Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Sunday, December 2, 2018

Zari awajia juu mashabiki wanaomtaka ahame kwenye nyumba ya Diamond ya Afrika Kusini

Mjasiriamali  Zari Hassan ambaye pia ni mzazi mwenzie na Diamond Platnumz amejikiuta akishindwa kuvumilia maoni ya mashabiki wake mtandaoni wanaomtaka aondoke kwenye nyumba ya kifahari ya mzazi mwenzie,Diamond Platnumz
 
Zari kupitia ukurasa wake wa Intagram amesema kuwa hawezi kutoka kwenye nyumba hiyo, kwani yeye na watoto wake (Tiffah na Nillan) walinunuliwa nyumba hiyo ya kuishi.

Mrembo huyo kutoka Uganda ambaye makazi yake kwa sasa yapo Afrika Kusini, amesema kuwa kung’ang’ania kwake sio kwamba hana nyumba nyingine hapana anamiliki nyumba nne Afrika Kusini, bali anaishi kwenye nyumba hiyo kwani ni ya kwake na watoto wake.

Diamond na Zari wameachana mapema mwaka huu baada ya kuishi kwa takribani miaka mitatu kwenye mahusiano, wamefanikiwa kupata watoto wawili Tiffah ambaye ndio mtoto wa kwanza wa Diamond na Nillan.
Advertisement
==


Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Loading...
==

....

===
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )