Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, December 17, 2018

Saudi Arabia yalaani Seneti ya Marekani kwa 'kuingilia masuala ya ndani ya nchi yake'

Saudi Arabia imepuuzilia mbali maazimio ya Bunge la Seneti la Marekani ya kutaka kusitishwa kwa msaada wa kijeshi wa Marekani katika vita vinavyoongozwa na Saudi Arabia nchini yemen.

Bunge la Seneti limemlaumu mwanamfalme wa Saudia kwa mauaji ya mwanahabari wa nchi hiyo Jamal Khashoggi nchini Uturuki.

Wizara ya mambo ya nje ya Saudi Arabia, imeelezea hatua hiyo kama kuingilia masuala ya ndani ya taifa na kutoa "madai yasiyo ya kweli''.

Maamuzi hiyo ya Marekani Alhamisi ya wiki iliyopita, kwa kiasi kikubwa ni ishara tu na hakuna uwezekano mkubwa wa kufanywa kuwa sheria inayoweza kutekelezwa karibuni.
 
Lakini wametuma ujumbe wakimuonya Rais Donald Trump kuhusiana na hasira ya wanasiasa wa Marekani dhidi ya sera za Saudi Arabia.
 
Kwa njia ya taarifa rasmi iliyochapishwa na chombo kikuu cha habari cha nchi hiyo- Saudi Press Agency, Wizara ya nchi za kigeni inasema kwamba: "Utawala wa kifalme unalaani msimamo huo wa Bunge la Seneti la Marekani. "

Inasema kuwa, msimamo kama huo "umejengwa juu ya madai ya uongo". Saudi Arabia inaongeza pia kuwa, inakataa katu "kuingiliwa kwa aina yoyote kwa maswala yake ya ndani".

"Awali utawala huo ulikanusha kabisa na kusema mauaji ya raia wake, mwaandishi habari Jamal Khashoggi, ni uhalifu mbaya mno ambao hauwezi kuhusishwa na sera za utawala huo wa kifalme au hata taasisi zake" na kurejelea tena kuwa, inakataa "jaribio la kuchukua suala hilo nje ya namna ilivyo sheria na haki ya utawala wa nchi hiyo."

Marekani bado haijajibu taarifa hiyo ya Saudia.

-BBC
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )