Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 25, 2018

Riwaya Kali: POWER - Sehemu ya 47

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA 
  
Tukafika katika jengo la kibiashara la Mlimani City. Jojo akashuka kwenye gari na kunifungulia mlango wa siti ya nyuma ya gar hili,i kisha tukaanza kutembea kuelekea ndani ya jengo hili, kabla ya kufika katika mlango mkubwa wa kuingia ndani ya jengo hili, tukamuona binti wa Poul Mkumbo akitoka huku akiwa ameongozana na walinzi wanne huku wawili wakiwa ni wa kiume huku wengine wawili ni wakike. Wakihakikisha wana mpa ulinzi mkubwa msichana huyu asiweze kusogelewa na mtu wa aina yoyote ile.

ENDELEA
Sikuhitaji kumkwepa dada huyu zaidi ya kutembea usawa ambao anatembea yeye, kitendo cha kumkaribia walinzi wake wakajaribu kunizuia, ila Jojo kwa haraka naye akasimama mbele yangu akionyesha msisitizo kwamba nisiguswe na walinzi hawa.
 
“Samahani”
Nilianza kuzugumza huku nikimtazama msichana huyu.
“Unahitaji nini?”
Binti huyu alizungumza kwa dharau kidogo huku macho yake yakiwa na kazi ya kunishusha na kunipandisha juu  na kunishusha chini.
“Ninaweza kuzungumza nawe kwa sekunde kadha?”
“Me……..!!?”
“Ndio”
“Umetokea wapi hadi uhitaji kuzungumza na mimi kwa maana kwanza sikujui na jinsi unavyo endelea kuwa mbele yangu ndivyo jinsi unavyo nipotezea muda. Tuondokeni?”
Dada huyu alizungumza kwa dharau  kubwa kisha akaanza kutembea kuelekea walipo acha magari yao. Japo nilipitia maisha ya kunyanyasika kutokana na ubaguzi wa rangi katika nchi ya Ujerumani, ila sijawahi kupitia hali ya kunyanyaswa kama hii tena na mswahili mwenzangu.
“Tuondoke zetu”
Nilimuambia Jojo huku nikiwa nimefedheheka sana moyoni mwangu.
 
“Hapana tuingie ndani, hivi tutaonekana kama tulikuwa tunamuhitaji yeye”
Nikakubaliana na wazo la Jojo, tukaingia ndani ya jengi hili na kuanza kupita pita kwenye maduka ya nguo. Tukanunua nguo kadhaa, kisha tukarudi hotelini huku mpango wangu wa kwanza ukiwa umegonga mwamba.
“Umekata tamaa ya kuwa na binti huyu?”
“Ana dharua kubwa sana ila dharau yake nina uhakika itakwenda kupotea siku moja”
“Kesho kuna mkutano wa kununua hisa katika kampuni anayo ifanyia kazi. Mwenye kampuni ana hitaji kuiuza kwa matajiri sasa kesho ni muda wa kumuonyesha kwamba wewe unaweza”
 
Jojo alizungumza huku akiwa ameshikilia simu yake mkononi, akanionyesha juu ya uuzaji wa kampuni hiyo ambayo itagarimu zaidi ya dola za kimarekani bilioni mbili na nusu kwa yule ambaye atahitaji kuinunua nzima, ila kama nitahitaji kuwa mwana hisa basi nitanunua kiasi cha hisa katika kampuni hiyo.
“Nahitaji kununua kampuni nzima?”
“Nzima?”
“Ndio nahitaji  kuimiliki na awe chini yangu”
“Hicho kiasi cha pesa unacho?”
“Ndio ninacho, nina makapuni mengi na nina kiasi cha kutosha tu”
“Sawa, kama unahitaji basi tuingize jina lako kwenye watu watakao hudhuria mkutano huo wa kununua hisa za kampuni hiyo”
“Wewe ingiza, kikao kitakuwa ni saa ngapi?”
“Saa mbili asubihi”
“Sawa fanya hivyo nahitaji kutumia simu yako kuwasiliana na dada yangu, je unaweza kunisaidia katika hilo”
“Hakuna shida”
 
Nikamtafuta Mery kupitia mtandao wa Imo, kwa bahati nzuri nikampata,, nikampigia simu yake na ikaanza kuita, akaipokea na tukaanza kuonana.
“Ethan ni wewe?”   
Dada Mery alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana usoni mwake.
“Yaa ndio mimi”   
“Ohoo Mungu wangu, za Tanzania”
“Salama vipi mama anaendeleaje?”
“Mama anaendelea vizuri na nina habari nzuri”
“Habari gani?”
“Timu yako jana imechukua kombe, je ulitazama?”
“Ohoo hapana, weee wameshinda goli ngapi?”
“Goli nne kwa moja, yaani wote walisema kombe hilo ni kwa ajili yako. Hapa nipo nao hotelini huku tunaendelea kushangilia”
“Hahaaa daa wasalimie sana ila usiwaambie kwamba mimi nipo wapi”
 
“Najua wala usijali kwa hilo jambo. Ehee vipi unaendeleaje?”
“Safi, kesho kuna kampuni nitahitaji kuinunua huku Tanzania”
“Waoo ni jambo zuri mdogo wangu, mimi nitaendelea kukuunga mkono kwa asilimia mia moja. Niambie nini unahitaji?”
“Nilikuwa ninakuap taarifa hata nitakapo toa kiasi cha pesa benki usije ukashangaa”
“Usijali mdogo wangu. Ikiwa baba aliamua kukuachia majukumu yote mikononi mwako. Nafurahi kuona jinsi uanvyo zidi kujitanua kiuchumi”
“Nashukuru dada yangu, basi tutawasiliana kesho pale nitakapo kuwa nimemaliza kufanya biashara hiyo.
“Sawa mdogo wangu kesho”
“Sawa”
Nikakata simu na kumrudishia Jojo simu yake.
“Nimesha ingiza jina lako na langu, mimi nitasimama kama mlinzi wako”
“Sawa dada nashukuru kwa kuniunga mkono”
“Usijali jukumu langu ni kuhakikishakwamba kile tunacho kwenda kukifanya kinafanikiwa kwa asilimia mia moja”
“Sawa”
 
Usiku wa siku hii Jojo akanitembeza kwenye baadhi ya maeneno ya kumbi za starehe kisha tukarudi hotelini na kulala. Asubihi na mapema tukaanza kujianda huku mimi nikivalia suti ya rangi ya kaki pamoja na shati la blue. Kiufupi nimependeza sana. Jojo akanitengeneza nywele zangu vizuri kisha tukaanza safari ya kuelekea katika kampuni ya ZAirtel. Majira ya saa mbili kasoro tukawasili katika kampuni hii yenye jengo moja refu lenye gorofa zipatano kumi na tano. Tukapokelewa na wahudumu wa kampuni hii ambayo wanapokea wageni rasmi walio kuja kununua hisa za kampuni hii.
 
Tukapelekwa moja kwa moja hadi ukumbi ambao nikakuta baadhi ya wafanya biashara huku wengine wakiwa ni watu kutoka katika mabara tofauti ikiwemo Ulaya na Asia. Nikakaribisha moja ya kiti huku Jojo akikaa kiti cha nyuma yangu kama mlinzi wangu. Wakaendelea kuingia wafanya biashara wengine, ilipo timu saa mbili kamili asubihi kikao kikaanza. Kila kwenye meza kuna maiki ambayo mtu anaweza kuzungumzia pale atakapo hitaji kutangaza dau lake. Nikamuona mtoto wa Poul Mkumbo akiwa amekaa pembeni ya mmiliki wa kampuni hii ambaye nilimsoma jana usiku asili yake ametokea nchini Afrika kusini.
 
“Karibuni sana, sasa tunaanza kupokea ofa zenu”
Muendeshaji wa ununuzi wa hisa hizi alizungumza huku dada mmoja akianza kutusambazia karatasi kila mmoja yenye maelezo niliyo anaza kuyasoma taratibu.
Nilipo maliza kuhakikisha kusoma maelezo haya yanayo panga kiwango cha hisa na bei yake nikaendelea kusikiliza ni kitu gani kinacho endelea. Wafanya biashara wezangu ambao wote ni watu wazima wakaanza kutangaza viwango vyao huku wote wakiwa wameanza na dola milioni kumi.
Muda wote macho yangu yapo kwa mtoto wa Poul Mkumbo, adui yangu namba moja, kila ninalo lifanya nina hitaji kuhakikisha kwamba ni moja ya mbinu  ya kuhakikisha  kwamba nina lipiza kisasi.
 
“Dola milioni mia tisa”
Muarabu mmoja alizungumza na kuwafanya watu wote tumtazame kwani hadi sasa hivi yeye dau lake ndio lipo juu.
“Dola bilioni moja”
Mama mmoja wa kizungu alizungumza na kufanya macho ya watu kuyahamishia kwake.
“Moja pointi moja moja bilio”
Muarabu huyu alizungumza tena na kuwafanya wafanya biashara wengine kumtazama. Majibizano ya wafanya biashara hawa yakaendelea hadi ikafika dola bilioni moja nukta nane.
 
“Dola bilioni moja nukta nane kwa mara ya kwanza”
Wafanya biashara wote wakaka kimya, nikageuka na kumtazama Jojo usoni mwake. Jojo akanikonyeza akimaanisha sasa ni muda wangu wa kuhakikisha kwamba ninatangaza dau kubwa la kuweza kuinunua kuampuni hii.
“Dola bilioni moja nukta nane kwa mara ya pili?”
“Dola bilioni  mbili na nusu”
Kwa mara ya kwanza nikawafanya watu wote kutazama upande wangu. Macho yakawatoka huku kila mmoja akionekana kushangaa sana kwani ni kiasi kikubwa na ndio kiasi kilicho kusudiwa na mmiliki wa kampuni hii katika kuiuza. Binti wa Poul Mkumbo akanitazama usoni mwangu kwa mshangao mkubwa sana kiasi cha kunifanya nitabasamu kwa dharau.
 
Hadi inafika mara ya tatu hapakuwa na mfanya biashara yoyote ambaye aliweza kufungua kinywa chake juu ya kiasi nilicho kitangaza. Baada ya kukosenaka mtu aliye weza kunipiku kibiashara, mkutano ukaisha huku nami nikielekezwa kuelekea kwenye ofisi kuu ili kufanya malipo na kuandikishana mkataba wa manunuzi.
 
“Ninaitwa bwana Josam Zuma, naamini wewe ndio bwana Ethan Klopp?”
“Ndio”
“Naamini jina lako si geni sana kwenye masikio yangu. Wewe ni mchezaji mpira?”
Mmiliki wa kampuni hii alizungumza huku tukiwa tumeshikana mikono.
“Ndio hujakosea mkuu”
“Ohoo nashukuru sana kufanya bishara na kijana mdogo sana ambaye anajiamini sana kama wewe”
“Nashukuru sana”
“Ohoo huyu ni mkurugenzi wa hii kampuni, anaitwa Biyanka Poul Mkumbo”
 
“Nashukuru kwa kuweza kufahamu”
Biyanka akajawa na kigugumizi kikubwa sana cha kuweza hata kuupokea mkono wangu kwani nina imani anakumbuka kila jambo ambalo amenifanyia jana mchana.
“Vipi Biyanka mbona kama una kigugumizi vipu muna fahamiana?”
“Hapana mkuu. Nashukuru sana kwa kukufahamu Ethan Klopp”
Biyanka alizungumza huku akinishika mkono wangu, nikauminya vizuri mkono wake ikiwa ni ishara moja ya kihuni. Tulipo maliza kutambulishana, nikaanza kufanya hatua za kuhamisha kiasi hichi cha pesa kutoka kwenye akauti yangu moja ya kibiasha na kuanza kuhamishia kwenye akauti ya mmiliki wa kampuni hii. Nilipo maliza zoezi hilo tukaandishikisha mikataba na nikawa mmiliki halali wa kampuni hii.
 
“Utabaki kuwa mkurugezi wa hii kampuni, kuanzia kesho nitahitaji kuweza kupata ripoti zote za hii kampuni. Kuanzia mauzo, hasara na faida zitokanazo na hii kampuni sawa Biyanka”
Nilitoa maelekezo haya  yote mara baada ya kumaliza kuandikishiana mikataba.
“Sawa mkuu”
“Utakabidhi Jojo namba yako ya simu na nitahitaji kuzungumza nawe mambo mengi sana ikiwezekana leo usiku kabla ya kesho”
“Sawa sawa mkuu”
Biyanka akanijibu kwa heshima zote, kiburi na dharua zote alizo kuwa akinifanyia jana usiku zote zimemuisha. Tukarudi hotelini na Jojo huku tukiwa na furaha kubwa sana kwani mpango wetu umekwenda kama vile tulivyo panga. 
 
“Hongera”
“Nashukuru Jojo, nakushukuru sana kwa kile ulicho nifanyia”
“Usijali, huyu binti amesha nipatia namba yake”
“Waoo sasa muda wa kwenda kuwaangusha maadui zangu hivi sasa umewadia. Umeona jinsi dharau zake zilivyo muisha”
“Yaa sasa kama unafanya kweli kweli mapenzi hakikisha kwamba unafanya kweli na ukimpata hakikisha ana kupenda kupitiliza na akisha kolea hakikisha kwamba una mpa pigo kubwa sana yeye na baba yake naamini kwamba huo ndio utakuwa anguko lao umenielewa”
“Nimekuelewa nanitafahanya hivyo kuhakikisha kwamba ninawaangusha chini yeye na familia yake.”

==>.ITAENDELEA KESHO
ad
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )