Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 184 na 185 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA   
   
Hatukuwa na namna zaidi ya kutoka humu ndani, moja kwa moja tukaeleka hadi chumba cha mawasiliano. Tukamkuta K2 akiwa amesimama kwenye Tv hii, usoni mwake amejawa na tabasamu pana sana.
“Nashukuru kwa kuja pole kwa msiba Dany wa huyu nguruwe wako. Ninahitaji tufanye biashara ya amani, niachie mwanangu nikupatie huyu”
K2 akamsogeza Yemi mbele yake, akamkaba kabali ya shingo na kumuweka bastola begani mwake.
“Ninawashukuru Wamarekani kwa kuniletea hii zawadi nono. Sasa ni kidonda kwa kidonda”
K2 akafyatua risasi iliyo toboa bega la Yemi na kumfanya alie kwa uchungu sana hadi nikabaki nikitetemeka mwili mzima kwa hasira kali sana.

ENDELEA       
Kilio cha Yemi kikaendelea kutawala humu ndani, hazikupita hata dakika tano akaanguka chini na kupoteza fahamu.
“Nipatie mwanangu, nikupatie huyu malaya wako la sivyo ninamuua huyu malaya. Sharti nilazima uje wewe katika mabadilishano akija mtu tofauti na wewe nilazima nitamuua”
Nikaichukua rimoti iliyopo mezani na kuzima hii Tv, nikashusha pumzi nyingi huku nikikosa kitu cha kuzungumza.
“Dany”   
“Namm”
“Tunafanyaje?”
“Sijui kwa kweli”
“Samahani wakuu ila ninaomba nishauri kitu”
“Zungumza tu Ester”
 
“Mimi ningeona tufanye kwanza mazishi ya Martin baada ya hapo tutajua ni kitu gani tunaweza kukifanya juu ya K2”
“Wazo zuri, Dany tufanye kwanza mazishi ya Martin”
“Tutamzika wapi?”
“Utaratibu uliopo hapa, huwa mtu akifariki tunamchoma moto kisha majivu yake tunayamwaga baharini”
Nikakaa kimywa kwa muda huku nikimtazama Livna usoni mwake, kisha nikatingisha kichwa kwa kukubaliana na utaratibu wao wa mazishi. Taratibu za mazishi zikaanza, baada ya masaa mawili, sote tukakusanyika katika ukumbi mkubwa. Msichana mmoja akaongoza sala iliyo fanyika kwa imani ya kikristo. Baada ya hapo  mwili wa Martin ukaingizwa kwenye chumba maalumu cha kuchomea miili, sikuhitaji kukaa karibu kabisa na chumba hicho kwani sihitaji kusikia mzinga wa kichwa cha Martin kikipasuka katika moto. 
 
“Dany”   
Hawa aliniita na kunifanya nimgeukie na kumtazama usoni mwake.
“Ninaweza kuzungumza nawe?”
“Ndio”
Tukaka kwenye viti vilivyopo katika mgahawa uliopo humu ndani ya hii meli.
 
“Ninaimani kwamba bado una chuki na mimi ila….”
“Kwa sasa sihitaji kuzungumzia mazungumzo hayo, zungumza jambo la muhimu unalo hitaji kuzungumza na mimi”
“Samahani kama nimekuudhi, ila pole kwa yaliyo mkuta rafiki yako”
“Ni hilo ndio ulihitaji kuzungumza?”
Kabla Hawa hajanijibu kitu chochote, nikamuona Ester akija huku kwa kasi akasimama pembeni yangu na kininong’oneza.
“Osama anahitaji kuzungumza na wewe, ameweza kufahamu ni wapi alipo Yemi”
“Ni wapi?”
“Tanzia”
Kwa haraka nikasimama pasipo kumuaga hawa nikaondoka eneo hili na moja kwa moja tukaelekea katika chumba cha mawasiliano na kumkuta Osama akizungumza na Livna.
“Dany nina habari njema”
“Ndio”
 
“Yemi kwa sasa yupo Tannia na vijana wangu tayari wamesha ingia nchini hapo”
“Mumefahamu anashikiliwa na nani?”
“Ndio, anashikiliwa na raisi wa nchi hiyo  je tumlete raisi huyo akiwa hai au amekufa”
“Ninamuhitaji akiwa hai, mukimkatama sehemu yoyote niambieni mimi nitafika sawa”
“Sawa baada ya masaa kumi nitakufahamisha ni wapi tukutane nina imani vijana wangu watakuwa wamesha ikamilisha kazi hiyo”
“Sawa nitashukuru sana”
“Sawa ila pole kwa msiba wa rafiki yako Martin”
“Asante”
 
Tv ikazimwa na Livna.
“Unatakiwa ukayamwage majivu ya rafiki yako baharini”
“Muda huu?”
“Ndio”
Tukatoka chumbani humu na kuelekea juu kabisa ya meli hii, nikakabidhiwa chungu kilicho jaa majivu ya mwili wa Martin. Taratibu nikachoa majivu haya na kuanza kuya mwaga baharini, zoezi  hili nikasaidiana na Livna, Winy pamoja na Babyanka.
“Mwezetu ametutoka, kifo chake tuchukulie kama changamoto. Tutambue tupo kwenye changamoto kubwa, tupo katika vita. Tupo katika hali ya kupambana, sasa inakwenda kuisha, sasa nilazima kuwaagusha maadui walio baki mbele yetu. Si K2 wala Marekani”
 
Nilizungumza kwa msisitizo huku machozi yakinilenga lenga usoni mwangu.
“Baada ya masaa kumi, kila kitu kitaelekeweka, ninajua sasa hivi Wamarekani wameungana na K2, na sasa watakuwa wanashirikiana kwa kila jambo, sasa ninacho hitaji ni kunzisha vita. Acha dunia ilie kwa uzumbe wa viongozi wao”
Niliendelea kuzungumza huku nikiwatazama wezangu hawa walio simama mbele yangu.
 
“Ninahitaji kila mmoja wenu kuhakikisha kwamba masaa kumi yanayo kuja dunia nzima imesha badilika, niwakati wa vita niwakati watu kuweza kunifahamu mimi kama wanavyo mfahamu Adolf Hitler”
Watu wote wakaka kimya wakinitazama usoni mwangu.
“Dany natambua kwamba hupendi huruma yangu wala hupendi jinsi ninavyokuwa ninakushauri. Wewe sio gaidi, wewe ni mtu mwema,  kwa nini wengine walie kwa ajili ya watu wachache. Kuna wamama, kuna watoto ambao hawana hatia ya vita ambayo unakwenda kuianzisha. Tafadhali Dany nipo chini ya miguu yako”
 
Babyanka alizungumza na kupiga magoti chini huku akimwagikwa na machozi chini. Taratibu Winy naye kapiga magoti chini akiwa ni mnyonge sana. Kilicho zidi kunishangaza zaidi ni Livna naye kupiga magoti chini, wasicha walipo katika eneo hili nao wote wakapiga magoti chini kuniomba nigairi kwa maamuzi yangu niliyo yapanga. Nikawatazama kwa muda kisha nikaondoka eneo hili, nikaelekea chumbani kwangu na kujitupa kitandani. Hazikupita hata dakika kumi akaingia Livna huku akiwa mnyonge sana 
 
“Dany”
Livna alizungumza huku akinisogea akaka pembeni yangu huku akinitazama usoni mwangu.
“Samahani kwa kuweza kukutatisha tamaa katika lile ambalo umekusidia kulifanya. Jana nilitoka kukuambia kwamba ninahitaji kuzaa na wewe, alicho kizungumza Babyanka kusema kweli ni kitu cha muhimu hakuna haja ya watu wengine kuingia kwenye vita kwa ajili y….”
“Nimekuelewa”
Ilinibidi kumkatisha Livna sentensi yake kwani anahitaji kuzungumza kitu kule kile ambacho tayari walisha kizungumza.
“Ninakuomba nipumzike, ninahitaji kulala. Osama akihitaji kuwasiliana nami ndio muniamshe”
“Dany sijamaliza kuzungumza mpenzi wangu”
“Kuna kitu gani hapo cha kuzungumza Livna?”
 
Livna akakaa kimya baada ya kuniona nimekasirikia sana. Taratibu akanyanyuka na kuanza kutembea kueleka mlangoni, nikamtazama jinsi alivyo mnyonge kwa haraka nikasimama na kupiga hatu za haraka sana hadi mlangoni na nikauegemea.
Nikamvuta Livna kifuani mwangu na kuanza kumnyonya mdomoni, nikamnyanyua juu juu, nikamlaza kittandani huku nikiendelea kumnyonya midomo yake, Tukaanza kuvuana nguo, nikayashika  ya Livna kwa pamoja na kuyakutanisha semu moja, nikaanza kuyanyonya kwa fujo na kumfanya Livna kutoa kilio cha mhaba.
Shuhuli ya kuburudishana ikaanza, kila mmoja safari hii anajitahidi kuhakikisha kwamba anamburudisha mwenzake, Livna hakuihitaji kuwa mnyonge sana kama mara ya kwanza,
 
“Dany ninakupenda mume wangu, ninakupenda mume wangu,"
 
“Una uhakika gani kwamba ni mwanao aliyopo tumboni, ikiwa Martin alinisimulia kwamba Yemi alichukuliwa na aliyekuwa mume wake”
“Mimi ndio ninaye fahamu kitu gani ambacho kimetokea kati yangu mimi na Yemi. Japo aliondoka akiwa ananichukia ila hawezi kuzaa na mwanume yule”
“Sawa Dany swala hilo sihitaji kuliingilia sana”
“Poa”
Baada ya muda mchache tukajikuta nikipitiwa na usingizi mzito sana.
“Dany, Dany”
“Mmmmm”
“Amka muda umekwenda limebaki lisaa moja tu yatimie masaa kumi, ninaimani kwamba Osama ndani ya muda huo atawasiliana nawe”
 
Nikamtazama Livna kwa macho yaliyo jaa usingizi, taratibu nikajivuta kitandani na kukaa kitako.
“Bado nina usingizi nina siku nyingi sijalala vizuri”
“Amka bwana, nenda ukaoge upande nguvu”
Livna akaendelea kunishawishi hadi nikajikuta nikiamka taratibu kitandani, nikaingia bafuni na kuoga, nirudi chumbani na kukuta Livna akiwa ameniandalia nguo nyingine za kuvaa tofauti na nguo za jeshi nilizo kuwa nimevaa. Tatatibu nikaanza kuvaa nguo hizi ambazo zote ni nyeusi kuanzia suruali hadi tisheti. 
 
“Umependeza mpenzi wangu”
“Asante, saa ngapi hivi sasa?”
“Ni saa tato usiku”
“Mmmmmm”
“Yaaa, ndio maana nimekuamsha mpenzi wangu”
Tukatoka chumbani humu na kueleka katika chumba cha mawasiliano. Tukawakuta Logate na Ester wakiendelea na kazi.
“Hamulali jamani?”   
Niliwauliza huku nikikaa kwenye kiti ambacho nimezoea kukaa nikiwa ofisini humu.
“Tukilala sisi mkuu hakuna kitu kinacho weza kwenda”
“Sawa sawa, ninashukuru kwa kujitoa kwenu”
“Usijali ni jukumu letu”
 
“Vipi kuna mpya yoyote hadi sasa?”
“Hapana”
“Hembu fwatilieni kuna mpya yoyote kutoka Tannia”
“Sawa”
Ester na Logate wakaendelea kufanya kile nilicho waagiza, baada ya dakika tano, Ester akanitazama usoni mwangu huku akiwa na tabasamu kubwa.
“Kuna website moja imeandika kwamba raisi wa Tanania amepotea katika mazingira ya kutatanisha”
Taarifa hii ikanifanya nianze kupata matumaini makubwa ya kuamini kwamba Osama Bin ladanen na way wake wameifanya kazi ambayo waliniahidi kwamba wataifanya.
 
AISIIIII……….U KILL ME 185

“Website hiyo munaweza kuiamini kweli je ikiwa imezusha story za uongo?”
Livna alizungumza huku akitutazama usoni.
“Mkuu hii website ni ya uhakika hata taarifa zake ni za uhakika”
“Serikali ina mamlaka ya kuambia website, blog ziandike chochote wakitakacho wewe na mukumbuke kwamba K2 ni mtu mmoja mjanja sana, mukumbuke kwamba ana uwezo wa kubadilisha moja ikawa mbili na mbili ikawa moja kama alivyo yafanya maisha ya Dany hapa”
 
Maneno ya Livna kidogo yakakata matumaini yangu yote niliyokuwa nayo juu ya hii taarifa.
“Tusubirini tuone kitakacho si limebaki saa moja?”   
“No zimebaki dakika kama arobaini na tano  hivi”
“Sawa”
Tukajaribu kufwatilia ya kutekwa kwa K2 kwenye vyombo vya habari vya Tanzania, ila hakuna kituo chochote cha Tv kilicho tanganza kutekwa kwa raisi. Hadi lisaa moja linakwisha hapakuwa na taarifa yoyote  kutoka kwa Osama Bin Laden.
“Umeona, niliwaambia hiyo website imefanya kitu walicho elezwa na K2” 
 
Livna alizungumza na kunifanya nikae kimya pasipo kuzungumza kitu chochote.
“Hembu jaribu kumpigia Osama video call”
Ester akaanza kazi ya kumtafuta Osama Bin Laden hewnai.
“Hapatikani”   
Ester alizungumza kwa sauti ya upole.
“Shitiii…..”   
“Ninahisi kuna mpango ambao  unaendelea”
Livna alizidi kuzungumza na kunifanya nifikirie ni kitu gani ninaweza kuzungumza.
“Osama anaweza kuwa msaliti kwetu”
Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo.
 
“Tumpe muda?”
“Muda gani tena hapo?”
“Jamani kuna hichi munatakiwa kukiona”
Logate alizungumza huku macho yakiwa yamemtoka. Tukaona video ambayo inaonyesha nje ya ikulu , gari mbili aina za Range rover nyeusi zilisimama, wakashuka waarabu wawili walio valia kanzu huku wakiwa na bunduki, akashuka Osama, tukamuona K2 akitoka ndani ya ikulu hiyo akisalimiana na Osama huku wakipeana mokono wakioneakana ni watu wanao juana kwa muda mrefu sana. Video hiyo ikawaonyesha watu hao wakiingia ndani, hazikupita hata dakika tano zikaja gari nyingine mbili zikiwa na bendera za Marekani ikiasiria kwamba anaye fika hapo ni kiongozi wa Marekani.Wakashuka walinzi wanne kisha akashuka mwanamama mrefu na mweusi .
 
“Ni nani huyo?”
Livn akanyanyuka kwenye kiti kikalia akasogelea karibu kabisa na Tv hii akionekana kuwa na wasiwasi.
“Ni balozi wa Marekani anaitwa Bi Efracia Godwin”
“Haiti Efracia hilo ni jina feki”
Livna alizungumza kwa msisitizo huku akiendelea kumtaza mwanamama huyo.
 
“Jina lake ni Livna Tomsond miaka ishirini iliyo pita nilikuwa naye kwenye chuo kitengo cha FBI, ila mimi nilikwenda kama undercover kwenye kitengo hicho. Kama sasa hivi ni balozi basi tupo katika hali ya hatari”
“Kwa nini?”
“Ana roho mbaya ya Osama ni ndogo, nina imani kwamba yeye ndio mshawishi mkubwa kwenye nchi yake hadi wameamua kukaa meza moja na Osama. Tagert ya kwanza watakayokuwa wanaijadili hapo ikulu ni juu yetu sisi”
Livna aliendelea kuzungumza kwa msisitizo mkubwa sana.
“Tukumbuke kwamba tunapigana na vita na watu watatu, wote wana uwezo, sisi tupo peke yetu.”
 
“Ningependa kupata majina yote yenye uhasama mkubwa na Marekani, tunatakiwa kuzishawishi hizo nchi ili kutengeneza kikosi ambacho wakituanza tu, basi nasi tutapata msaada”
“Ni nchi gani ambayo kwa sasa inaweza kutoa jeshi pamoja na silaha zake kutusaidia sisi ambao si nchi na tunahesabiwa kama kikundi cha kigaidi?”
“Naomba hiyo listi ya nchi japo tano tu, mimi nitajua ni kitu gani cha kuzungumza”
“Sawa, mimi ninanza ya Korea ya Kaskazini, Russia. Nyingine Ester zitafuteni”
“Sawa mkuu”
 
“Kabla hamjazitafuta hizo nyingine tatu ninaomba nizungumze na raisi wa Russia”
“Raisi wa Russia!!!!?”
“Ndio mbona unashangaa?”
“Mmmmm Dany sidhani kama hilo ni wazo zuri kuwasiliana na raisi huyo ni mkali sana”
“Ukali wake ni katika kuiongoza nchi yake na kuilinda nchi yake ila ninacho kihitakuzungumza naye ni kitu muhimu”
Wakatekeleza kile nilicho waomba, baada ya dakika kumi ikulu ya Russia ikakubaliana na ombi la mimi kuzungumza na raisi wao. Nikavaa earphone inayoweza kubadilisha lugha yoyote na kuwa katika lugha ya kiswahili.
 
“Habari yako muheshimiwa raisi”
“Wewe ni nani?”
Raisi huyu mwenye sauti nzito aliniuliza huku akinikazia macho.
“DANY”
“Ndio nani?”
“Kifupi mimi ni gaidi, vita yangu ninajitahidi kupambana na Marekani, katika siku mbili hizi nimeweza kuifanya Marekani kukaa katika hali ngumu ya wasiwasi mkubwa, je umenifahamu”
 
“Zungumza nini unahitaji kwangu”
“Ninahitaji kuiangusha Marekani. Mimi sio raisi wala sina nchi ya kuipigania, ila wewe ni raisi na una nchi ya kuipigania. Unapenda nchi yako kupitwa kiuwezo wa kiuchumi kijeshi na Marekani?”
Swali langu likamfanya raisi huyu kukaa kimya kwa dakika kadhaa huku akionekana kuwa mdadisi mkubwa sana kwangu.
“Nikisiema sipendi unahisi utafanya nini?”
“Ninahitaji kuungana na wewe, ninahitaji kuanza kuishambulia Marekani, tazama jinsi alivyo kuwekea vikwazo katika kutengeneza silaha za nyuklia na yeye anatengeza je unahisi nini. Ni ubabe au amekufanya uwe mnyonge?”
 
“Nchi yangu kwa sasa haipo tayari kupambana na nchi ya aina yoyote ninahitaji nchi yangu iwe na amani”
“Ni amani gani uliyo nayo ikiwa Ukrain inakusumbua. Hii ndio nafasi ya wewe kuiongoza dunia, ukishindwa sasa hivi hadi mwisho wa dunia huto weza kushika namba moja kama aliyo nayo Mmarekani. Haya mazungumzo laiti kizazi kinacho fwata kwenye nchi yako kikija kuyaona au  kuyasikia watakulaumu kwani umeshindwa kutengeneza future nzuri kwao na watabaki kuwa mbwa wa Marekani ha…..”
 
“Tulia”
Raisi huyu alizungumza kwa sauti nzito huku akiunyanyua mkono wake mmoja, nikanyamaza huku nikiendelea kumkazia macho.
“Unazungumza sana, nipe muda nitakujibu”
“Kuwa makini, kwa maana vita ninayo kwenda kuianzisha duniani, usipo jipanga na wewe taifa lako linakwenda kufitika duniani. Kama nimemuweza Mmarekani, basi kukuweza wewe pia ninaweza”
“Kijana uinajiamini nini?”
“Unahisi  kwamba ninajiamini na nini?”
“Nionyeshe unajiamini na nini?”
Nikavua earphone moja kisha nikamgeukia Ester aliyekaa pembeni ya Logate.
 
“Kuna kitu gani ambacho tunaweza kukifanya kwa huyu mtu?”
“Tuelekeze mabomu yake ya nyuklia kwenye mji wake wa Mossow?”
“Itachukua muda gani kwa yeye kuweza kugundua?”
“Ndio tunamalizia kuyaelekezea kwenye mji wake mwenyewe?”
“Itamchukua muda gani?”
“Sekunde hamsini hazifiki”
Taratibu nikavaa eaphone hii na kumgeukia raisi huyu.
“Muheshimiwa unahakika na kitu ambacho umekizungumza kwamba ninajiamini kwa kitu gani?”
“Ndio”
Hata kabla sijanyanyua kinywa changu, msichana aliye valia nguo za jeshi akaonekana kwenye video, akamnong’oneza raisi wake. Raisi akaonekana kustuka, akanitazama kwa macho makali yaliyo jaa wasiwasi mkubwa.
 
“Je unahitaji nikuaminishe kwa vitendo?”
“Hapana sihitaji vitendo, nipe lisaa nijikirie na ninahitaji kujadiliana na kamati yangu”
“Muda ni wako”
“Shukrani kwa kunisikiliza muheshimiwa raisi”
Nikazima Tv hii huku nikimgeukia Livna nikiwa na tabasamu pana usoni mwangu.
“Mmmm si kwa biti hilo, yaani kauli  yangu haijaanguka”
“Kauli gani?”
“Ile niliyokuambia kwamba ninahitaji kukufanya uwe gaidi, ni kweli umekuwa gaidi tishio hadi kwangu sasa”
“Hahahaaa, eheee raisi wa Kaskazini mwa Korea naye vipi?”
“Tunasubiria majibu yetu kujibiwa, kwani tayari tumesha pelekea maombi”
“Ila si munaficha sehemu ambayo tupo?”
“Ndio nilazima tufiche, na jinsi wanavyo ona wao sehemu uliyo ona ni kwenye sayari nyingine ambayo ninaimani kwamba wanapata wasiwasi.”
 
“Sayari nyingine?”
“Ndio winaonyesha sisi tupo sayari ya Mars na si duniani”
“Duu kweli hilo lazima wachanganyikiwe”
“Ombi limekubaliwa, wanaomba dakika tano raisi wanajiandaa”
Logate alizungumza huku akiwa amejawa na furaha.
“Kazi nzuri Logate, je kikao chao hakijaisha?”
“Bado nahisi wana mipango mikubwa wakitoka nitawajulisha”
“Raisi yupo online sasa unaweza kuwasha Tv”
Ester alizungumza, nikajiweka vizuri nguo yangu niliyo vaa, nikawasha Tv hii na kukutana na raisi wa Korea Kaskazini ambaye siku zote ninamuona kwenye Tv na anashria zake kali sana na ana maamuzi ya kipeke yake peke yake.
 
“Muheshimiwa raisi”
“Habari yako Dany”
Aliuzungumza huku akiwa amejawa na tabasamu tofauti na raisi wa Russia.
“Salama muheshimiwa raisi?”
“Nimefwatilia harakati zako kusema kweli ni harakati ambazo zimenivutia sana ila nikawa ninajaribu kukutafuta tangu jana ila nikawa ninashindwa kwani sikujua ni wapi unapo patikana”
 
“Basi Mungu ameamua kutukutanisha muheshimiwa raisi, nimekuja kwako na ombi moja”
“Ombi gani?”
“Ninaimani umeweza kukiona nilicho kifanya kwa Marekani, nina imani kwamba hakuna mtu aliye weza kukifanya hicho kitu. Nanitaji nchi yako iwe namba moja duniani. Mimi sio raisi wala sina nchi ila wewe unayo inchi na raisi je unakubali kuwa chini ya Marekani miaka yote hiyo?”
Ilibidi nitumie ujanja huo ili kuwaroga maraisi hawa, ambao watashirikiana nami katika kupambana ila mwisho wa siku watajua wao wenyewe nani atakuwa namba moja.
 
“Nipo tayari kukupa msaada wangu kwa asilimia mia moja, wewe niambie ni lini na saa ngapi tuanze kufanya mambo kwa maana ninaona ninafanya tu majaribio ya makombora yangu ila nashindwa kujua ni nani nimtupie japo mawili matatu, akijinyanyua tu kurudisha majibu basi mimi ninaye”
Raisi huyu alizungumza kwa furaha sana.
 
“Ninashukuru sana muheshimiwa raisi, ninakuomba usubiri simu yangu. Kabla ya siku ya kesho kuishi nitamjaribu tena Mmarekani, akiona hivyo ninakuomba na wewe ujaribu makombora yako mawili matatu yaliyo shiba, akitujibu, basi ninaimani kesho haiisi atakuwa amebaki magofo kama ilivyo Iraq”
“Wewe ndio watu ninao wahitaji hapa duniani, sio kuwa na maamuzi ya ajabu ajabu. Ninahitaji nguvu basi nguvu yanu umeipata mdogo wangu”
“Shukrani muhshimiwa raisi”
“Ninakukaribisha”
“Shurkani”
Tukaagana na raisi huyu w Korea Kaskazini, nikanyanyuka kwenye kiti nilicho kali huku nikiwa nimejawa na furaha kubwa sana kwani mpango wangu niliokuwa nimeupanga umekwenda sawia.
 
“Tumepata nchi nyingine ambazo zina chuki na Marekani, ila hazina nguvu kubwa ya kuweza kutusaidia katika mpango wetu”
“Ziacheni, tusije tukazisababishia matatizo makubwa ikiwa wenyewe wana matatizo yao”
“Sawa”
“Naona kikao chao cha siri kimekwisha, je tuwafanyaje?”
“Unamaanisha nini Logate?”
“Kana ni kuwashambulia hapa sasa hivi tunaweza kuwashambulia?”
“Tusiwashambulie sasa hivi”
 
“Kwa nini?”
“Ninahitaji kukutana na Livna, kuna mambo mengi sana ninahitaji kumuhojia”
“Mambo gani hayo?”
“Utafahamu siku tukionana naye”
“Sawa”
“Ester andaa kikosi ambacho kitakwenda kumkomboa Yemi na kumrudisha hapa, watu wote wakiwa ndani ya hii meli nina ikani kwamba hakina mwengine ambaye ataweza kutuumiza kichwa huko nje, tukishambulia tumewashambulia”
Livn alizungumza kwa msisitizo.
“Livna huoni kwamba inaweza kuwasababishia matatizo hao wanakwenda huko?”
 
“Wanakwenda wasichana wawili tu, hao wanauwezo mkubwa wa kufanya chochote kinachokuja mbele yao, na wakishindwa hao  basi ujue hakuna yoyote atakaye weza kufanya oparesheni hiyo”
“Ninahitaji kuwaona wasichana hao kabla ya kwenda”
“Sawa”
Tuakanyanyka kwenye viti tulivyo vikalia na kutoka ndani humu, tukashuka chini kabisa ya meli hii ambapo kuna ndege kadhaa za kivita, na eneo zima limetawaliwa na rangi nyekundu.
“Mbona kuna taa nyekundu?”
“Huku huwa hashuki mtu wa aina yoyote zaidi yangu mimi, na aliyeweza kuja huku ni Logate tu, ila wasichan wengine hawakuwahi kuja huku”
 
“Sasa wasichana hao  wapo huku chini?”
“Ndio wanaishi huku chini, wapo nane tu, wasichana hawa ni hatari kuliko unavyo fikiria, na akili zao yaani zipo kama zimechanganyikiwa fulani hivi, wanaye msikiliza ni mimi sasa chochote watakacho kuambia ninakiomba uwe mpole, ukileta ujinga watakua, na mimi nitashindwa hata kukutetea sawa”
Livna alizungumza huku tukiwa tumesimama nje ya mlango huu wa chuma.

 Akaweka kiganja chake cha kulia katika sehemu ya kufungulia mlango huu, ukakaguliwa na mionzi ya rangi nyekundu, baada ya sekunde kadhaa ikabadilika na kuwa na rangi ya kijana. Mlango ukafunguka, tukakaribishwa na mwanga mweupe, eneo hili limejengeka vizuri na lina kila kitu cha ndani, akatoka msicha mmoja mzuri kwenye moja ya chumba, akamtazama Livna akatabasamu, alipo geuza macho yake kwangu akakasiria akaanza kutembea kwa kasi na kunifwata sehemu nilipo simama, nikaanza kuridi nyuma nyuma kwa bahati mbaya nikagota mlangoni na tayari mlango umesha funga. 

Msichana huyu akasimama mbele yangu, akanikaba koo langu kwa mkono wa kulia, sikuwa na jinsi zaidi kujitahidi kuutoa mkono wake, cha kushangaza Livna akatingisha kichwa akiniomba niitoe mikono yangu kwenye mkono wa msichana huyu ambaye nikimuachia basi habari yangu ya kuishi duniani itaisha kizembe kwani hapa nilipo nimesha anza kuhisi pumzi kuniisha na haja kubwa nanisi ina dalili ya kunitoka muda wowote kwa maana  kukabwa koo sio mchezo.
 
ITAENDELEA
‘Hay sasa Dany amesha pata ushirikiano na maraisi wa nchi mbili ambazo zina uhasama mkubwa na Marekani, ameingia kwenye chumba ambacho ni cha wasichana hatari, je atatoka salama ikiwa anakaribia kufa? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )