Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Tuesday, December 18, 2018

Sumaye ataja maadui wanaoiua CHADEMA

adv1
Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amewataja maadaui ambao watapelekea Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kukosa ushindi katika chaguzi mbili zijazo.
 
Akifungua mkutano wa ndani wa Baraza la uongozi la CHADEMA Kanda ya Pwani, Sumaye amesema kuwa, maadui wa chama hicho ni baadhi ya wanachama wanaoweka maslahi binafsi mbele kuliko ya Chama na ya wananchi waofifisha jitihada za kukijenga.

"Umefika wakati kwa wanachama wetu kufikiria masilahi mapana ya wananchi na chama la sivyo itakuwa vigumu kushika dola, na kama wanachama watajikita kutetea masilahi binafsi kama ilivyotokea kwa baadhi, ni dhahiri lengo la kuongoza nchi halitafikiwa", amesema Sumaye.

Sunaye ametoa kauli hiyo katika kipindi ambacho baadhi ya wabunge, madiwani, wenyeviti wa halmashauri na wanachama wakijiuzulu nafasi zao na kutimkia CCM ambako baadhi yao walipitishwa na kurudi kwenye nyadhifa hizo.

Uchaguzi wa serikali za mitaa nchini unatarajiwa kufanyika mwakani kabla ya uchaguzi mkuu 2020.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )