Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 13, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 186 na 187 )

adv1
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588 
ILIPOISHIA      
 
Mlango ukafunguka, tukakaribishwa na mwanga mweupe, eneo hili limejengeka vizuri na lina kila kitu cha ndani, akatoka msicha mmoja mzuri kwenye moja ya chumba, akamtazama Livna akatabasamu, alipo geuza macho yake kwangu akakasiria akaanza kutembea kwa kasi na kunifwata sehemu nilipo simama, nikaanza kuridi nyuma nyuma kwa bahati mbaya nikagota mlangoni na tayari mlango umesha funga. 

Msichana huyu akasimama mbele yangu, akanikaba koo langu kwa mkono wa kulia, sikuwa na jinsi zaidi kujitahidi kuutoa mkono wake, cha kushangaza Livna akatingisha kichwa akiniomba niitoe mikono yangu kwenye mkono wa msichana huyu ambaye nikimuachia basi habari yangu ya kuishi duniani itaisha kizembe kwani hapa nilipo nimesha anza kuhisi pumzi kuniisha na haja kubwa nanisi ina dalili ya kunitoka muda wowote kwa maana  kukabwa koo sio mchezo.

ENDELEA   
Msichana huyu akanitazama kwa muda kisha akaniachia na kujikuta nikikaa chini huku nikikohoa sana kwani pumzi zimeniishia kabisa.
“Mkuu huyu ni nani?”
Msichana huyu aliuliza kwa sauti ya upole sana hadi nikajikuta nikishangaa.
“Anaitwa Dany ni rafiki yetu mpya tutakuwa naye hapa”
“Mzuri, naweza kumgusa tena”
“Ahaaa sio kihivyo bwana”
Nilizungumza huku nikijizoa zoa chini nilipo kaa na nikanyanyuka. 
 
“Kivipi Dany?”
Msichana huyu aliendelea kuzungumza kwa upole sana. Sihitaji hata kumuamini, kwani alicho nifanyia ni nusu ya kufa
Wakatoka wasichana wengine, alipo niona wakaonekana kunishangaa sana. Wakamsalimia Livna ila mimi hawakunisalimi wote wana kazi ya kunitazama kwa dharau huku wakinishusha na kunipandisha kwa macho yao. 

Mbaya zaidi hawa wasichana wote ni wazuri, hakuna hata mmoja ambaye ana ubaya wa sura wala mwili, ila roho zao ndio hivyo ni mbaya na kuua mtu kwao ni swala la kawaida sana.
“Warembo huyu anaitwa Dany, ni mwezetu yupo nasi hapa kwa kipindi chote cha maisha yetu hapa duniani”
 
“Ngoja kwanza mkuu, huyo yupo nasi kwa kipindi cha maisha yetu yote. Ila yeye ni mwanaume inakuwaje aishi na sisi?”
Msicha mmoja alizungumza huku akinitazama kwa macho makali sana
“Kuwa mwanaume hilo kwetu sisi halina shida sana”
“Ila mkuu utakuwa unavunja utaratibu tulio uzoea”
“Ninaelewa ila kwa sasa mambo yamebadilika, huyu kwa sasa ni tegemezi letu kwa asilimia kubwa”
 
“Samahani mkuu, unasema ni tegemezi. Ana kitu gani cha maana ambacho kinakufanya wewe useme kwamba nitegemezi letu?”
Livna akanitazama kwa sekunde kadhaa kisha akawatazama wasichana hawa huku akishusha pumzi nyingi kwani maswali ya wasichana hawa kwa upande mmoja ama mwengine ni magumu sana.
“Sipendi kuwaamrisha na kuwapa amri kama wezenu huko juu. Dany kwa sasa ndio kiongozi msaidizi. Ninahiji heshima ifwate mkondo wake sawa”
 
Ilibidi Livna azungumza kwa ukali wasichana wote wakabaki kukaa kimya huku wakionekana hawajaridhishwa kwa kitendo cha mimi kuwa humu ndani.
“Mkuu tunakuheshimu na tunaishi huku chini tunakosa raha za kujiachia huo juu huko. Kusema kweli hatujaridhika na majibu yako. Hembu tupe ufafanuzi wa kueleweka huyo jamaa anafanyaje humu ndani ya meli yetu.”
Wasichana hawa wanaonyesha hawana nidhamu ya woga kabisa. Livna akabaki kimya kwa muda huku akionekana kutafakari ni kitu gani atawajibu wasichana hawa.
 
“Nitaondoka kama hamunihitaji kwenye hii meli. Livna umenisaidia sana na ninashukuru kwa kunifikisha hapa, kwa hareni”
Nilizungumza huku nikijiweka sawa shingo yangu.
“Hembu ngoja wewe unaga aga nini?”
Msicha mmoja alizungumza kibabe huku akinitazama usoni mwangu, akaanza kunisogelea taratibu huku akionekana kuhitaji kufanya jambo fulani kwangu.
“Tutakukubali endapo utapambana na mmoja wetu hapa, ukimshinda utakuwa kiongozi wetu kama anavyo hitaji mkuu hapa, ukishindwa utafanya kile tutakacho kuambia kukifanya”
Livna akanitazama na kutingisha kichwa kwamba nikubaliane na pambabo hilo analo lihitaji msichana huyu.
 
“Poa”
“Chagua ni nani hapa upigane naye?”
Nikawatazama wasicha wote hawa, kila mmoja anaonekana ana uwezo wake.
“Ninakuhitaji wewe”
“Mimi hahaaaaaa”
Msichana huyu akaanguka kicheko cha dharau kubwa sana.
“Atakaye shindwa lazima apige mkono chini kuashiria kushindwa sawa”
“Poa”
Nilizungumza kw akijiamini huku nikimtazama msichana huyu. Wote wakarudi nyuma na kutuachia duara kubwa, msichan huyu akaruka hewani huku akirusha teka lililo nifanya niiname chini, kabka hata sijanyuka nikastukia teke jengine likitua kifuani mwangu na kunipeleka chini.
“Kumbe mzembe hivyo, nyanyuka mwanaume, kwa maana hatuwezi kuongozwa na mwanaume ambaye hata kupambana na mwanamke hawezi”
 
Msicha huyu aliendelea kizungumza kwa dharau kubwa sana. Nikanyanyuka na kusimama wima, kama kawaida yangu ya kumsoma ninaye pambana naye ikaanza. Msichana huyu  akaanza kurusha mateke mfululizo pamoja na ngumi kadhaa. Ambazo zote nilizidi kujitahidi kuhakikisha kwamba ninayazuia kwa kadri niwezavyo, huku nikiendelea kumsoma mapigo yake ya kasi. Nikakumbuka siku nilipokuwa ninapambana na mtu wa baba Yemi, ambaye aliamini kwamba mtu hiyo ana uwezo mkubwa sana kuliko mwanajeshi wake yoyote ila nilifanikiwa kumumpiga.
 
‘Umekwisha’
Nilizungumza mara baada ya kuweza kugundua siri zote za msicha huyu japo amenipiga kwa kiasi fulani ila sasa ni muda wangu wa kuhakikisha kwamba ninamdhibiti. Hali ikabadilika kwa msichana huyu kwani mateke ambayo ninayatuma kwake ni mfulilizo na yana guvu kiasi kwamba akikwepa mawili nikimpata moja basi ni lazima apepesuke na akishindwa kupepesuka basi nilazima aanguke chini. Sikuwa na huruma hata kidogo kwa msicha huyu kwani ninahitaji kuwaonyesha uwezo kwamba japo Livna anawasifu wana uwezo mkubwa wa kupambana ila hata wao wenyewe wanabaki wakiwa wamenikodolea macho.
 
Masichana huyu akajifanya kujikaza ili kuto waingiza wezake katika ahadi ambayo ameiweka, ila sikuhitaji kumpa nafasi hiyo, akaanza kunifwata huku akipiga kelele, nikaruka hewani na kumtandika teke moja la kichwa lililo mfanya anguke china na hakunyanyuka tena. 
 
Nikajifuta damu za mdomo zinazo nitaoka huku nikimtazama msichana aliye nikaba koo. Nikawatazama wasichana wengine wote wakaonekana kuingiwa na hofu nami.
“Huyu ndio mkuu wenu?”
Niliwauliza huku nikimnyooshea kidole msicha huyu  aliye lala chini akiwa amepoteza fahamu.
“Musipende kujaribu kurusha mawe kwenye mzinga wa nyuki, mutakufa”
Nilizungumza huku nikielekea mlangoni na kuacha ukimya mwingi ukiwa umeyawala humu ndania.
 
“Njoo unifungulie”
Nilizungumza kwa sauti nzito inayo kwaruza kwaruza.
“Dany”
Livna alizungumza na kunifanya nigeuke nyuma, nikawaona wasichana wote wakiwa wamepiga magoti chini.
“Tunakuomba utusamehe”
Mmoja wao alizungumza, nikaka kimya kwa sekunde kadhaa. Taratibu nikarudi sehemua lipo simama Livna.
“Simameni”
Wakasimamammoja baada ya mwengine.
“Kiongozi wenu ni Livna, mimi hapa sio mkaaji wa kuduma kama alivyo sema mkuu wenu. Muwe na amani juu yangu, sijakuka kumdhuru yoyote kati yenu kwa maana vita yangu si kwa ajili yenu, ni kwa ajili ya Marekani na K2. Ninahitaji msaada wenu”
 
“Msaada gani?”
Msicha aliye nikaba koo langu alizungumza kwa haraka hukua akinitazama usoni mwangu.
“Kuna msicha ninihtaji mukamlete hapa kama inawezekana”
“Msaidieni huyu, nitawahitaji wanne muweze kuiteleza hiyo kazi, Livna anawalete katika chumba cha mawasiliao”
“Sawa mkuu”
Nikatembea hadi mlango, Livna akanifungulia mlango kwa kuweka mkono wake sehemu maalumu ambayo pasipo kuweka mkono wake mlango hauwezi kufunguka. Moja kwa moja nikaelekea chumbani kwangu, nikapitiliza hadi bafuni na kusimama mbele ya kioo kimoja. Nikatazama jinsi nilivyo umia sehemu ya juu ya jicho langu la upande wa kulia. Nikaanza kujisafisha damu zilizo nitawala usoni mwangu, japo msichana yule nimemuhimili ila na yeye amenipa kipondo kila sehemu ya mwili wangu inaniuma.
Mlango wa bafuni ukafungukiwa, akaingia Livna, akasimama pembeni yangu.
 
“Upo vizuri mpenzi”
“Ulihisi nitapigwa?”
“Ndio nilihisi utapigwa kwa maana wasichana wale wapo vizuri”
“Wapi, unatambua kwamba ni jinsi gani nilivyo mbishi. Siwezi kupigwa na msichana ambaye hana hata presha ya kutafutwa na majeshi makubwa duniani”
“Sawa, nikuletee nguo nyingine”
“Kama ikiwezekana”
Livna akajaribu kunishika mbavu zangu ila kwa haraka nikamtoa mkono wake.
“Vipi?”
“Mwili mzima unaniuma, hapa sitamani hata kushikwa”
“Kumbe na wewe umebumundwa”
Livna alizungumza huku akicheka sana. Nikavua tisheti yangu, baadhi ya sehemu zimejaa alama nyeusi nyeusi zinazo onyesha jinsi gani ambayo alama za mateke na ngumi zilivyo jichora.
 
“Mungu wangu, Dany huyu msichana amekufanya vibaya, inabidi upate huduma ya dokta”
“Hapana nipo poa”
“Dany kwa hali hii kila unapo guswa mwili unakuuma unasema kwamba upo sawa”
“Livna ninakuomba unielewe nipo sawa, ninakuomba ukaniletee hizo nguo”
“Sawa baba”
Livna akatoka bafuni humu, baada ya dakika tano akarudi akiwa ameshika nguo nyingine zinazo fanana na nguo hizi, nilizo zivaa.
 
“Wasichana wapo tayari wanakusubiria katika chumba cha mawasiliano”
“Ninakuja”
“Sawa”
Livna akatoka humu ndani, nikaanza kuoga taratibu kutokana na maumivu makali ya mwili wangu. Nikavaa nguo hizi safi na kutoka humu chumbani huku nikiendelea kuyavumilia maumivu yaliyopo humu chumbani. Nikaingia ndani ya chumba cha mawasiliano na kuwakuta wasichana wanne wakiwa wamesimama wakinisubiria mimi. Ester na Logate wakaonekana wakinishangaa.
“Vipi mkuu umepata ajali?”
Logate alizungumza huku akitabasamu.
“Jamani si umetoka humu ndani mzima?”
Ester naye alizungumza akiwa amejawa namshangao. Sikujibu chochote zaidi ya kukaa kwenye kiti changu. Sikuweza hata kuegemea kwani mgongo mzima unaniuma.
 
“Kuna jipya gani?”
“Hakuna jipya hapa kitu kikubwa ni kuhakikisha kwamba tunampata Yemi”
“Mumewapa maelezo japo kidogo?”
“Hapana”
“Livna wape maelezo”
Livna akaanza kuwapatia maelezo wasichana wake hawa. Maelezo yakaenda sawa kama ninavyo hitaji.
“Mutaweza kuifanya hiyo kazi”
“Ndio mkuu”
“Itawachukau muda gani?”
“Masaa kumi, kwa maana si Tanzania”
 
“Ndio”
“Masaa kumi yatatosha sisi kuweza kuifanya hiyo kazi kikamilifu”
“Niwatakie kazi  njema”
“Sawa”
Wasichana hawa wakatoka hapa humu ofisini na kuelekea kujiandaa.
“Osama anapiga video call je tuwasiliane naye?”
Ester alizungumza huku akinitazama usonimwangu.
“Mpokelee”
Livna akanisaidia kuiwasha video. Nikamuona Osama akiwa amecaa mavazi niliyo muona nayo masaa machache alipokuwa anaonana na Livna. Nikavaa earphone sikionim wangu huku nikimtazama Osma kwa macho ya kumdadisi huku nikiwa nina hamu ya kusikia ni nini atazungumza kwangu kwani tayari ninamuhesabu ni msaliti kwangu.
 
“Habari yako Dany”
“Salama, umefanikisha kupatikana kwa Yemi?”
“Bado vijana wangu wanaendelea kuifanya oparesheni ya kuwatafuta”
“Uliniambia masaa kumi, na sasa ni masaa zaidi ya kuni na tano kama sijakosea”
“Ndio, ila ninaendelea kujitahidi kumtafuta. Ila unaweza kukutana nami baada ya kupambazuka”
“Unahisi kwamba mimi ni mpumbavu. Nilikusaidia Wamarekani wasikuue kwa mara ya pili, sasa sijajua ni kwa nini umeamua kuungana nao tena umeungana na mtu ambaye nilikuagiza ukamkombea mke wangu ila umekwenda kushirikiana nao.”
 
Osma akabaki macho yamemtoka na jinsi ndevu zake zilivyo nyingi na uzee ulio mtawala akazidi kunifanya nimuone kituko hadi nikatamani kucheka.
“Mimi na wewe sasa sio marafiki, ninakuomba ukae mbali na mimi. Usiingie kwenye kumi na nane zangu, kwa maana nitakupiga zaidi ya Marekani alivyo kupiga umenielewa mzee, kama muda wako ulisha kwisha katika kuwa mbabe wa dunia tulizana na kundi lako”
 
“Siawa kutishwa maisha mwangu, na wewe unajaribu kunitisha unajiamini nini kijana mdogo ambaye hata maziwa ya mama hayajaisha kukunuka mwilini mwako?”
‘Mungu wangu wazee wengine hawa wanatokea wapi wanapi mbona wanatafuta bifu za kijinga hivi?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku  nikimtazama mzee huyu. Nikamgeukia Ester ambaye anajua nini cha kufanya kwa watu wabishi kama hawa ambao wameshoboka na ngoma waliyo ikutia katikati na wanataka kuicheza pasipo kufahamu ngoma hiyo ni ya kabila gani.
 
AISIIIII……….U KILL ME 187 
 
“Unamfahamu mama yangu mzee?”
“Sina haja ya kumfahamu mama yako”
“Sasa utamfahamu kilazima”
Nilizumgumza kwa msisitizo kisha nikaizima Tb hiii, nikamge Ester anaye subiria amri yangu.
 
“Tumshambulie?”   
“Hapana, yupo wapi?”
“Yupo bado Dar es Salaam”
“Ninahitaji kwenda kumakamata mimi mwenyewe”
“Dany huwezi kufanya hivyo hali yako haipo sawa”
“Niitie daktari”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikimtazama Livna.
“Dany huwezi kwenda kumkamata Osama, ni mtu hatari ana jeshi kubwa na amesha ungana na K2 pamoja na Marekani, kwa nini unahitaji kujitoa sadaki ikiwa bado lengo halijamilika?”
 
Livna eliendelea kuzungumza huku akinibembeleza niitengue maamuzi yangu niliyo yaamua. Kwa macho makali niliyo mtazama Livna akajikuta akitulia, akanyanyua mkonga wa simu ya mezani na kumpigia daktari na kumuagiza aweze kufika katika chumba hichi haraka iwezekanavyo. Hazikupita hata dakika tano daktari akaingia huku akiwa na kibegi kidogo. Nikapandisha tisheti yangu juu kidogo na kuwafanya watu kuona alama za mateke na ngumi nilizo pigwa mwalini mwangu.
“Oooohooo my God, ni nini kimekupata?”
Daktari alizungumza huku akinifwata nilipo kaa. Akaanza kunichunguza mwili mzima huku a kionekana kuzidi kushangaa hizi alama.
“Nichome sindano ya kutoa maumivu mwilini”
“Ila inabidi tukufanyie chake up ya ndani, kama nje kuna alama kama hizi basi ujue ndani ni lazima kutakkuwa na tatizo kubwa”
“Nimekuambia nichome sindano ya kuzuia maumivu”
“Sawa sawa”
 
Daktari alizungumza huku akimtazama Livna usoni mwake, kwa haraka akafungua kibegi chake, akatoa kichupa kidgo pamoja na bomba la sindano.  Akafunga sindano na kuifunga kwenye bomba hilo kisha akaichomeka kwenye mfuniko wa kichupa hichi ambao umetengenezwa na mpira mlaini. Akavuta kiasi cha dawa, kisha akaniomba ninyooshe mkono wangu wa kushoto huku nikiwa nimekunja ngumi.
Hakuwa na haja ya kunifunga kitu chochote kwani mishipa inaonekana vizuri. Akanichoma sindano hii na kuisukuma dawa taratibu hadi ikaisha ndani ya bomba hili.
“Munaweza kutengenza sura bandia?”
Swali langu likamfanya daktari  kumtazama Livna, aliye kaa kimya kwa muda huku  akionekana kujawa na wasiwasi mweingi sana.
 
“Ndio”
Livna alinijibu kwa unyonge sana.
“Ninahitaji kufanyiwa hiyo oparesheni sasa hivi”
“Dany mpenzi wangu ninakuomba usifanye hivyo”
Livna alishindwa kuzuia hisia zake mbele ya wasichana wake anao waongoza ambao nina imani kwamba hawajawahi kufahamu upendo ni kitu gani.
“Kuna kitu muhimu sana ninahitaji kukifanya juu ya dunia. Tafadhali Livna ninakuomba unielewe, ninakuomba uridhike juu ya hilo sawa mama”
Nilizungumza huku nikiwa nimesimama mbele ya Livna. Ukimya ukatawala ndani ya chumba hichi huku sote tukisubiria jibu la Livna.
 
“Tafadhali ninakuomba ukubali, Osama ndio atakuwa ufunguo wa kila kitu kilicho fungwa kwangu”
“Una maana gani?”
“Nikubalie kisha utaweza kufahami ni kitu gani nina maanisha”
Livna akashusha pumzi nyingi, akamtazama daktari ambaye naye anasubiria jibu.
“Mtengeneezeeni sura ya bandia”
“Nahitaji kufanyiwa oparesheni kabisa ya sura ya bandia, itachukua muda gani dokta?”
“Ahaa…. Itachukua  masaa kama sita hivi au saba”
“Niandalieni”
 
“Je unahitaji sura gani?”
“Nichagulie”
“Sasa Dany mimi nitajua ni sura gani itakufaa jamani”
“Dokta hakikisha unanitengeneezea sura ambayo sio rahisi mtu kuweza kunigundua hata ikitokea wanajaribu ku scan kwenye mtandao wasiweze kuiona siura yangu halisi. Sijui umenielewa?”
“NImekuelewa nimekuelewa vizuri sana. Itanichukua kama dakika ishirini kuunda sura kama hiyo”
“Sawa fanya hivyo”
“Sawa”
Daktari akafunga kibegi chake na kutoka chumbani humu.
“Ester hakikisheni kwamba Osama hapoteni kwenye mitandao  yenu, hakikisheni munamfwatilia kila anapo elekea, kama atapiga simu yoyote ninaomba mazungumzo yake muweze kuyarekodi”
 
“Sawa mkuu”
Nikatoka chumbani humu huku Livna akainifwata kwa nyuma.
“Dany sipendi maamuzi ya kwako peke yako?”
“Kama yapi?”
“Kwa nini unaamua kwenda kupambana na Osama ikiwa unajua unatafutwa kila kona ya dunia”
“Livna umejitolea sana juu yangu, umewatoa watu wako wengi na woye wananipigania mimi. So nilazima na mimi niweze kufanya jambo, si kukaa mule ofisini na kutazama mambo jinsi yanavyo fanywa kwenye Tv, sasa unapo nipeleka ni kuwa gaidi boksi. Nahitaji kufanya kitu katika hili, nanitaji kuionyesha dunia kwamba ninauwezo wa kudanya jambo”
Nilizungumza kwa msisitizo huku nikiendelea kumtazama Livna usoni mwake.
“Nahitaji kwenda kuzungumza na Hawa”
“Sawa”
 
Nikamuacha Livna akiwa amesimama kwenye hii kordo huku akinitaazama. Nikaingia kwenye chumba anacho kaa Hawa, nikamkuta akiwa amelala kitanda kimoja na Livna huku wamekumbatia. Nikafunua shuka lililo wafunika na kuwakuta wote wapo uchi. Nikawatazama kwa muda jinsi maumbo yao yalivyo, nikaushusha mkono wangu karibu na alipo Hawa, ila nikasita, taratibu nikawafunika kama nilivyo wakuta na nikatoka humu ndani.
“Mbona umewahi kutoka?”
“Wamelala”
“Ila muda umekwenda kwa kweli”
“Ndio, ninahitaji hii oparesheni niifanye na msichana mmoja”
“Nitakwenda na wewe?”
“Ni hatari hatuwezi kwenda sisi wawili, ni juzi tu umetoka kwenye hatari na tumempoteza Martin, sihitaji uende kwenye matatizo hembu angalia kwanza afya yako itakavyo kwenda”
“Afya yangu ipo poa mbona”
 
“Simaanishi afya ya mwili, hapa”
Nikamshika tumbo Livna na kumfanya atulie kwa muda, akatabasamu nikatambua amenielewa.
“Niwakati wa kumuangalia mwanangu, na mama utakaa ndani na mimi baba ninakwenda kuifanya kazi hii sawa”
“Sawa mume wangu”
Livna akanibusu kwenye lipsi zangu. Tukaelekea katika chumba cha oparesheni na kuwakuta madaktari wanne wakike wakiwa tayari wamesha fanya maandalizi ya kufanya opareshi hii ya kuniweka sura ya bandia.
“Mkuu inabidi kukuchoma sindano ya usingizi kwa maana hii kazi haitaji usumbufu”
“Hakuna tabu, nipo tayari”
“Ngoja kwanza nimbusu mume wangu”
Livna alizungumza kwa furaha, akanikumbatia kwa muda kisha tukanyonyana midomo yetu kwa muda kidogo kisha tukaachiana.
“Ninakupenda sana Dany”
“Ninakupenda pia”
Nikamuachia Livna kisha nikaka kitandani, taratibu nikalala, daktari akanichoma sindano ambayo hata dakika mbili hazikuisha nikajikuta nikilala fofofo.
                                                                                                       ***
Nikayafumbua macho yangu taratibu, nikamuona Livna akiwa amekaa pembeni ya kitanda huku  anasinzia sinzia.
“Hei”
Nilimuita huku nikijitahidi kukaa kitako.
“Mume wangu umeamka”
‘Yaaa, niambie”
“Safi, umependaza, hembu jitazame kwenye kioo”
Nikashuka kitandani taratibu, nikajinyoosha viungo vyangu huku nikipiga miyayo mingi. Nikaanza kutembea kwa hatua za kivivu hadi kwenye kioo. Sikuamini muonekano ninao onekana kwa maana ninaonekana tofauti sana, sura waliyo niweka inanifanya nizidi kuonekana mzuri.
 
“Hapo hakuna mtu ambaye anaweza kukugundua hata iweje”
“Kweli?”
“Ndio yaani hapo hata mimi mwenyewe nikikutana na wewe barabarani na nikiwa sifahamu kama umebadilishwa sura basi sinto weza kukufahamu”
“Duuuu, sasa mauaji yote yaliyo baki mke wangu ninakwenda kuyafanya mimi mwenyewe”
“Ahahaaa, wewe unakwenda kumuua Osama, ninakuomba hii sura ya sasa hivi usiichafu, usiwape watu wazo kwamba unaweza kutumia sura ya bandia”
 
“Sawa nimekuelewa mpenzi”
“Hakikisha kwamba kazi unaifanya kisha unarudi hapa salama”
“Ninahitaji kurudi na Osama ndio maana ninameomba msaada wa kupata msichana mmoja ambaye anaweza kushirikiana nami”
“Sawa, nitakuchagulia msichana mmoja katu ya wale kule chini”
“Sawa. Hivi sasa ni saa ngapi?”
“Ni saa moja kasoro”
“Asubuhi?”
“Ndio”
“Poa, nahitaji suti nyeusi, bastola mbili, magazine kumi na mbili”
“Bastola mbili zinatosha kweli?”
“Ndio zinatosha, kikubwa ni kuhakikisha kwamba ninashabaha nzuri”
“Sawa mume wangu, ninakuandalia wewe. Pia kuna zawadi moja ninahitaji kukupatia”
 
“Zawadi gani?”
“Mmmmmm zawadi haisemwi hadi utakapo iona”
“Sawa”
Tukatoka katika chumba hichi na nikaelekea chumbani kwangu na kumuacha Livna akielekea sehemu ambayo anaweza kupata vitu ambavyo nimemuagiza. Nikavua nguo zangu na kuingia bafuni, nikaanza kuoga huku nikiwa na shauku kubwa ya kwenda kuifanya hii kazi iliyopo mbele yangu.
“Ni lazima nimfundishe kazi huyu mzee”
Nilizungumza huku nikizidi kuoga kwa furaha kubwa kana kwamba ninaelekea katika sherehe fulani hivi ambayo mimi ndio mgeni mualikwa, nikaanza kucheza huku nikijitazama kwenye kioo cha humu bafuni kwanini nimebadilika sana. Mlango wa bafuni ukafunguliwa, na nikamuona Livna akiwa anashangaa.
 
“Unashangaa nini?”
“Nashangaa jinsi unavyo cheza, unafuraha kubwa eheee?”
“Yaa nina furaha, yaani takacho mfanya Osama, lazima akafurahi na roho yake”
“Hahaaaaa haya mwanya”
Livna naye akavua nguo zake na kubaki kama alivyo zaliwa, akanisogelea huku akinitazama usoni mwangu. Akanikumbatia kwa nguvu.
“Dany unanipa raha sana, unanifanya nionekane mtu kati ya watu. Unajua muda mwengine nyge zinaweza kumfanya mtu afaye vitu vya ajabu ajabu, unalitambua hilo?”
“Yaa ninalitambua”

“Hujisikii  maumivu huku ulipo pigwa?”
“Hapana ile sindano imenisaidia”
 
 Livna kaanyanyua koti la suti na kunionyesha tisheti moja nyeusi ambayo kwa haraka haraka nikaikumbuka. Tisheti kama hii nilisha wahi kukabidhiwa na mama yangu kipindi cha ujana wake, sifa yake ni moja, ni kwamba haiingii risasi.
“Umeipata wapi hiyo tisheti?”
“Hii tisheti alinikabidhi baba yako kipindi cha nyuma, aliniambia sifa yake ni kwamba haiingii risasi na ni kweli niliweza kuifanyia majaribio mengi sana na kweli haiingi risasi”
 
“Marehemu mama ndio alikuwa anazitengeneza hizo tisheti”
“Ni kweli hata baba yako aliniambia kwamba mke wake ndio alimtengenezea hizi tisheti. Sasa leo ninakukabidhi wewe, nina imani kwamba itakusaidia sana”
“Shukrani mpenzi wangu”
Nikabusu Livna mdomoni mwake, nikaichukau tisheti hii na kuivaa, na kunibana vizuri mwilini mwangu. Nikachukua shati jeupe na kuvaa, kisha nikafwatia, bosa pamona na suruali na nikamalizia koti. Livna akanivisha mkanda wa suruali vizuri. Akachuchumaa na kunivisha soksi kila mguu pamoja na viatu vizuri.
 
“Hapo unaonekana ni bonge moja la bilionea”
“Wapi”
“Kweli mume wangu na hiyo sura, ninapata mashaka wanawake jinsi watakavyokuwa wanakushobokea”
“Yaaa, ila ninakwenda kikazi na ninahitaji kurudi hapa nikiwa na kichwa cha Osama Bin Laden”
“Usirudi na kichwa chake, ninahitaji urudi naye hapa akiwa hai, nahitaji na mimi niweze kumuona”
“Etiee eheee?”
“Ndio”
Livna akanikabidhi bastola mbili, nikaanza kuikagua moja baada ya nyingine na kuzikuta zikiwa salama, akanikabidhi magazine za bastola hizi ambazo nikaanza kuzichomeka kila moja sehemua mbayo ninaona itakuwa ni rahisi kwangu pale nitakapo amua kuichomoa.
 
“Hii ni saa ambayo popote utakapo kwenda huku tutaweza kukuona, hakikisha kwamba unaitunza mume wangu, endapo itapotea utaniweka mimi katika wakati mgumu sawa mume wangu”
“Usijali mke wangu”
Livna akavaa nguo zake, tukatoka ndani humu na kwenda moja kwa moja katika chumba cha mawasiliano, Ester na Logate wakabaki wakiwa wananishangaa kwani nimebadilika sana.
“Mupo poa?”
Niliwasalimia, hapakuwa na aliye weza kuitikia salamu yangu kwa mshangao ambao bado unaendelea kuwatesa.
 
“Wanakushangaa wamekupenda”
Akaingia msichana mrefu, mweupe amevalia gauni jeusi lenye mpasuo mkubwa hadi karibi kabisa na kiuno chake, paja lote la mguu wa kulia lipo wazi. Nywele zake ni ndefu zinaning’inia mgongoni mwake na baadhi zimeficha jicho lake la kushoto kidogo. Umbo lake ni namba nane yenyewe, kwani ana hispi ambazo kusema kweli zinanitamanisha.
“Dany huyu anaiwa Magreti, ndio utakuwa naye kwenye kazi unayo kwenda kuifanya ya kumkamata Osama Bin Laden”
‘Mmmmm kweli lazi itafanyika hapa?’
Nilizungumza kimoyo moyo huku nikiendelea kumtazama binti huyu aliye jaribu kunipa mkono wake wa kulia ila nikabaki nikimazama kwani ni mzuri kupindukia hata Livna mwenyewe hamfikii msicha huyu hata nusu yake.
 
 ITAENDELEA
‘Hay sasa Dany anaingia kibaruani yeye mwenyewe huku sura yake ikiwa imebalishwa na anahakikishiwa kwamba hakuna anaye weza kuigundua je atafanikiwa kwenye kazi yake anayo kwenda kuifanya? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )