Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, December 21, 2018

Waziri Ummy Apeleka Gari Ya Wagonjwa Ruangwa.

adv1
Na Bakari Chijumba, Lindi
Serikali imeahidi kukipatia kituo cha afya cha Luchelengwa wilayani Ruangwa, gari la kubebea wagonjwa pamoja na mashine ya kisasa ya Xray kabla ya Aprili 2019, lengo likiwa ni kuboresha  huduma za afya kwa wananchi.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mheshimiwa Ummy Mwalimu, ametoa ahadi hiyo alipofika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa na  kupokea taarifa ya Afya ya Wilaya hiyo jana 20 Desemba 2018.

Waziri Ummy amefikia uamuzi huo baada ya Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa, kutaja changamoto zinazosabababisha kusuasua kwa upatikanaji wa huduma ya afya ya uhakika.

"Mwezi wa tatu mwakani nitakabidhi gari la kubebea wagonjwa kituo cha Afya luchelengwa na mwezi  wa pili nitakabidhi machine ya mionzi ya kisasa " amesema Waziri Ummy

Aidha Waziri amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, kuanza ujenzi mara moja wa chumba cha kisasa cha kuhifadhia machine ya mionzi katika hospital ya Wilaya, ili iwe rahisi kukabidhi mashine hizo kwa wakati.

Katika hatua nyingine waziri Ummy, amepongeza kitendo cha Hospitali ya Wilaya kuwa na dawa zote muhimu zinazotakiwa kupatikana hospital na hiyo ni baada ya kukagua na kuona stoo ya dawa zilizopo hospitalini hapo.

"Nimefurahishwa na uwingi wa dawa uliopo hospitalini, niwatake muendele hivi hivi kuwa na dawa za muhimu za kutosha ili tupunguze suala la wananchi wetu kununua dawa kwenye maduka ya nje ya watu binafsi" amesema Mheshimiwa Ummy.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa  ametoa shukurani kwa serikali  kwa kuahidiwa kupatiwa Gari la wagonjwa na mashine ya mionzi (XRAY).

Mgandilwa amewataka madaktari kuhakikisha kila siku asubuhi wanabadili chati ya dawa ili iwe rahisi katika utendaji wao na kujua dawa ipi ipo kwa siku hiyo na ipi haipo.

" Mara nyingi nimekuwa nikipita naona hamfanyi mabadiliko ya chati ya dawa hii inasababisha wagonjwa kuandikiwa dawa zisizokuwepo, kuweni na taratibu kila siku asubuhi kubadilisha itawasaidia sana katika utendaji wenu" amesema Mgandilwa

MWISHO
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )