti mija nyeusi yenye shati jeupe, huku Camila naye akivaa gauni moja refu la rangi ya nyeupe ila ina vimweko mweko ya dhahabu. Camila akaziweka nywele zake vizuri huku akivaa miwani moja nzuri ambayo kwa asilimia kubwa imebadilisha muonekano wake.
“Tayari”
Nilizungumza mara baada ya kufungua mlango wa helicopter hii.
“Ohoo umependeza sana wajina”
“Nashukuru ndugu yangu”
“Sawa, hati za kusafiria zote zipo tayari. Mzee atawakabidhi mukifika uwanja wa ndege”
“Poa”
 
Mzee Fransico akaingia kwenye helicopter hii upande wa rubani. Taratibu akawasha helicopter hii na tukaanza kuondoka katika eneo hili huku tukimpingia mkono Ethan ambaye tukamshuhudia akiingia kwenye gari na kuondoka eneo hili. Safari ya kuondoka nchini hapa Ujerumani ikaanza huku Camila akionekana kujawa na mawazo mengi sana kichwani mwake.
“Baby mbona una mawazo?”
“Namfikiria baba yangu, naondoka nchini kwangu pasipo hata kutegeme kama kweli ninaondoka muda huu”
“Ni kweli mke wangu, ila hili swala litakwisha nina imani kwamba baba akiingai madarakani kila jambo linaweza kwenda vizuri naamini atakuwa na nguvu ya kupigania hili jambo”
 
“Ni kweli ila nina ogopa sana”
“Usijali nipo karibu nawe”
Safari ya kuelekea nchini Ujerumani ikatuchukua masaa kadhaa hadi kufika katika kiwanja cha Paris Orl. Tukashuka kwenye helicopter ikiwa ni majira ya saa moja kasoro usiku, tukainagi kwenye ndege ya kukodi ambayo ni private jet.
“Ndani ya ndege kuna simu mbili na zina maelezo ya nani atawapokea mukifika nchini Tanzania. Hii ni card ya benk ambayo inaweza kutoa pesa katika nchi yoyote duniani. Ni Gold Master Card”
 
Mzee Fransico alizungumza huku akinitazama usoni mwangu.
“Nashukuru mzee”
“Ndani ya ndege kuna kila aina ya huduma ambayo mutahitaji na marubani wetu ni wawili. Mr Cosovo na Mis Anna.
“Tunashukuru kwa msaada wenu”
“Ndani ya akaunti kuna kiasi cha dola milioni tano za Kimarekani, hakikisheni kwamba munaitunza vizuri”
“Asante”
Tukaagana na mzee Fransico kisha tukaingia kwenye ndege hii ambayo abiri ni sisi wawili. Tukaa kwenye siti mbili nzuri, tukajifunga mikanda na taratibu ndege hii ikaanza kuondoka kwenye uwanja huu. 
 
“Nikupe matunda?”
“Ndio mke wangu”
Camila alizungumza huku akiwa amefungua friji ndogo iliyopo pembeni yake. Akatoa matunda mawili aina ya Apple.
“Sikutarajia kurudi nchini Tanzania leo”
“Ndio tunarudi mum wangu”
“Baada ya miaka kumi na mbili sasa nina rudi nchini kwangu”
“Kweli”
“Ndio, hembu naomba simu hapo nisome maelezo ya mpokeaji”
Camila akanikabidhi simu moja, nikaiwasha na kukutana na melezo ya jinsi ya kuifungua simu hii. Nikakutana na maelezo ya jinsi gani ninaweza kuifungua simu hii. Nikaanza kukutana na maelekezo ya kuifungua simu hii. Nikakuta picha ya msichana mmoja ambaye anaitwa Jojo Dany. Ni msichana mmoja mzuri na anaye vutia kwenye macho ya mwanaume.
“Mbona unashangaa sana”
 
“Huyu ndio msichana ambaye tunakwenda kukutana naye”
Nilizungumza huku nikimgeuzia Camila simu hii niliyo ishika.
“Sawa”
Camila aliitikia kinyonge.
“Ethan nahitaji kuzungumza na baba yangu”
“Sasa hivi?”
“Ndio mume wangu nahitaji kuzungumza naye”
Tukaitazama simu hii niliyo ishika, kisha nikamkabidhi Camila na akaingiza namba ya mkononi ya baba yake.
“Vipi simu inaita?”
“Ndio”
“Halo baba”
“Ohoo asante Mungu kwa kuisikia sauti yako”
“Nipo salama baba yangu, nina mshukuru Mungu, nipo kwenye ndege hivi sasa nina eleeka nchini Tanzania”
“Tutazungumza mambo mengi baba nikifika nchini humo”
“Nipo na Ethan, huu hapa zungumza  naye”
 
“Sawa”
Camila akanikabidhi simu huku usoni mwake akiwa amejawa na batasamu kidogo. Nikaipokea simu hii na kuiweka sikioni mwangu.
“Ndio mzee”
“Nashukuru kwa kuendelea kumlinda mwanangu, ila ninakuomba huko Tanzania munapo kwenda uhakikishe kwamba anakuwa salama”
“Nashukuru baba, ila nina imani kwamba unaelewa ni jambo gani ambalo linaendelea?”
“Ndio kuna kijana amenifwata kama masaa manne yaliyo pita na amenieleza kwa kila kila kile kinacho endelea kwa sasa”
“Sawa baba, nashukuru kwa kulifahamu, ila ninacho kuomba kuanzia hivi sasa jilinde, nahitaji uingie ikulu. Ukiingia ikuli tutakuwa tayari kurudi nchini Ujerumani”
“Sawa nitahakikisha kwamba ninaichukua nchi na maadui zangu wote watakwenda kulipa kwa hili jambo ambalo wamelifanya.”
“Sawa sawa”
“Ila kuna kitu kimoja ninaomba unisaidie baba mkwe”
“Kitu gani hicho mwanangu?”

==>>ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )