Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, December 16, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 45

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA

Jojo akatufwata hapa tulipo simama huku akiwa na sura ya tabasamu.
“Ethan”           
“Mmmm”
“Huna kumbukumbu yoyote na wazazi wako?”
“Ndio”
“Unahitaji kufahamu ni kitu gani kilicho wapata?”
“Ndio”
Jojo akanisogelea na kunishika kichwani mwangu, nikahisi ubaridi mkali ambao taratibu katika ufahamu wangu wa akili nikaanza kuona ngurumo za radi huku mvua nyingi ikinyesha. Kumbukumbu zangu zikazidi kusonga mbele na kumuona mzee mmoja akiwa amezungukwa na kundi kubwa la vijana huku  wakimshambulia kwa kumpiga kwa magongo pamoja na mateke huku wakihitaji afariki dunia.

ENDELEA
Nikamuona mama yangu akiwa amejificha kwenye migomba pamoja nami huku akilia. Radi iliyo piga yenye mwanga mkubwa, ikanifanya niweze kumuona mwanaume mmoja ambaye baada ya kuiona sura yake nikajikuta nikistuka sana.
“Vipi?”
Dany aliniuliza hukua kinitazama usoni mwangu. Nikashindwa kulijibu swali lake kwani mapigo yangu ya moyo yananienda kasi huku jasho likinimwagika usoni mwangu.
“Kuna nini kinacho endelea hapa”
Camila alizungumza mara baada ya kufika hapa tulupo simama. Nikawatazama watu wote hawa kisha nikaondoka na kuanza kuelekea kwenye gari tulipo liacha.
“Ethan, Ethan”
Camila aliniita, sikuweza kumuita zaidi ya kuzidi kusonga mbele. Nikajaribu kufungua mlango wa gari ila haukufunguka.
“Ethna mume wangu kuna kitu gani kinacho endelea?”
Camila alizungumza huku akinishika mkono.
“Nimemuona”
“Umemuoan nani?”
“Mtu aliye niulia baba na mama yangu”
Camila macho yakamtoka kwa maana hakuamini kama ninaweza kukumbuka  vitu hivi kwa muda huu.
“Ni nani?”
 
“Simfahamu jina lake, ila nimeikumbuka sura yake”
“Ohoo jamani mpenzi wangu, tulia kidogo”
Camila alizungumza huku akinikumbatia mwilini mwangu. Dany na Jojo wakanifwata sehemu hii tulipo simama.
“Ethan umeona nini?”
Jojo aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Nimemuona mtu aliye niulia baba na mama yangu”
“Una uhakika?”
“Ndio”
“Twendeni ndani jamani”
Dany alishauri na kutufanya mimi na Jojo kumtazama. Dany akaanza kuongoza kuelekea ndani, nasi tukaanza kumfwata kwa nyuma. Tukaelekea eneo lenye kiwanja kikubwa cha mpira. Tukakutatimu ya vijana chini ya miaka kumi na nane wakifanya mazoezi katika eneo hili. Baadhi ya watu nao wamejumuika katika kuitazama timu hii. Tukakaa katika moja ya sehemu ambayo tunaweza kuona mazoezi yao vizuri sana.
“Ethan”
“Naam”
“Mtu huyo anafananiaje?”
Nikamtazama Jojo huku nikijaribu kuvuta kumbukumbu yake, kitu kilicho nishangaza, sikuweza kuipata kumbukumbu yake tena.
 
“Mbona simkumbuki”
“Humkumbuki?”
“Ndio”
“Ngoja”
Jojo alizungumza huku akinishika kichwani mwangu, nikaanza kuoana jinsi mwanaume huyo alivyo toa amri ya sisi kukimbizwa pamoja na mama yangu. Mama akajitahidi kukimbia kwa kuchechemea huku akiniongelesha kwa lugha ya kichaga kwamba tukimbie. Kutokana na utoto wangu nikakimbia hadi kwenye migomba mingi ila nikashindwa kuendelea na kukimbia, nikarudi sehemu alipo mama yangu na kukuta akitaka kubakwa na vijana walio kuwa akitukimbiza. Vijana wawili wakaninyanyua juu juu na kunipeleka hadi kwenye korongo. Kitendo cha kujigonga kichwa changu kwenye jabali nikakurupuka tena huku nikishika kichwa changu upende ambao nilijibamiza kwenye korongo.
 
“Vipi umeona nini?”
Nikashusha pumzi taratibu huku nikimtazama Jojo usoni mwake.
“Nimeona jinsi mama alivyo kuwa akibakwa na mimi nikapigwa na kusukumia kwenye korongo”
“Hujamuona tena huyo mtu?”
“Hapana”
“Ukimuona picha je utamkumbuka?”
“Nahisi, ila kumuelezea kwamba yupo vipi siwezi kwa kweli”
“Chukua muda wa kutosha ukimkumbuka basi utanifahamisha sawa”
“Sawa”
Camila akanisogelea karibu yangu na kunishika mkono wangu na kukiegemesha kichwa chake karibu yangu.
“Unajisikiaje mume wangu?”
 
“Sasa nimejitambua mimi ni nani?”
“Kivipi?”
“Jina langu sio Ethan mpenzi wangu”
“Mmmmmm?”
“Yaa jina langu sio Ethan, jina hilo nimepewa ila sio lile nililo pewa na wazazi wangu”
Camila akabaki akiwa na mshangao mkubwa sana huku akinitazama usoni mwangu.
“Jina lako halisi ni lipi?”
“Naitwa LOLE, hilo ndio jina langu katika kabila langu la Kichaga”
“Wachaga ni watu wa wapi?”
“Moshi”
Camila akaka kimya huku akinitazama usoni mwangu akionekana kutafakari haya mambo niliyo mueleza.
“Lole sinto kuita Ethan tena sawa mume wangu?”
“Nashukuru mke wangu”
Nikamkumbatia taratibu Camila, tukaendelea kutazama mazoezi ya wachezaji hawa, japo wana kocha ila yamejaa udhaifu mkubwa sana.
“Natamani nikawaelekeze kidogo mke wangu”
“Mazoezi!?”
 
“Ndio”
“Ohoo mume wangu wasije wakahitaji kukuchukua, kumbuka mambo yaliyo tutokea Ujerumani”
“Nawaelekeza kidogo, kidogo tu”
“Mmmm haya”
Nikamuachia Camila na kuanza kushuka ngazi na kuelekea uwanjani. Walinzi wanao linda wachezaji  hawa wakanizuia kuingia.
“Samahani kuna machache nahitaji kuzungumza na kocha, tafadhali ninaomba munisaidie katikahilo”
Mmlinzi mmoja akanikazia macho sana, kisha baada ya muda kidogo akatabasamu.
“Kama sijakosea wewe ni Ethan Klopp?”
“Yaa ndio mimi”
“Pita pita”
Mlinzi huyo alizungumza kwa furaha kubwa sana na kuwafaya wezake nao wajawe na furaha kwa maana hapo awali hawakuweza kunifahamu. Nikafika katika sehemu walipo simama makocha wawili mmoja akiwa ni kocha wa kizungu. Nikasalimiana nao kwa heshima sana, kwa bahati nzuri wakaweza kunifahamu kwa haraka sana.
 
“Ohoo Ethan upo Tanzania?”
Kocha huyu wa kizungu alizungumza huku akiwa amejawa na mshangao sana.
“Ndio nina siku ya pili sasa japo nimekuja Tanzania kwa siri sana”
“Ohoo karibu sana yaani nilikuwa ninatamani sana kukuita kwenye kikosi changu ila sikuweza kufahamu ni wapi nitakupata”
“Nimekuja kwenye mapumziko mafupi, ila nitaandoka”
“Oohoo sasa unataka kuniambia kwamba huto kuwepo kwenye fainali zinazo endelea Ujerumani?”
“Yaa sinto kuwepo kwenye kikosi, naamini kama ni mfwatiliaji wa mambo utaweza kugundua ni kitu gani ambacho kimetokea kwenye wiki za hivi karibuni”
“Yaa nafwatilia”
 
“Ndio maana nipo hapa. Kuna mambo kadhaa ambayo naomba niweze kuwaelekeza timu yako. Nimekaa juu kule nikaona mapungufu kadhaa. Sijui unaweza kunipa nafasi japo dakika kumi na tano nikafundisha vijana wako”
“Kwa nini usiingie ukacheza ndani?”
“Hapana, labda siku nyingine, ila leo nahitaji kutoa maelekezo madogo madogo ili tumu iwe vizuri”
“Sawa darasa ni lako”
Kocha akapiga  filimbi na wachezaji wote wakakusanyika sehemu tulipo simama sisi. Nikasalimiana na wachezaji hawa ambao nao wakaonekana kufurahi sana kwangu.
“Mimi ni Mtanzania kama nyinyi tena ni mchaka. Hivyo naomba musiwe na ile hali ya kuhisi labda mimi ni mtu maarufu au nimetokea Ujerumani, hivyo mukajihisi unyonge kwenye mioyo yao. Mimi sifahamu mengi sana kwenye mpira, ila kwa yale machache niliyo nayo, nimeona ni vyema tukabadilisha yote katika yote ni kuweza kuijenga timu yetu si ndio”
 
“Ndio ndio”
Nikaanza kuwapa mbinu washambuliaji pale wanapo kuwa uwanjani. Nikagawa timu hii mara mbili kisha nikasimama kama refarii. Wakaanza kucheza mpira kama vile nilivyo walekeza, ndani ya dakika kumi thelathini, wakacheza kwa kiwango cha hali ya juu hadi watu hawa walio kuja kushuhudia mazoezi haya wakaanza kushangilia kana kwamba wanatazama mechi ya wapinzani. Kutokana tayari imesha kuwa jioni, nikapiga kipenga cha kumaliza mpira huu. Kila mchezaji akanifwata na kunipa pongezi kwa maelezo mazuri ambayo nimewapa.
“Kwa nini usibaki na sisi ukawa mchezaji?”
Mchezaji mmoja alizungumza huku tukiwa tunatembea kutoka uwanjani hapa.
“Hapana rafiki yangu kila jambo linawakati wake, wakati wangu wa kucheza hapa Tanzania ukifika basi nitacheza”
“Sawa, ila hakika wewe ni kocha bora kwa kweli, yaani huyu mzungu hapa anakula pesa za serikali yaani anatufundisha kawaida sana”
 
“Ngoja niwaambie kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Siri ya kuwa timu bora sio kocha. Nyinyi wachezaji munatakiwa kuwa upande kati yenu na mujue kwamba nyinyi ni kama familia ya baba mmoja. Mukipambana hakikisheni kwamba munapambana kama familia, musiangalie eti yule ana uwezo au yule hana uwezo. Mukishikamana hakika kocha yeye kazi yake itakuwa ni kusimama tu nje ya uwanja, ila nyinyi mutajua ni nini munafanya”
“Kweli kaka unacho zungumza ni kitu cha kweli kabisa. Unajua tatizo letu sisi huwa tumetolewa kila mtu kwenye timu yake hivyo tukikuatana hapa utakuta huyu  anacheza hivi huyu anacheza hivi yaani ni tabu tu?”
“Hiyo sio sababu ya maana. Muna muda gani toka muweke kambi?”
“Leo siku ya tatu?”
“Katika masaa mawili nyuma mulikuwa muna chezaje?”
“Kawaida?”
 
“Sasa toeni ukawaida, hakikisheni kwamba munacheza kwa kujituma na upendo, acheni kuweka matabaka. Kapteni ni nani?”
“Ni mimi”
“Ohoo kumbe nipo na timu kapteni. Sasa wewe ndio wa kuyafanyia kazi kama vile nilivyo kuelekeza sawa kaka”
“Sawa”
Tukafika sehemu walipo makocha hawa wawili, tukakusanyika kwa pamoja.
“Jamani mumeona mulicho cheza leo. Sasa nataka iwe hivi hivi kwenye mashindano ya kombe la dunia ambayo tunaiendea”
Kocha alizungumza huku akiwa amejawa na furaha sana. Wakanipongeza sana huku wakiniomba kesho niweze kurejea ili nizidi kuungana na makocha hawa katika kuhakikisha tunakinoa kikosi hichi cha vijana.
“Nitazungumza na wenyeji wangu kama wataniruhusu kufika hapa kila siku”
“Kwani wenyeji wako ni kina nani?”
“Wapo kule juu”
Nilizungumza huku nikiwatazama Dany, Jojo na Camila sehemu walipo kaa.
 
“Sawa naomba uzungumze nao”
“Sawa jamani kwa herini”
Nikaondoka eneo hili huku wachezaji wakiwa wamejawa na furaha kunwa sana. Nikajimuika na wezangu huku nao wakionekana kunisifia hususani Dany. Tukaondoka katika eneo hili na kuelekea katika hoteli nyingine kwa ajili ya chakula cha usiku. Tukaagizia chakula tunacho kihitaji na baada ya muda muhudumu akatuletea chakula hicho. Moyo ukanistuka kwa mara nyingine mara baada ya kumuona mwanaume ambaye ameniuliza wazazi wangu katika taarifa ya habari, akiwa ni miongoni mwa wagombea walio tangaza nia ya kogombania kiti cha uraisi katika nchi hii ya Tanzania.

ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )