Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Monday, December 10, 2018

Serikali Yazitaka Taasisi za Dini Ziendelee Kuhubiri Amani

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tamisemi), Seleman  Jafo amesema taasisi za dini na viongozi wake wana kila sababu ya kuhimiza upendo na mshikamano wa kuliombea Taifa ili Watanzania waendelee kuishi kwa amani  na utulivu.

Jafo ambaye ni Mbunge wa Kisarawe ametoa kauli hiyo, jana Jumapili Desemba 9,2018 wakati ufunguzi wa mkutano wa 34 wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Mashariki ya Pwani (DMP).

Ufunguzi wa mkutano huo wa siku tatu ulitanguliwa na ibada iliyoendeshwa na Askofu kwa kanisa hilo, Dk Alex Malasusa iliyofanyika katika kanisa la Kilutheri la Mbezi Beach.

Jafo alisema baadhi ya mataifa hayana amani wala utulivu lakini Tanzania kuna  hali hiyo na vyema viongozi wa dini na taasisi hizo zikaendeleza maombi kwa Taifa ili Watanzania kuishi kwa usalama.

"Taifa bado linahitaji maombi, nawashukuru viongozi wa dini kwa kuliombea Serikali ipo bega kwa bega na ninyi kwa sababu mnaisadia kuwajenga  wananchi kwenye msingi wa kiroho," alisema Jafo.

Dk Malasusa alisema mkutano huo una malengo mbalimbali ikiwamo kujadili masuala kadhaa yanayohusu dayosisi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

"Ndani ya miaka miwili tumefanikiwa masuala kadhaa ndani ya dayosisi hii. Miongoni mwa mambo hayo ni kuunda mfuko wa elimu wa dayosisi hii kwa ajili kutoa huduma," alisema Dk Malasusa.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )