Tuesday, December 4, 2018

Uteuzi Mpya Uliofanywa Leo na Rais Magufuli

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Jaji Mstaafu Steven Bwana kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha miaka 3.

Pamoja na kumteua Mwenyekiti wa Tume, Rais Magufuli amewateua Makamishna 5 wa Tume ya Utumishi wa Umma.

Walioteuliwa ni George D. Yambesi, Balozi Mstaafu John Michael Haule, Immaculate P. Ngwale, Yahaya F. Mbila, Balozi Mstaafu Daniel Ole Njoolay.

Uteuzi huu wa Mwenyekiti na Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma umeanza tarehe 22 Novemba, 2018.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )