Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 7, 2018

Waziri Mkuu Atoboa Siri ya Kuvunjwa kwa bodi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Desemba 7, 2018, ametoboa siri ya kuvunjwa kwa bodi ya Shirika la Hifadhi ya Jamii NSSF.

Amtetoboa siri hiyo alipotembelea kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mkulazi namba mbili kilichopo Gereza la Mbigiri wilayani Kilosa mkoani Morogoro leo.

Majaliwa amesema alikuwa akipata taarifa kutoka kwa uongozi uliopita kuwa mradi unaendelea vyema, lakini baada ya kuwatuma wataalamu mbalimbali kutembelea mradi huo ulionekana kusuasua, Serikali iliamua kuchukua hatua ya kuivunja bodi hiyo pamoja na idara nyingine zilizokuwa zikihusika na mradi huo.

Ameipongeza bodi mpya ya NSSF na Mkulazi kwa namna zinavyoshirikiana na Jeshi la Magereza katika kutatua changamoto zilizopo  pamoja na  kuwafikia wakulima wa nje wa miwa katika kiwanda hicho.

Waziri Mkuu ameziagiza bodi mbili zilizoteuliwa hivi karibuni za NSSF na ile ya Mkulazi, kufanya jitihada za kutosha kuhakikisha mradi wa kiwanda cha sukari cha Mkulazi namba mbili unakamilika kama ilivyopangwa.

Amezitaka kuimarisha mfumo wa  maji na kuangalia namna nzuri ya kuyadhibiti yanayopotea kipindi cha mvua ili yaweze kusaidia wakati wa kiangazi kwa nia ya kuzalisha miwa kwa wingi na isikauke kama ilivyo sasa.

Ametaka pia kuimarishwa kwa mashine za umwagiliaji, kutafuta nyingine mpya ili kuondokana na changamoto ya sasa ukosefu wa mashine mpya za kusaga miwa.

Pia amewaagiza wakuu wa wilaya za Kilosa na Mvomero kuwahimiza wananchi kulima miwa jirani na kiwanda hicho cha Mkulazi kinachoendeshwa na Serikali kupitia NSSF kwa kushirikiana na Jeshi la Magereza.

Amesema kwa kufanya hivyo, viwanda vilivyopo vitazalisha sukari ya kutosha na kuondokana na utegemezi na gharama kubwa za uagizaji wa sukari toka nje ya nchi.

Mbali na kutoa maagizo hayo, Majaliwa amewataka watumishi wa serikali kuchangamkia fursa ya kulima mashamba yaliyo jirani na kiwanda hicho ili kujipatia kipato.

Mwenyekiti wa bodi mpya mbia ya Mkulazi Holding Company, Dk Hildelitha Msita amezungumzia namna walivyotekeleza maagizo ya waziri mkuu baada ya awali kusua sua kwa kiwanda hicho na changamoto zilizopo hasa umeme na ukame.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenister Mhagama amesema anaamini mradi huo utakuwa wa mfano na wabia wanatakiwa kukubaliana huku wakiongozwa na uzalendo na uaminifu.

Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba kwa upande wake amemuomba waziri mkuu kusaidia kiwanda cha mkulazi namba moja nacho kianze uzalishaji .
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )