Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 11, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 182 na 183 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
"Carin hakikisheni mkuu anakuwa salama”
Ester alizungumza huku akiwa ameishika vizuri earphone aliyo ivaa sikioni mwake.
“Muweke loudspeaker”
Ester akafanya hivyo, akaminya moja ya simu za mezani na tukaanza kusikia milio ya risasi jinsi inavyo endelea kurindima katika eneo hilo. Wanajeshi wa Marekani wakazidi kuongezeka jambo ambalo ni hatari sana kwa vijana Livna.
“Mkuu tumezidiwa tunaomba msaada, narudia tena tumezidiwa tunaomba msaada”
Tuliisikia sauti ya Carin alizungumza jambo lililo tufanya sote kutazamana, kwani hata tukituma wasichana wengine ili kuweza kufika eneo hilo watachukua muda mrefu njiani na wanaweza kukuta kila kitu kimekwisha, jambo ambalo ni hatari sana kwetu.

ENDELEA
“Tunatuma kikosi sasa hivi”
Ester alizungumza kisha akazima simu hii na kuvua earphone aliyo ivaa sikioni mwake.
“Tunafanya nini kwa maana hata tukitoa timu ikaenda kwa njia ya angani kwa kutumia helicopter hatutoweza kufika”
“Kuna mbinu yoyote ambayo tunaweza kumtishia Mmarekani?”
Kila mtu akaka kimya huku akifikiria ni kitu gani anaweza kunijibu.
 
“Mbinu ya mwisho iliyo baki  ni ile ya kuzipambanisha Marekani na Korea Kusini”
“Haito chelewa kutimia?”
“Hapo ni kumuomba Mungu, pia tunaweza kufanya mashambulizi makubwa sana kwa Korea Kaskazini na tutamfanya apatwe na hasira ya kuhakikisha kwamba anajibu mashambulizi”
“Kazi ianze mara moja”
Ester na wezake wakaka kwenye viti kila mmoja akiwa na laptop yake, nikaendelea kutazama mapambano ya wasichana hawa na jeshi la Marekani.
“Mungu wangu risasi zimewaishia”
Nilizungumza huku nikiwatazama wasichana hawa wakiwa wamejificha sehemu walipo huku kila mmoja akiwa hana silaha kabisa.
 
“Nina wazo pia?”
Msicha mwengine ambaye bado sijamfahamu jina lake alizungumza na kutufanya sote kumgeukia.
“Ndio”
“Kuna ndege ya kivita ambayo tunaweza kuitumia kwa kuwashambulia hao wanajeshi”
“Ipo wapi hiyo ndege?”
“Ipo chini kabisa ya hii meli, ndege hii mkuu alinionyesha na hiyo ndio silaha ya haraka kwa sisi kujilinda pale tunapo shindwa”
“Nani anayeweza kuiendesha?”
“Uzuri hiyo ndege haitumii rubani, unaweza kuiendesha kupitia hata hii laptop”
Sote tukabaki tukimtazama msichana huyu huku tukiwa na mshangao.
 
“Itachukua muda gani kufika eneo la tukio?”
“Dakika kumi hadi saba hivi”
“Anza kuiendesha sasa”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama msicha huyu ambaye kwa muonekano wake ni mpole sana, ila kichwa chake kina akili na kinaweza kufanya mambo mengi sana makubwa.
“Ukiendesha hiyo ndege naomba video uitume kwenye video hii”
Nilizungumza huku nikimuonyesha tv ya kwanza, akatingisha kichwa huku akiendelea kuminya minya batani zake kwa kasi kubwa sana. Tukaanza kuiona ndege hii ambayo sio kubwa sana ikianza kutoka chini kanisa ya meli hii kwa kasi ya ajabu ikaanza kuelekea angani, binti huyu mwenye utalamu wa hii kazi akazidi kuiendesha ndege hii ambayo kusema kweli hata mimi leo ndio mara yangu ya kwanza kuiona. 

Kwa jinsi binti huyu anavyo endesha ndege hiyo kwa kutumia laptop yake, hadi jasho usoni mwake likaanza kumwagika, ndani ya dakika sita ndege ikafika eneo la kisiwa, shambulizi la kustukiza kwa wanajeshi wa marekani likaanza, cha kumshukuru Mungu wasichana hao bado hawakuwa wamekamatwa, ikamuwia urahisi msichana huyu kushambulia kisawa sawa wanajeshi hawa, na kila aliye bahatika kupigwa risasi japo ya mguu, basi mguu wake uliweza kukatika kabisa, na inaonyesha ndege hii ina risasi kubwa na zenye uwezo wa kutoboa hata ukuta.
 
“Wasichana hawa walivyo ona wamepata msaada nao hawakuwa wanyonge, wakanza kuchukua bundiki za wanajeshi walio kufa na kuendelea kujibu mashambulizi kwa wanajeshi wanao jihahidi kushambili hiyo. Ester akavaa tena earphone sikioni mwake na kiiwasha simu iliyopo mezani.
“Songeni mbele hamuwezi kuudhurika sawa”
Ester alizungumza kwa msisitizo.
“Sawa mkuu”
Wasichana hawa wakaanza kukimbilia ndani ya hospitali alipo Sara na wagonjwa. 
 
“Wanasarenda masikini ya Mungu weee”
Logate alizungumza huku akiwaona wanajeshi wa Marekani wanao kimbialia baharini ambapo ndipo walipo ziacha boti.
“Kumbe walikuja na meli?”
Nilizungumza huku nikiitazama meli hiyo kubwa ya Wamarekani
“Ndio hiyo”
“Tuishambulie?”
“Ishambuli tu, usiiche”
Msicha huyu akapelekea mashambulizi kwenye meli hiyo, na safari hii mashambulizi ni ya mabomu makubwa makubwa na kuifanya meli hiyo kuanza kuteketea kwa moto na mwishowe ikaanza kuzama ndani ya maji ya bahari.
 
“Kazi imekwisha”
“Ngoja kwanza usiirudishe, hembu wasiliana na hao mabinti waulize wamewaona kina Livna”
“Carin mume wapata wagonjwa?”
“Ndio tumewapata na wapo salama kabisa na japa nao walikuwa wakisaidiana na dada Sara kuhakikisha wana wazuia wamarekani hawa kuingia ndani ya hospitali.”
Maeno ya Carini yakazidi kunipa faraja moyoni mwangu.
“Mtoto wa K2 je?”
“Pia yupo”
 
“Basi  hakikisheni muna rudi naye hapa”
“Sawa mkuu”
Tukajikuta tukishangulia kwa furaha, Logate pasipo kujali akajikuta akinikumbatia kwa nguvu, kitendo hichi kikanifanya nisisimke sana na kumuachia Logate haraka sana kwani sikuwahi kukumbatiana na mwanamke na damu yangu kunisisimka haraka kama hivi.
“Kazi nzuri, unaotwa nani?”
“Ritha”
“Oohoo hongera sana, kusema kweli ni kazi nzuri iliyo tukuka”
“Shukrani, ila nitawaomba munilinde kwa mkuu kwani ndege hii hakuihitaji watu waifahamu na wala hakihitaji itumike pasipo  idhini yake”
“Usijali nitazungumza na Livna akija sawa Ritha”
“Shukrani kaka Dany”
 
Carin na wezake wakafanikiwa kuwachukua Livna na wezake na kuanza safari ya kurudi huku tulipo huku wakiwa wameongozana na Sara pamoja mtoto wa K2. Sura za furaha zikazidi kutawala ndani ya chumba hichi. Livna na wezake walipo fika karibu na hii meli sote tukatoka ndani ya chumba hichi na kuelekea sehemu ambayo boti hiyo inasimama. Livna akashuka kwenye boti na kwaharaka akanfwata na kunikumbatia kwa nguvu huku machozi yakimwagika.
“Nimerudi”
Livna alizungumza huku akizidi kunikumbatia kwa nguvu.
“Shiiii usilie”
Taratibu nikamuachia Livna kifuani mwangu na kumtazama usoni mwake. Tukaondoka eneo hili huku nikimtazama mtoto huyu wa K2 .
 
“Kama sijakufa leo, basi siwezi kufa siku  nyingine kwa kushambuliwa kama leo”
Livna alizungumza huku tukiingia kwenye ofisi ya ambayo tulikuwepo.
“Sara asante, sikutegemea kama unaweza kuwa na akili kaama hiyo uliyo itumi. Logate, Ester asanteni, ilifikia hatu ya sote tulikata tamaaa kwani tulisha shindwa kabisa na mashambulizi”
Livna alizungumza kwa sauti ya upole na unyonge sana.
“Dany nina imani na wewe mchango wako umeonekena ninakushukuru sana kwa kweli”
“Usijali tupo pamoja”
 
“Tumekueletea uliye hitaji kumuona, sasa kazi ni kwako”
Nikamtazama mtoto wa K2 ambaye anaonekana amelia sana hadi amechoka, taratibu nikamsogelea na kuchuchumaa mbele yake.
“Unanikumbuka?”
“Mmmmmm”
Alijibu kwa kutingisha kichwa akimaanisha kwamba ananikumbuka.
“Ninaitwa nani?”
“Dokta Lameck”
Jina la dokta Lameck likawafanya watu wote kunishangaa.
“Sawa utazungumza na mama yako muda si mrefu”
“Sawa, kwa nini umenichukua?”
“Utajua baada ya muda ni kwa nini nimekuchukua. Kampeni chakula”
 
“Sawa”
Pacha mmoja akamchukua mtoto wa K2 na kutoka naye humu chumbani.
“Sara nina imani kwamba umemsikia Dany, sasa huyu ni Dany”
“Kweli anafaa kuwa gaidi, nashukuru kukufahamu Dany”
“Nashukuru nawe pia kwa hili ulilo nifanya, ila ni kwa nini unasema kwamba ninafaa kuwa gaidi?”
“Muonekano wako japo ni mzuri ila kwa watu kama sisi tunaweza kuona ni kitu gani ambacho kipo ndani yako”
“Samahani jamani kuna simu inaingia”
Ester alizungumza huku akitutazama.
 
“Kutoka wapi?”
“Hii kwa sasa inatokea Iraque na anaye piga ni Osama Bin Laden”
“Ngojeni kwanza mumesema Osama!!?”
“Ndio rafiki yangu, Osama yupo hai na nimarafiki wazuri na Dany”
Nikasimama mbele ya Tv ambayo ninawasilianana Osama, nikavaa eaphone aliyo nikabidhi Ester.
“Asallam Alghaikum?”
“Salama, nina imani umepata sehemu sahii ya kujificha?”
“Ninashukuru sana Dany kwa maana kuna mmoja wa watu wangu ndio alikuwa anavujisha signal ndio maana wamarekani waliweza kufanikiwa kuyanasa mawasiliano yetu”
 
“Sawa ninaimani hilo umelishuhulikia?”
“Ndio nimelishuhulikia kabisa kabisa. Ila sijasikia mashambulizi yoyote kutoka sehemu ambayo ilikuwa maficho yangu?”
“Niliweza kuziteketeza ndege zote hewani, kwa hiyo hapakuwa na ndege moja iliyo weza kufika nchini Pakistani”
“Ohoo Allah akuzidishie”
 
“Shukrani”
“Sasa tunaweza kuonana, kwa maana kuna mengi sana ninahitaji kuzungumza nawe”
“Hilo halina kipingamiza, ila kuna jambo moja ninahitaji unisaide”
“Zungumza”
“Wamarekani wamamkamata mke wangu ambaye ni mjamzito kwa sasa, wanamtumia yeye kuhitaji nijisalimishe mikononi mwao, ninakuomba sana uweze kuniasidia katika kumuokoa kutoka mikoni mwao, na siku tukionana basi itakuwa ni siku nzuri ya urafiki wetu”
 
“Usijali katika hilo, nitahakikisha kwamba wapelelezi wangu wanafanya kazi usiku na mchana kufahamu ni wapi alipo mke wako kisha tutamchukua tu. Nipatie picha yake ili iwe raisi kuweza kumpata”
“Utatumia muda wowote kuanzia hivi sasa”
“Tayari”
Ester aliziungumza
“Nimeipata, ninakuahidi rafiki yangu nilazima mke wako tumpate”
 
“Ninashukuru”
“Basi nikimpata nitakuambia ni wapi tuonane ili tuweze kukabidhiana”
“Sawa sawa”
Mazungumzo kati yangu na Osma yakaishia hapa na kunifanya niwageukie Livna na Sara walio simama pembeni yangu.
“Sara nina imani kwamba umeamini”
“Jamani huyu baba tuliambiwa ni marehemu kabisa”
“Yupo hai na taafira zilikuwa ni za uongo”
“Mmmm makubwa basi”
“Martin pole sana mdogo wangu”
“Usijali mkuu  ni jukumu langu”
“Usiku huu ninahitaji tufanye sherehe na wasichana wangu wote, kwa maana leo nimepata nafasi nyingine ya kuishi. Ninakuomba Ester ulisimamie hilo, pia tutamkaribisha Sara nyumbani sasa”
“Sawa mkuu”
 
“Jamani ninaomba nikapumzike kidogo”
Martin alizungumza kwa sauti ya upole kidogo nikamtazama kwa sekunde kadhaa kisha nikatingisha kichwa kumkubalia kwamba aende akapumzike.
“Unaonaje ukawasiliana na K2 sasa hivi ili kumpa presha?”
“Hapana ngoja siku ya leo ipite, tunahitaji kupumzika, kwani tumefanya kazi kubwa sana”
“Sawa ni wewe tu Dany”
Maandalizi ya sherehe yakaanza kufanyika, Livna akaanza kunitembeza katika meneo ambayo sikuwahi kuingia ndani ya hii meli kubwa sana.
“Dany”
“Naam”
“Ninakupenda”
Livna alizungumza huku tukiendelea kutembea taartibu tukielekea katika eneo jengine ambalo ameniambia linatatumika kwa kuzalishia mazoa mbali mbali yanayo tumika ndani ya hii meli.
“Ninakupenda pia”
“Kweli Dany, yaani leo nilipo zimia pale, picha ambayo inijia akilini mwangu ni yako, nilihisi ninakwenda kufa kusema kweli nilimuomba Mungu kwa mara yangu ya kwanza kunipa nafasi ya kiishi ili nije kuishi kama mama sasa”
 
“Unahitaji kuzaa na wewe?”
“Ndio, Dany umri wangu unakwenda sasa, na mimi siku nahitaji kuwa mama ninahitaji kuwa mama. Wewe ndio mwanaume sahihi wa kunipatia ujauzito sihitaji kufa nikiwa sina mtoto japo kwa mara ya kwanza niliapa kutokuwa na mtoto ila sasa ninahitaji”
Tukaingia katika eneo hili ambalo ni kubwa kama hekari kumi, limejaa udogo mwishi pamoja na mazoa ya kila aina, nikajikuta nikiwa ninashangaa kwani utaalamu huu sijajua wameutolea wapi.
“Mumefanyaje fanyaje hadi kuwa hivi?”
“Mimi mwenyewe kusema kweli nimekuta hili shamba kutoka kwa waanzilishi, na mimi nikaliendeleza kulilima na vijana wanaendelea kupata matunda ya kila aina”
 
“Kusema kweli sijapata ona kitu kama hichi”
Tukaanza kutembea ndani ya hili eneo ambalo kwa pembeni limezingushiwa vioo.
“Haya mazao yanakua kwa mionzi ya jua inayo ingia, seme sasa hivi ni jioni kama tungefika mchana basi tungeweza kuona jinsi mionzi ya juu jinsi inavyo ingia ndani ya hili eneo”
“Inashangaza kusema kweli daaaa”
Niliendelea kuzungumza huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa kwani hili eneo unaweza kusmea ni shamba ambalo lipo nchi kavu kumbe ni ndani ya meli hii kubwa ambayo imeundwa kwa utaalamu mkubwa ambao unaweza kuwafanya watu kuishi miaka kwa miaka. Simu ya Livna ikaita, akaitoa mfukoni mwake na kuipokea. Akasikiliza kwa sekunde kadhaa akionekana anakabidhiwa maeleo fulani.
“Tunakuja sasa hivi”
Livna akakata simu na kuiridisha mfukoni mwake.
“Kuna nini?”
“Martin”
Livna alijibu huku akianza kukimbia, tukazidi kukimbia kuelekea ndani. Tukafika katika chumba cha Martin na kukuta madaktari wawili wa kike wakiwa wamemvua shati lake huku pembeni ya tumbo lake upande wa kulia kukiwa na damu nyingi.
 
“Amefanyaje?”
“Amepigwa risasi iliyo zama ndani na imeharibu sehemu kubwa sana ya vitu vya ndani, jambo linalo weza kupelekea kufa muda wowote kuanzia hivi sasa”
Maneno ya msichan huyu ambaye ni daktari yakanifanya nibaki na mshangaoo huku machozi yakinilenge lenga, hapa ndio nikakumbuka jinsi nilivyo mtazama Martin usoni mwake kipindi alipo aga anakwenda kupumzika, alikuwa ni mnyonge sana kupita siku zote nilizo wahi kumfahamu na kufanya naye kazi.    
 
AISIIIII……….U KILL ME 183 

“Apegiwa risasi saa ngapi jamani?”
Livna alizungumza huku machozi yakimlenga lenga  usoni mwake.
“Hili jeraha alikuja nalo na mimi ndio mtu wa kwanza kumuona”
Daktari alizungumza huku wakiendelea kujaribu kuitoa risasi iliyopo tumboni mwa Martin.
“Martin, Martin, Martin?”
Niliita huku niwa nimechumaa pembeni yake. Martina hakuitika wala kuyafumbua macho yake zaidi ya kukaa chini.
“Tunahitaji damu ya mtu mwenye group A plus”
Nesi alizungumza huku akiweka kifaa maalumu cha kupumulia pauni mwa Martin.
 
“Nitoeni mimi”
“Inabidi kukupima kwanza, tufahamu kwamba ni group O plus kwa maana Martin kundi lake la damu ndio hilo”
“Nipimeni tu”
Nilizungumza huku nikikunja mikono ya shati hili la jeshi nililo vaa, nikatoka chumbani humu na daktari mmoja na kuelekea hadi maabara. Akatoa damu yangu kiasi na kuipima.
“Damu yako ipo safi, na ni group A plus, inabidi utoe japo chupa mbili za damu”
“Sawa dokta fanya haraka haraka basi”
“Sawa”
 
Dokta akaufunga mkono wangu na mpira unao vutika kisha akanichoma sindano iliyo anza kupeleka damu kwenye dripu.
“Itachukua muda kidogo hadi kujaza chupa moja”
“Sawa, hivi ulimuonea wapi Martin kama amepigwa risasi?”
“Nilimkuta karibu na mlango wake akiwa ameegemea ukutani huku ameshika tumbo lake, nilipo mchunguza nikaona kiganja chake kimelowana damu, ikanibidi kumdadisi sana japo alikuwa anaficha mtu asione, katika kuminyana minya ili nione, akaanguka chini na kupoteza fahamu. Nikamuingiza chumbani kwake na tukaanza kumshuhulikia, na katika semehu ya jeraha tuliona amejifunga kitambaa kikubwa ambacho kilizuia kuonekana kwa damu yake”
 
“Daaa”
Nilizungumza huku nikiwa nimejawa na majonzo mengi sana. Ikamalizika chupa moja, dokta akaitoa na kuweka chupa nyingine, kisha akatoka na chipa hii na kuniacha mimi nikiendelea kutoa damu hii.
‘Mungu ni mwema kwa kweli, kugongana kote huku sijapata Ukimwi mmmmmm’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kutazama damu hii jinsi inavyo ingia kwenye dripu. Nesi akaingia ndani ya chumba hichi huku akiwa ameshika dripu alilo toka nalo.
“Vipi?”   
Nilimuuliza huku macho yakiwa yamenitoka sana.
“Martin amekufaa”
 
Nikahisi kama nipo ndotoni, nikajaribu kuyafumbua macho yangu zaidi na zaidi ila hakuna kilicho badilika mbele yangu kwani, daktari ninaye muona na mandhari ninayo yaona ni yale yake. Kwa haraka nikachomo sindani niliyo chomwa kwenye mkono wangu, nikafungua mpira huu na kutoka chumbani humu nikikimbia kuelekea katika chumba cha Martin. Nikiwa ninakaribia mlangoni nikaisikia sauti ya Winy akilia kwa uchungu, nikaingia ndani na kumkuta Winy akiwa amelaza kichwa chake kifuani mwa Martin, Livna amesimama pembeni yake huku naye machozi yakiwa yanabubujika usoni mwake. Daktari amesimama pembeni Livna akiwa ametulia kimya.
 
“Hapana Martin huwezi kufa kizembe hivi”
Nilizungumza huku nikisegelea kitanda cha Martin, nikakaka pembeni ya kitanda hichi na kumtazama usoni mwake.
“Martin acha ujinga basi kuigiza vipi hivi rafiki yangu eheeee”
Niliendelea kuzungumza huku machozi yakinimwagika usoni mwangu. Hawa na Babyanka nao wakafika ndani ya hichi chumba kila mtu aliye muona Martina akiwa amelala hapa kitandani na ameyafumba macho yake kusema kweli roho yake iliweza kumuua kwa staili yake.
 
“Martin si umetoka kuniaga kwamba unakwenda kumchukau mtoto wa K2 jamani mbona umeondoka mapema jamani, ikiwa penzi letu ndio kwanza limeanza jamaniii Martinnnnnnn”
Winy aliendelea kuzungumza machozi yakizidi kumwagika. Nikanyanyuka kiitandani humu na kumshika mkono Livna na kutoka naye.
“Dany tunaelekea wapi jamaani”
Livna alizungumza huku akijaribu kusimama ila nikamshika kwa nguvu na kuendelea kumvuta.
“Mtoto wa K2 na Wamarekani ni lazima walipe kwa hili walilo lifanya, siwezi kumpoteza mtu ninaye mpenda. Martin ni sawa na mdogo wangu”
 
Niliendelea kuzungumza kwa jazba kubwa. Tukaingia katika chumba cha mawasiliano na kukuta kukiwa hakuna mtu.
“Niitie Ester na Logate, waje na huyo kibonge”
Livna akabaki akabaki na bumbuwazi, nikamgeukia na kumtazama kwa macho makali sana, akatoka chumbani humu yeye mwenyewe. Baada ya dakika mbili akarudi akiwa ameongozana na Ester pamoja na Logate.
“Yupo wapi kibonge?”
“Amelala”
“Kamlete, analala hapa kwao. Fanya fasta sawa”
Nilizungumza kwa ukali, Logate akatoka kwa haraka humu ndani kwani kila mmoja nina imani leo hii ndio ananiona nikiwa nimekasirika kwa kiwango hichi.
“Wasiliana na LIVNA”
“Livna!!?”
“K2”
 
Ester akati kufanya kile nilicho muagiaza, haikuisha hata dakika moja nikamuona K2 mbele ya hii video.
“Mbona macho mekundu hivyo unavuta bangi siku hizi?”
Swali la kejeli la K2 likanifanya nizidi kupandwa na hasira, mtto wake akaingizwa humu ndani, alipo muona mama yake kwenye hii tv akakimbilia sehemu nilipo simama.
“Mamaaaa”
K2 akastuka sana kumuoan mtoto wake mikononi mwangu.
“U…..uu….umefikaje huk…..”
K2 alizungumza kwa kigugumizi kikali sana, nikamuona jinsi jasho likimwagika usoni mwake.
“Nipatie bastola”
Nilizungumza huku nikimshika mtoto wa K2 na kumuweka mbele yangu.
 
Livna akanirushia bastola yake, nikaidaka vizuri, nikaikokoki na kuiweka kichwani mwa mtoto wa K2 aliye anza kutetemeka mwili mzima.
“Mtu wangu mmoja amekufa. Martin amekufa kwa ajili yako wewe malaya, pamoja na huyu nguruwe wako. Umemuua Lucy sasa shuhudia ninavyo mfumua ubongo sawa”
Nilizungumza kwa ukali sana.
“Mamamaaaaaaa”
“Dany, Dany ninakuomba, ninakuomba sana nipo chini ya mguu yako, nipo tayari kufanya chochote unacho niagiza hivi sasa”
K2 alizungumza huku machozi uakiendelea kumwagika usoni mwake.
“Dany vita yako ni mimi na wewe, mwanangu hana hatia yoyote katika hii vita…ha……”
“Hana nini mpuuzi wewe, ulivyo muua malaika wangu ambaye hata raha ya dunia hakuwahi kuiona. Hadi leo sitambuu ni wapi walipo zikwa, alafu unaniambia kwamba hana hatia”
“Dady nimekosa, shetani shetani alini……”
Nikampiga risasi ya bega mtoto wa K2 na kumfanya aanguke chini na kuangua kiliok ikali sana. Nikamnyanuyua huku nikimtazama K2. 
 
“Ulihisi nitakushindwa, ulihisi kumuweka mwanao mbali na Afrika, nitashindwa kumuangamiza eheeee”
Niliendelea kufoka, K2 machozi  yaliyo ambatana na makamasi yakazidi kutiririka usoni mwa K2.
“Dany nipo tayari kufa, nipo tayari uniue na mkono wako”
Kilio cha mamuvu cha mtoto wa K2 pamoja na mama yake vikaendelea kutawala hapa. Nikamtazama K2 kwa muda wa dakika moja, kisha nikamsukumia mtoto wake pembeni.
“Unamasaa kumi na mbili hakikisha unajisalimisha kwa mtu nitakaye kuambia”
 
“Niambie tu Dany, niambie mimi nipo tayari kujisalimisha”
“Kwanza kiri dhambi zako kupitia vyombo vya habari, nitakatishe na useme kwamba mimi sina hatia na ugaidi wote huo. Wewe ndio gaidi japo itakuwa ni ngumu kwa watu kunielewa, ila hakikisha kwamba unanisafisha mimi sawa”
“Nitafanya hilo”
“Pili ukimaliza jisalimishe mikononi mwa OSAMA Bin Ladane”
“Osama!!?”
“Fanya hivyo, sihitaji maswali mengi na sihitaji kuwasiliana nawe, nikiwasiliana nawe masaa kumi na mbili yajayo uwe mikononi mwa Osama sawa”
“Sawa nimekuelewa, nimekuelewa Dany”
Nikazima Tv na kumtazama mtoto wa K2 anye endelea kulia hapa chini huku bega lake likiendelea kuvujika damu.
“Mtoeni hapa nisije nikamuua”
Logate kwa haraka akamnyanyua mtoto huyo na kuondoka  naye. 
 
“Dany”
Livna aliniita huku akinisogelea pembeni yangu, akanishika mkono wangu wa kulia na kuichukua bastola yake na kuichomeka kiunoni mwake. Taratibu akanikumbatia huku machozi yakiendelea kumwagika.
“Naogopa Dany, Martin amechukua kifo changu. Yote ni makosa yangu Dany”
“Shiiii…..sio makosa yako, usijilaumu katika hili”
“Kwa nini jamani nisinge mzuia, kwanini eheeeee?”
Nikazidi kumkumbatia Livna. Baada ya dakika kama kumi nikamuachia na kumkalisha kwenye kiti.
“Ester sherehe zote zikatishe, watu wote wavae nguo nyeusi. Tupo kwenye msiba”
Livna alizungumza kwa sauti ya ungonge huku akimtazama Ester usoni mwake.
 
“Sawa mkuu”
“Muje kusafisha hii damu hapa sawa”
“Sawa mkuu”
Masaa yakazidi kusonga mbele huku nikiwa siamini kabisa kwamba Martina amekufa, kwa mara kadhaa nikajikuta nikienda kwenye sehemu maalumu alipo hifadhiwa, kumuangalia kama atanyanyuka kutoka katika usingizi ila ndio hiyo hata kufumbua macho yake hawezi. Uhodari wake na kujitoa kwake kote kumeishia hapa.
“Samahani kwa kukusumbua”
Daktari aliye muhudumia alizungumza huku akiingia akirudishia mlango wa chumba hichi maalumu cha kuhidadhia maiti.
 
“Kwenye nguo za Martin tumeikuta hii karatasi, nina imani kwamba ni ujumbe wako”
Daktari akanikabidhi karatasi hii iliyo kunjwa vizuri, kisha akatoka chumbani humu. Taratibu nikaifungua na kuanza kuisoma humu ndani.
{Dany kaka, ninajua utaumia sana kuona siku moja nikiwa nimeondoka duniani. Ninautambua upendo wako mkubwa unao zidi kuuonyesha kwangu mimi. Leo hii roho yangu imekuwa ni nzito sana, sijui kama siku ya leo kama nitaimaliza. Ninawaona rafiki zangu wa boko haramu wakiniita niwafwate kule walipo, natamani kubaki na wewe, ila muito wao ni mkubwa sana……}
Nikajikuta nikimwagikwa na machozi yaliyo anza kuidondokea karatasi hii, nikajifuta kisha nikaendelea kuisoma.
 
{……Sina jinsi kaka itabidi niondoke nikuache peke yako. Sijui ni kwa nini ninajikuta ninaandika maneno haya ila moyo na hisia zangu zinanisukuma kuandika hivi. Sijawahi kufanya kazi na mtu cheshi kama wewe, japo watu wa nje wanakuchukualia wewe vibaya, ila kusema kweli nimefurahi sana kufanya kazi kwako. Umenifanya niwe mahiri, japo ilikuwa ni hatari ila hukusita kunitetea na kunielekeza nini cha kufanya pale nilipo hitajika kufanya hivyo. Bro walinde watu wako, hakikisha maadui zako unawamaliza wote na baada ya hapo kaka mrudie Mungu wako, kwani yeye ndio atakuwa muamuzi wa mwisho pale siku ya mwisho itakapo wadia. Ninakuependa sana kaka Dany na Mungu azidi kukulinda. Amen}
 
Kijikatuni kidogo alicho kichora Martin hapa chini ya barua yake kinachomuonyesha amenipigia saluti kikanifanya nizidi kulia kwa uchungi tena kwa sauti ya juu sana. Kusema kweli kutoka moyoni mwangu, kifo cha Martin kinaniuma sana. 
 
Hadi kunapambazuka sijapata hata lepe la usingiza zaidi ya kukaa pembeni ya mwili wa Martin ambao umechomwa sindao maalimu ya zuia kuto kuoza. Nikasimama wima, kisha nikapiga saluti huku machozi yakiendelea kunitiririka usoni mwangu. 

Nikatoka katika chumba hichi, kila msichana ninaye muona amevaa nguo nyeusi ikiashiria kwamba msiba huu umewagusa wote japo wengine. Nikaelekea chumbani mwa Livna na kumkuta akiwa amekaa kitandani, machozi uyamemjaa mwilini mwake na mkononi mwake ameshika pete ya ndoa.
 
“Japo nilichukulia ni jambo la kupita, ila pete hii inanikumbusha tabasamu lake. Kusema kweli Martin alikuwa ni mcheshi sana. Alijitoa kwa ajili yangu, japo nilimuumiza moyo wake na nikashindwa kujali hisia zake, ila bado aliona umuhimu wangu kwake.”
 
Livna alizungumza kwa sauti ya upole sana huku macho yake yote ameyaelekezea kwenye pete hii ya dahabu anayo endelea kuizungusha zungusha taratibu.
 
“Martin kusema kweli sipati mfano wake, jana aliweza kunilinda kwa kila namna kwa maana yeye ndio alikuwa mtu wa kwanza kuzinduka baada kuzima. Kusema kweli alijikaza, kupigwa risasi na kutembea nayo pasipo kuonyesha dalili yoyote ya maumivu, kusema kweli amejikaza”
 
Livna aliendelea kuzungumza, mlango ukagongwa.
“Nimesema sihitaji kusumbuliwa leo nahitaji kichwa changu kutulia”
Mlango ukafunguliwa akaingia Ester na kusimama mbele yetu.
“Kuna nini tena Ester, hujasikia nilicho kuambia?”
“Samahani mkuu ila hili swala ni muhimu sana. Ninawaomba mukaone”
“Ni nini?”
Nilimuuliza Ester huku nikinyanyuka kitandani na kusimama.
“Ni vyema tukaenda kujionea”
Hatukuwa na namna zaidi ya kutoka humu ndani, moja kwa moja tukaeleka hadi chumba cha mawasiliano. Tukamkuta K2 akiwa amesimama kwenye Tv hii, usoni mwake amejawa na tabasamu pana sana. 
 
“Nashukuru kwa kuja pole kwa msiba Dany wa huyu nguruwe wako. Ninahitaji tufanye biashara ya amani, niachie mwanangu nikupatie huyu”
K2 akamsogeza Yemi mbele yake, akamkaba kabali ya shingo na kumuweka bastola begani mwake.
“Ninawashukuru Wamarekani kwa kuniletea hii zawadi nono. Sasa ni kidonda kwa kidonda”
K2 akafyatua risasi iliyo toboa bega la Yemi na kumfanya alie kwa uchungu sana hadi nikabaki nikitetemeka mwili mzima kwa hasira kali sana.

ITAENDELEA
‘Haya sasa K2 amekabidhiwa Yemi kutoka mikononi mwa Wamarekani ikiwa ni njia ya pekee itakayo mfanya Dany kutoka mafichoni mwake... je Dany atakubali kumuachia mtoto wa K2? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
 
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )