Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Friday, December 7, 2018

Serikali Yaiagiza Bodi Ya Wataalam Wa Ununuzi Na Ugavi Kudhibiti Maadili Ya Wataalam Wa Ununuzi Na Ugavi

Na Josephine Majura, WFM, Dodoma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Bi. Susana Mkapa, ameiagiza Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi nchini (PSPTB), kuhakikisha kuwa inadhibiti maadili ya wafanyakazi wa sekta ya ununuzi na ugavi ili fedha za serikali zinazotumika kwenye ununuzi ziwe na tija kwa wananchi.

Bi. Mkapa ametoa maagizo hayo Jijini Dodoma, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Naibu Katibu Mkuu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mipango wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Richard Mkumbo, wakati akifunga kongamano la tisa la wataalam wa ununuzi na ugavi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara.

Bw. Mkumbo amebainisha kuwa licha ya vitengo vya matumizi mabaya ya fedha za umma kupitia sekta ya ununuzi na ugavi, ikiwemo rushwa kuendelea kupungua, Bodi inatakiwa kuhakikisha kuwa vitendo vya rushwa vinadhibitiwa ipasavyo.

Amesema asilimia 75 ya fedha za umma zinatumika kupitia mchakato wa manunuzi ambao taarifa ya mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali (CAG) na Mamlaka ya Ununuzi nchini PPRA, umebaini kuwepo kwa viashiria vya rushwa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi, Sister Dkt. Hellen Bandiho, amesema kuwa Bodi yake itahakikisha inasimamia kikamilifu maadili ya watumishi wa sekta ya ununuzi ili iweze kushiriki katika kukuza uchumi wa viwanda.

Kongamano hilo limewashirikisha wataalam wa ununuzi na ugavi wapatao 650 kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara

Mwisho
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )