Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, December 20, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 46

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA
“Kwani wenyeji wako ni kina nani?”
“Wapo kule juu”
Nilizungumza huku nikiwatazama Dany, Jojo na Camila sehemu walipo kaa.
“Sawa naomba uzungumze nao”
“Sawa jamani kwa herini”
Nikaondoka eneo hili huku wachezaji wakiwa wamejawa na furaha kunwa sana. Nikajimuika na wezangu huku nao wakionekana kunisifia hususani Dany. Tukaondoka katika eneo hili na kuelekea katika hoteli nyingine kwa ajili ya chakula cha usiku. Tukaagizia chakula tunacho kihitaji na baada ya muda muhudumu akatuletea chakula hicho. Moyo ukanistuka kwa mara nyingine mara baada ya kumuona mwanaume ambaye ameniuliza wazazi wangu katika taarifa ya habari, akiwa ni miongoni mwa wagombea walio tangaza nia ya kogombania kiti cha uraisi katika nchi hii ya Tanzania.

ENDELEA
Nikajikuta nikisimama kwenye kiti nilicho kikalia na  kuanza kutembea hadi hadi karibu na tv hii jambo lililo wafanya Camila na watu wengine kushangaa sana. Nikamtazama mwanaume huyu huku kifua changu kikiwa kimejawa na hasira kali sana.
“Ethna”
Nilistuka mara baada ya Camila kunishika begani mwangu. Nikamtazama usoni mwake huku nikishusha pumzi nyingi sana.
 
“Vipi mume wangu”
“Huyu mwanaume”
“Amefanyaje?”
“Ndio aliye niulia wazazi wangu”
Camila macho yakamtoka huku akijiziba mdomo wake kutoka na an mshanagao mkubwa ulio mpata.
“Kama kweli yupo hapa Tanzania lazima nami nimuue”
“Ethan zungumza kwa sauti ya chini kidogo si unajua kuna watu wengi”
Camila alizungumza huku akinishika mkono na kurudi tulipo  kuwa tumekaa.
“Vipi?”
Dany aliniuliza huku akinitazama usoni mwangu.
“Yule mwanaume pale ndio aliye niulia wazazi wangu”
Dany na Jojo wakastuka kidogo huku wakinitazama usoni mwangu.
 
“Unasema kweli?”
“Sina haja ya kuwaongopea, ninacho kizungumza ni kitu cha ukweli na ninamkumbuka vizuri sana”
Ukimya ukatawala huku Dany na Jojo wakiitazama taarifa hii ya habari. Sikuweza hata kuendelea kupata chakula hichi, nikanyanyuka na kuelekea sehemu ya maegesho ya magari.
‘Fu* Fu*”
Nilizungumza huku nikipiga piga tairi  la gari tulilo jia.
“Ethan utajiumiza mume wangu usiwe hivyo bwana”
Camila alizungumza huku akinikumbatia kwa nyuma.
“Najua una hasira mume wangu, ila nina kuomba sana mpenzi wangu uwe mvumili, tutahakikisha tunamfungulia mastka na atashtakiwa kwa mujibu wa sheria za nchi hii”
“Nchi hii, unahisi mtu ana nguvu  ya kwenda kugombania urahisi, unahisi atashtakiwa ehee?”
 
“Ethna”
“Sio Ethan Camila. Hii sio Ujerumani, huku ni barani Afrika. Bara la watu weusi, hakuna haki, mwenye nguvu ana nguvu na asiye na nguvu hato kuwa na nguvu mke wangu”
Nilizungumza huku nikimwagikwa na mchozi usoni mwangu.
“Sasa mume wangu unahitaji tufanye nini?”
“Nahitaji alipe kwa kila baya alilo lifanya juu ya maisha yangu na wazazi wangu”
“Nitahakikisha  mume wangu nina kuwa nawe bega kwa bega kuhakikisha kwamba una fanikiwa katika kazi yako hii ya kulipiza kisasi sawa mume wangu?”
 
“Nashukuru mke wangu”
Jojo na Camila wakatufwata sehemu tulipo na tukaondoka eneo hili. Ndani ya gari sikuzungumza kitu chochote hadi tukafika nyumbani.
“Ethan nahitaji kuzungumza nawe”
Dany alizungumza huku akishuka kwenye gari, nikaanza kumfwata hadi nyuma ya nyumba hii, akafungua geti kubwa na kuingia ndani ya ukumbi mkubwa sana ambao  umejaa vitu vingi, ikiwemo silaha kubwa kubwa ambazo sikuwahi kuziona kwenye maisha yangu.
“Kaa hapo”
Dany aliniambia huku akinionyesha moja ya kiti cha kuzunguka kilichomo pembeni ya meza kubwa. Nikaka kwenye hichi kiti huku naye akizunguka kwenye meza hii na kukaa kwenye kiti kingine. Dany akaminya minya batani ya laptop iliyopo mezani mwake kisha akanigeuzia.
 
“Ni huyu”
Dany alinionyesha picha ya mzee ambaye ameniulia wazazi wangu. Nikafumba macho kwa sekunde kadhaa kisha nikafumbua na kumtazama tena.
“Ndio ni yeye”
“Anaitwa Poul Mkumbo, kabila lake ni Mnyiramba. Ana uwezo wa asilimia sabini na tano ya kuwa raisi wa nchi hii na ana nguvu katika jamii  kwa maana alijitengenezea nafasi ya kugombania uraisi zaidi ya miaka kumi na mbili kwa sasa”
“Nitampataje?”
“Unahitaji kumuua?”
“Nahitaji alipe kwa yale yote ambayo amenitendea kwenye maisha yangu”
“Kulipa kupo kwa aina nyingi, moja ni kumuua je hiyo ya pili una hitaji kumfanya nini?”
“Kwanza nahitaji  ngome yak e aliyo ijenga kwa miaka yote hiyo kuiangusha na ninahitaji kurudisha kila kitu alicho kichukua kwa wazazi wangu ana kirudisha”
 
“Alichukua nin na nini?”
Kumbukumbu zangu zikanirudisha kipindi nipo na wazazi wangu katika shamba letu moja kubwa la migomba. Katika harakati za wazazi wangu kupalilia migomba hii huku nami nikiwa nina cheza cheza pembeni ya moja ya mgomba huku nikichimba chimba chini, nikaona jiwe moja kubwa kiasi likiwa ni tofauti kabisa na mawe ambayo nilisha wahi kuyaona kwenye maisha yangu. Nikamkimbilia baba yangu na kumuonyesha jiwe hili, baba na maam wakaanza kutazama jiwe hili na kuniuliza ni wapi nilipo litoa.
Nikawaonyesha sehemu ambayo tumelitoa jiwe hili, baba akaanza kuchimba katika eneo hili na kuona jiwe jengine linalo fanania na jiwe hili.
 
“Hii ni dhahabu”
Maneno ya baba niliyakumbuka vizuri sana huku  akiwa na furaha kubwa sana huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Eneo hili lina dhahabu, hii ni mali mke wangu tumesha kuwa matajiri”
Baba aliendelea kuzungumza kwa furaha kubwa sana, kutokana hapa shambani si mbali sana na nyumbani, akaniagiza niweze kwenda  nyumbani kuleta moja ya kibegi ambacho hukitumia sana pale anapo kwenda mjini kuuza mikungu ya ndizi.
Kumbukumbu zangu zikazidi kusonga mbele hadi pale nilipo fika nyumbani, nikatafuta kibegi hicho, japo ilinichukua muda mwingi sana kuweza kuwapata, ila niliweza kufanikiwa kukiona. 
 
Nilipo rudi shambani, nikamkuta baba pamoja na mzee mmoja ambaye ni rafiki yake huku wakiwa wanachimba eneo hilo ambalo lina mawe haya ya dhabu. Nikakumbuka kibegi hicho kilijaa mawe hayo yanayo ng’aa sana na kururahisha unapo yatazama. Usiku wa siku hii ndipo tulipo vamiwa na kundi la vijana pamoja na mzee huyu bwana Mkumbo na hapo ndipo yalipo kuwa ni matatizo yangu na familia yangu.
“Utajiri wake mkubwa umetokea kwenye mgoni wa dhahabu huko Arusha ana umiliki”
Maneno ya Dany yakanistua sana na akaanza kunionyesha picha nyingine za mgodi mkubwa sana ambao unamilikiwa na bwana Mkumbo jambo ambalo limenifanya nizidi kuchanganyikiwa na kushikwa na hasira sana.
 
“Huu mgodi upo kwenye eneo ambalo ni mali ya wazazi wangu, ninahitaji kuuchukua”
“Hilo unalo lizungumza sio jambo rahisi sana”
“Nina akili na nina uwezo wa kufanya kila kitu na nitahakikisha kwamba ninafanikiwa”
“Etthan”
“Ninaomba unipatie taarifa zake na mali zake zote anazo zimiliki nitaanza kushuhulika na moja baada ya jingine”
“Unahisi njia hiyo unayo hitaji kuitumia ni sahihi kuweza kupata hizo mali?”
“Ndio”
“Sawa”
“Nitakapo hitaji msaada wako nitakujulisha na kesho nahitaji kwenda jijini Dar es Salaam, naamini huko ndipo nitakapo kwenda kufanya mipango yangu ili iweze kwenda”
“Dar es Salaam?”
“Ndio””
Dany akakaa kwa sekunde kadha kisha akatingisha kichwa ikiwa ni ishara ya kunikubalia kile nilicho muomba. Dany akafungua droo ya hii meza na kutoa moja ya simu na kunikabidhi.
 
“Utaitumia hii na ina kila aina ya habari za mgombea uraisi bwana Mkumbo. Utazipitia usiku kucha kisha kesho nitapanga safari ya wewe kuelekea jijini Dar es Salaam”
“Sawa”
Nikatoka ndani humu na kurudi chumbani kwangu na kumkuta Camila akiwa amekaa kitandani akinisubiria.
“Vipi kuna kitu gani kinacho endelea?”
“Nahitaji kupambana sasa”
“Kivipi mpenzi wangu?”
Nikaanza kumuelezea Camila juu ya mzee huyu. Nikamueleza na historia nzima ya maisha yangu na ya wazazi wangu, katika umri huu sasa ndipo nilipo weza kufahamu kwamba baba na mama yangu walikuwawa na mzee Poul Mkumbo kwa ajili mgodi wa madini.
“Kesho nitakwenda Dar es Salaam na wewe utabaki hapa sawa”
 
“Dar es Salaama unakwenda kufanyaje tena mume wangu”
“Nalianzisha hili swala, nitakuhitaji ubaki hapa sawa”
“Ethan hapana, siwezi kukuacha wewe uende peke yako. Kumbuka kwamba hili jambo  ni letu wote tafadhali mume wangu”
Camila alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake.
“Hapana sihitaji nikuweke matatizoni Camila. Kumbuka kwamba hii vita ni yangu, wewe kaa kama silaha yangu ya siri, siwezi kuingia vitani na silaha zangu zote za maangamizi kwa maana mtu ambaye ninakwenda kupambana naye sifahamu ana uwezo gani, sijui ana weza kutumia nguvu gani na kumbuka ninakwenda kumuangusha raisi ambaye anakwenda kuingia madarakani huku nyuma akiwa na dhambi na damu za watu ambao amewapokonya haki zao. Umenielewa?”
 
Nilizungumza kwa msisitizo na kumfanya Camila kukaa kimya huku akiendelea kumwagikwa na machozi usoni mwake.
“Nakupenda Camila nakuhitaji mke wangu. Ila acha nifanye hii kazi. Nina muda mfupi sana ila nakuomba mpenzi wangu unielewe sawa”
Camila akajibu kwa kutingisha kichwa akimaanisha  kwamba amenielewa kile nilicho mueleza.
“Nitakujulisha kila kila kitu ambacho kitakuwa kinaendelea katika katika kazi yangu sawa”
“Nimekuelewa mume wangu”
Tukakumbatiana na Camila kwa nguvu sana huku kila mmoja akiwa amejawa na huzuni pamoja na uchungu mwingi sana. Usiku huu, tukapeana penzi zito kana kwamba hatuto peana tena kwenye maisha yetu ya baadae.
                                                                                                                        ***
Tukaanza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam, tukiwa tumeongozana na Jojo, huku Dany akimsisitizia Jojo aweze kunilinda kwa kila namna. Safari ya kufika jijini Dar es Salaam ikatuchukua takribani masaa saba kwani nakumbuka ni sehemu moja tu ndio tulisimama ili kuweza kupata chakula cha mchana. Tukafika katika hoteli moja ya kifahari yenye hadhi ya nyota tano, Serena Hotel. Nikawasiliana na Camila na kumueleza kwamba tayari nimesha fika jijini Dar es Salaam na akanitakia kila la heri katika kuhakikisha kwamba nina ianzisha vita yangu ambayo haito mwaga damu ila itajaa uchugu na mateso makubwa sana kwa mzee Poul Mkumbo.
“Nakusikiliza Ethan, mpango wako wa kwanza ni upi?”
Camila aliniuliza huku akiwa ameweka nne kwenye sofa alilo kalia ndani ya chumba hichi tulicho fikizia.
 
“Katika meelezo nimeona mzee huyu ana mtoto wake wa kike na anafanya kazi katika shirika moja la simu si ndio?”
“Ndio”
“Nahitaji kuanza na huyo mwanaye wa kike”
“Unataka kumteka au kumfanya nini?”
“Ndio ninahitaji kumteka hisia zake, kupitia yeye nitaweza kuingia ndani kabisa katika familia ya mzee Mkumbo”
“Mmmm ni wazo zuri ila je umemuelewesha Camila juu ya jambo hili, isije tukapigana vita ambayo itaturudia sisi wenyewe?”
“Anaelewa kila kitu na nilisha muelez akia aina ya mbinu ambayo ninakwenda kuitumia kuifanya. Kikubwa ni kuhakikisha tunamuangusha mzee huyu”
“Sawa kama ni hivyo basi kila kitu kina wezekana”
“Nitahitaji kufahamu kwa sasa biti huyo yupo wapi ili tujue ni nini anacho kipanga”
“Sawa”
Jojo akafungua laptop tuliyo kuja nayo na kuanza kumtafuta binti huyo kupitia mtandao. 
 
“Sasa hivi namuona hapa anaelekea katika jengo la kibiashara Mlimani City”
“Ndio wapi?”
“Utafadhamu kama ukiamua twende”
“Sawa, linalo wezekana hivi sasa lisingoje baadae”
“Poa, je nibadilishe mavazi haya au?”
Nikamtazama Jojo jinsi alivyo vaa gauni lake refu lililo mpendeza.
“Una suti yoyote labda ulio kuja nayo?”
“Ndio”
“Vaa hiyo basi”
Camila akavaa suti nyeusi iliyo mfanya dhairi aonekane ni mlinzi wangu. Nikavaa koti langu la suti nililo livua muda nilipo kuwa tuna ingia ndani humu. 

Tukapanda kwenye gari letu tulilo kuja nalo aina ya BMW X6, nikakaa siti ya nyuma huku Jojo akiwa amekaa siti ya mbele kama dereva na nywele zake ndevu akiwa amezibana kwa nyuma huku baadhi ya nywele akiwa ameziachia eneo la usoni mwake na kufunika jicho lake la upande wa kulia. 

Nikaitazama hii saa ya dhahabu aliyo nikabidhi Dany asubuhi, kwa haraka haraka mtu akinitazama ni lazima atagundua kwamba mimi ni kijana mwenye pesa zangu tena sio chache ni nyingi sana. Nikaanza kupitia sura ya binti huyu wa Poul Mkumbo, ni binti mzuri kwa kukadiria ana umri kama miaka ishirini na tano au na kuendelea hivi, ila kutokana Mungu amenipa umbo kubwa kiasi sio rahisi kunidhania kwamba mimi ni kijana wa miaka kumi na nane. 
 
Tukafika katika jengo la kibiashara la Mlimani City. Jojo akashuka kwenye gari na kunifungulia mlango wa siti ya nyuma ya gar hili,i kisha tukaanza kutembea kuelekea ndani ya jengo hili, kabla ya kufika katika mlango mkubwa wa kuingia ndani ya jengo hili, tukamuona binti wa Poul Mkumbo akitoka huku akiwa ameongozana na walinzi wanne huku wawili wakiwa ni wa kiume huku wengine wawili ni wakike. Wakihakikisha wana mpa ulinzi mkubwa msichana huyu asiweze kusogelewa na mtu wa aina yoyote ile.

ITAENDELEA KESHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )