Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 17, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 194 na 195 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA      
     
“Baba yako yupi?”
Nilizungumza huku nikimdadisi sana huyu msichana.
“Wewe”
“Mimi?”
“Ndio, wewe ni baba yangu. Mama yangu ni OLVIA HITLER”
Nikapatwa na kigugumizi nikashindwa kabisa kumjibu msichana huyu ambaye ninakumbuka nilizaa na mama yake ambaye ni jini miaka mingi ya nyuma na alisha wahi kuniahidi kwamba ipo siku mwanangu ninaye mpatia atakuja kunisaidia na hichi ndicho kilicho tokea kwa siku ya leo, ahadi ambayo hata akilini mwangu sikuwahi  kuifikiria kwamba inaweza kuja kutokea ila leo imetimia.
   
ENDELEA
“Naamini kwamba utakuwa unashangaa kuniona kwenye hali kama hii ila nina imani kwamba umenikumbuka”
“Yaa, nimekumbuka”
“Nimekuja kukusaidia, kwenye kila jambo linalokusumbua kwenye maisha yako”
Moyoni mwangu wala sina kipingamizi cha aina yoyote kwani maneno ya msichana huyu yamenifanya kumuamini kwa asilimia mia moja, kwani siri ya kuzaa na Olvia Hitler, nilikuwa nayo mimi mwenyewe na nimeishi nayo kwa miaka sana na sikuwahi kumuambia mtu wa aina yoyote.
 
“Njoo hapa”
Nilizungumza huku nikimuita mwanangu taratibu nikamkumbatia kwa nguvu sana huku machozi yakinilenga lenga, kwani kwenye maisha yangu nimebahatika kupata mtoto mmoja tu ambaye alisha uwawa na wengine wapo kwenye matumbo ya mama zao, ila huyu nimekutana naye.
Magreti akashuka kwenye gari huku akionekana kutushangaa sana jinsi tulivyo kumbatiana.
“Kuanzia leo  utaitwa Jojo”
“Asante baba kwa jina lako, nimelipokea kwa moyo mmoja”
“Mama yako anaendeleaje?”
Jojo taratibu akaniachia, usoni mwake amejawa na machozi mengi.
 
“Niambie mama yako amefanyaje?”
“Muda wake wa kuja ulimwenguni umekwisha na sasa yupo tu chini ya bahari”
“Ina maana hato kuja tena duniani?”
“Ndio, safari yake ya mwisho kuja duniani ni siku ambayo mulikutana, na alinihitaji unipate mimi ili niendele kuzifanya kazi zake alizo ziacha huku duniani”
Jojo alizungumza kwa sauti ya upole kidogo huku akinitazama usoni mwangu.
“Dany”
Magreti aliniita na kunifanya nigeuke na kumtazama usoni mwake.
“Mumejuana juana vipi na huyo msichana?”
“Huyu ni mwanangu anaitw Jojo”
 
“JOJOOOOOOO….!!!”
“Yaaa”
“Danu una mtoto mkubwa kiasi hicho?”
“Ndio”
“Jojo anaitwa Magreti”
“Ninamfahamu”
“Unanifahamu?”
“Yaa tangu ukiwa mdogo ninakufahamu”
“Mmmmmm”
“Yaa, tuondokeni hii sehemu sio salama Wamarekani wanakuja”
Kutokana nina ujua uwezo wa mwanangu Jojo, sikuwa na kipingamizi wala ubishi kwa haraka tukarudi kwenye gari, tukaingia ndani na kuondoka eneo  hili.
“Wewe umesema kwamba unanijua mimi kutoka nikiwa mdogo?”
 
“Siitwi wewe, baba yangu amenipatia jina la Jojo, niite Jojo Dany”
“Sawa Jojo Dany, umenijuaje wewe na huku porini ulikuwa unafanyaje?”
“Na nyinyi huku porini mulikuwa munafanyaje?”
Jojo  alizungumz ahuku akimgeukia Magreti aliye kaa siti ya nyuma pamoja na Osama Bin Laden.
“Kuna kazi maalumu ilikuwa imetuleta huku”
“Hata mimi kuna kazi maalumu ilinileta huku.”
“Kazi gani?”
“Magreti huwa sipendelei maswali mengi kutoka kwa mtu ambaye hanihusu, anaye nihusu hapa ni baba yangu tu”
Nikamtazama Jojo kwa jicho la kuiba huku nikiendelea kuendesha gari hili kwa mwendo wa kasi.
 
“Kunja kilia”
Jojo alizungumza.
“Kuna kulia Wanajeshi wapo mbele hapo?”
Nikafanya alicho nieleza Jojo, nikaingia kulia, ambapo kuna kichaka kikubwa. Kwa ishara Jojoakaniomba nisimamishe gari, hazikupita hata dakika mbili gari zipatazo nane za Wamaerekani zikaanza kupita kwa kasi kuelekea sehemu tulipo toka.
“Tunaweza kwenda sasa”
Nikarudisha gari nyuma taratibu, na kuondoka eneo hili kwa kasi sana.
“Baba sitisa mpango wa kurudi kwenye meli unayo ishi, nahitaji tuimalize hii kazi iliyopo mbele yetu”
“Ila mwanangu nina imani kwamba tutakuwa tunatafutwa?”
“Yaaa wanatutafuta na sura zenu tayari wamezinasa kwenye satelaiti”
“Jojo ninakutegema sasa mwanangu, kwa maana sijui nini cha kufanya”
 
“Upo nami, baba hilo usijali”
“Hivi munajua munacho kizungumza mimi siwaelewei nyinyi, kwa maana Dany usalama wetu ni kurudi kwenye meli”
“Mukirudi mutasababisha maafa makubwa kwa wengine kwa maana sasa hivi wamarekani wamegundua teknolojia mpya ya kuweza kuwatafuta watu wanao wahitaji popote pale waendapo hususani sura zao wakiwa tayari wamesha zihifadhi. Kwa sasa musipige simu wala musitume meseji popote ndio maana nimezifanya simu zenu kupoteza uwezo wa mawasiliano. Najua mutajisifu kwamba muna vifaa ambavyo vinaweza kufanya chochote duniani ila kwa hicho kimoja walicho kizindua jana wamewashinda”
 “Jojo kusema kweli sikuelewi, wewe ni nani kwani?”
“Mimi ni Jojo”
Magreti akabaki na swali la kishindwa kumelewa Jojo kabisa, ila mimi nina muelewa.
 
“Sasa hapa si lazima watakuwa wataufwatilia?”
“Ndio wanatufwatila ila wanashindwa”
“Wanashindwa kwa nini?”
Jojo akanisogela sikioni na kuninong’oneza.
“Nimewafunga uwezo wao wa kiakili  hawawezi kujua ni wapi tunapo elekea japo wanatuona tu kwenye mitandao yao”
“Mbona munanificha jamani minieleze kile kinacho endelea”
“Magreti usijali nitakuambia sehemu tutakayo fika ni kitu gani kitakacho endelea”
Jojo alizungumza huku akimtazama Magreti ambaye bado anaonekana kuto kuridhika kabisa na mazungumzo yyetu.
“Simama hapo”
 
Jojo alizungumza, nikasimamisha gari kwenye moja ya njia inayo ingia kushoto kwetu. Jojo akashuka kwenye gari na kutufanya mimi nami nishuke kwenye gari.
“Kuna kitu gani kinacho endelea”
“Hapo mbele kuna ukaguzi mkubwa sana wa wanajeshi”
“Tutapita wapi?”
“Hakuna njia ya pekee zaidi ya kwenda kuwaua, kwa maana ni hapo chini ukimaliza hiyo kona hapo mbele”
“Ni nini kinacho endelea”
Magreti alizungumza kwa sauti ya juu huku akinifwata sehemu tulipo simama na Jojo.
“Kuna rod block hapo mbele na wapo wanajeshi wengi”
“Mmmmmm sasa itakuwaje?”
“Tunakwenda kuwaua”
Jojo alizungumza kwa kujiamini sana.
“Chukua silaha” 
   
Magreti alizungumza huku akimkabidhi jiji bunduki.
“Huwas itumiagi silaha samahani”
“Dany huyu mwano vipi?”
“Mlinde Osama tunakuja”
Jojo akaanza kupandisha kwenye njia hii iliyopo pembezoni mwa barabara huku akikimbia, nikaanza kumfwata kwa nyuma huku nami nikiwa nimeshika bastola yangu. Tukafika juu ya kilima kilichopo pembezoni mwa hii barabara, tukasogelea karibu kabisa na ukingo wa barabara na tukawaona wanajeshi wengi wa Kimarekani wakiwa wamesimamisha magari wakiendesha ukaguzi mkali sana.
“Wapo ishirini na nane, chukua watatu walio baki mimi nitadili nao”
 
Jojo baada ya kuzungunza maneno yaho akaruka na nikabaki nikimtazama, akatua katikati ya wanajeshi wanne, kwa kasi ya ajabu ambayo hakuna binadamu anaweza kuienenda, akaanza kuwavunja vuja wanajeshi hao.
Wanajeshi wengine wakaananza kumshambulia kwa silaha, ila Jojo, akazidi kuwa mahiri na hatari kwao kwani mapigo yake hayakunishangaza mimi tu ila hata wanajeshi. Nikashusha pumzi nyingi na kuanza kufyatua risasi kwa wanajeshi watatu nilio ambiwa niwaue. Ndani ya dakika kadhaa wanajeshi wote wamalala chini na wamekufa. Jojo akaninyooshea kidole gumba ikiwa ni ishara kwamba amefanikisha kazi.
 
“Ruka”
“Eheee?”
“Shuka?”
Nikatazama umbali ambao Jojo aliruka, kwa binadamu wa kawaida, nilazima utajifikiria mara mbili mbili hata kama ni hodari kiasi gani.
“Ruka tu baba”
Nikarudi nyuma hatua mbili kisha nikajitosa hewani, nikafanikiwa kutua chini salama pasipo kupata tatizo lolote. Watu ambao wapo kwenye magari yao, ni muda mrefu wamatoka na kukimbia baada ya kuona mashambulizi tuliyo yafanya.
 
“Hizi maiti inabidi tuzitoe hapa?”
“Si itatuchukua muda?”
“Hapana, dakika chache”
Jojo akaanza kubeba maiti moja baada ya nyingine na kuitupia pembeni ya barabara. Tukasaidia kwa haraka haraka kuzitoa hizi maiti kisha tukarudi kwenye eneo ambalo tulipo muacha Osama na Magreti.
 
“Mumefanikiwa?”
Magreti alizungumza mara baada ya kutuona tumeingia ndani ya gari.
“Ndio tuondokeni eneo hili”
Jojo alijibu na kuondoka eneo hili na kuendelea na safari. Tukafika katika nyumba ambayo Jojo alihitaji tuweze kufikia. Ni nyumba iliyo jengwa vizuri sana, ina gorofa mbili juu na vitu vyake humu ndani ni vya thamani sana.
“Karibuni hapa ni kwangu”
“Kwako?”
Magreti alizungumza huku akishangaa sana.
“Ndio kwangu, au ulihisi kwmba sina kwangu”
“Hapana ila ninashangaa kukuona binti mzuri una maisha mazuri kama haya”
“Hahaaaa hizi ni pesa za bibi yangu.”
Jojo alizungumza huku akinitazma usonini mwangu. Nikatamani kumuuliza juu ya bibi yake ila nikajikuta nikikaa kimya.
 
“Huyu Osama wenu munatembea naye wa nini, kwa maana hana msaada wowote kwenu”
“Huyo atatukutanisha na K2?”
“Atawakutanisha na K2 kivipi ikwa wamarekani wanamhitaji?”
“Wanamuhitaji kumua, ila si kumlinda. Tukiendelea kukaa naye hapa atatuletea matatizo”
“Ninahitaji kumuua kwa mkono wangu”
“Ila Dany hayo sio makubaliano?”
“Hata yeye alitugeuka, nahitaji kumrusha kwenye vyombo vya habari jinsi ninavyo muua”
“Ila si kwa sura hiyo baba yangu”
“Hii kwani vipi?”
 
“Ukiwa katika sura yako  halisi utazidi kupendeza”
“Kweli?”
“Ndio  baba, ngoja niandae mazingira ya wewe kumuua”
Jojo akaondoka hapa sebleni na kutuacha mimi, Magreti na Osama ambaye hakielewi Kiswahili kabisa.
“Dany hivi huyu ni mwanao wa aina gani mwenye roho kama yako”
“Like father, like a daughter”
Jojo akarudi hapa sebleni, akatuambai kwamba tayari amesha andaa mazingira, tukaongozana naye hadi gorofa ya kwanza tukaingia kwenye moja ya chumba, tukakuta kamera mbili zikiwa zimesimishwa vizuri, kiti kimoja pamoja na meza yenye laptop juu yake.
 
“Baba utakwenda hewani moja kwa moja, chaneli zote duniani zitaweza kuona kile kitu unacho kifanya”
“Hilo ninaona kama si wazo zuri?”
Magreti alizungumza huku akitutazama.
“Ni wazo zuri, kwa maana ni lazima baba yangu azidi kuwa maarufu”
“Maarufu kwa kumuua Osama?”
“Ndio kw akumuua Osama, kwani hata Marekani si walipata umaarufu kwa kumuua Osama”
“Dany hili sio wazo zuri sioni sababu ya kumua huyo Osama ikiwa mpango wa wazo nililo kupatia haujalamilika?”
“Nyote mulishindwa kwa kuweka hisia za mapenzi mbele, muliona njia ya kujiburudisha kwa ngono ndio itawapa muda wa kupumzika zivuri ikiwa kuna wezenu walijipanga kuja kuvamia hapo. Laiti ingekuwa sipo unahisi wewe na baba yangu mungekuwa wapi?”
 
Jojo alizungumza kwa ukali ambao si wakawaida, macho yake yakabadilika rangi, na kuwa kijani huku mboni yake ikibadilika kutoka rangi nyusi na kuwa nyekundu. Magreti baada ya kuona hali hii mwili mzima ukaanza kumtetemeka. 

Jojo akaanza kumfwata Magreti huku kucha zake zikianza kukua mikononi mwake, jambo ambalo hata mimi mwenyewe linaniogepesha kwani kuwa na mtoto wa aina kama hii inataka ujasiri na uvumilivu mkubwa sana.
 
AISIIIII……….U KILL ME 195

Nikataka kuzungumza kitu ila mdomo wangu ukashindwa kufunguka kabisa, Jojo kwa haraka akamkandamiza Magreti ukutani huku mkono wake mmoja ukiwa ameugandamiza kifuani mwake.
“Hivi ndivyo nilivyo sawa?”
Jojo alizungumza kwa ukali sana na kumfanya Magreti kutingisha kichwa chake, Jojo akamuachia Magreti, akarudi kwenye hali yake ya kawaida huku akinitazama na kutabasamu, akanikonyeza. Nikagundua yote aliyo yafanya ilikuwa ni njia moja ya kujidhihirisha mbele ya Magreti na hata kwangu kwamba yeye ni mtu wa aina gani.
“Baba unaweza kuendelea na utaratibu”   
“Inabidi  sasa niivue hii sura”
“Sawa”
Nikaanza kujibabadua sura hii ya bandia, japo ninapata maumivu makali ila nikazidi kujitaidi kukitoa sura hii hadi nikafanikiwa.
 
“Pole baba yangu”
“Asante mwanangu”
“Sasa tunarusha matangazo haya moja kwa moja hewani. Nimesha weka post muda fulani kwamba kuanzia muda wowote gaidi Dany atakwenda hewani na ana ujumbe maalumu kwa watu wote duniani”
“Sawa mwanangu”
Nikaichomoa bastola yangu moja na kusimama nyuma ya kiti  tulicho mkalisha Osama Bin Laden.
 
“Nahesabu moja hadi tatu, utaaza kuzungumza au kumuua yote ni sawa”
“Poa poa”
“Magreti simama kamera ile pale, usiniogope bwana nilikuwa ninakutania”
Jojo alizungumza kwa sauti iliyo jaa furaha, Magreti akamtazama Jojo kwa macho ya woga, taratibu Magreti akaisogelea kamera hiyo. Kwa ishara ya vidole, Jojo akaanza kuhesabu moja hadi tatu.
 
“Habari za muda huu, dunia nzima nina imani kwamba inashangaa kwa kile ambacho munakiona mbele yenu. Miaka mingi nyuma nchi ya Marekani ilitangaza ulimwenguni kwamba wamemuua gaidi anayejulikana kwa jina la Osama Bin Laden. Dunia iliweza kukubaliana na hilo, japo kuna baadhi ya watu waliweza kupinga kwamba hawajamuu Osama.”
“Ni kweli Osama Bin Laden hajafa na ninataka kuwadhihirishia dunia kwamba mimi ndio nitamuua Osama Bin Laden mbele yenu.”
 
“Sababu ya kumuu Osama Bin Laden, moja ni kutoka ameungana na nchi ya Marekani, pamoja na Tan katika kuhakikisha kwamba wanayaelekeza mashambulizi kwangu. Kutokana msaliti kwangu nilazima afe, basi mutashuhudia kifo chake mbele yenu”
Nikaikoki bunduki yangu, Osama akaanza kuzungumza maneno ya kiarabu akiashiria kwamba anamuomba Mungu wake sala ya mwisho. Jojo akanitazama na kunikonyeza kwamba nimuue, nikaielekezea bastola yangu kichwani mwa Osma Bin Laden, nikamtazama Magreti kisha nikampiga risasi mbizi ambazo zote zimeingia  kichwani mwake.
 
“Huyu aliiingia kwenye mfumo wangu wa kulipiza kisasi kwa maadui zangu, K2 jiandae ndio unaye fwata kwenye hili”
Baada ya kumalizia kuzungumza meneno haya nikafyatua risasi kadhaa mwilini mwa Osama, hadi risasi zote zilizopo kwenye magazine zikaisha.
 
Nikaondoka katika eneo hili, na kusimama pembeni ya Jojo huku tukiutazama mwili wa Osama Bin Laden jinsi unavyo mwaga damu. Jojo akaichomoa kamera iliyopo kwenye stand, akaanza kumsogelea Osama huku akiwa ameishika. Magreti akanisogelea nilipo simama.
 
“Dany”
“Ndio
“Ninaomba nijitoe kwenye huu mpango, ninaogopa”
“Unaogopa nini?”
“Dany kuna vitu vingine sijawahi kukutana navyo maishani mwangu. Kwa mafano huyo mwano unahisi kweli ninaweza kukaa naye sehemu moja kwa maana sio mtu”
Magreti alizungumza kwa sauti ya chini sana ambayo sisi wawili hapa ndio tunaisikia.
 
“Mimi ni mtu usiniogope bwana”
Jojo alizungumza huku akianza kutufwata sehemu tulipo simama.
“Ametusikiaje?”
“Magreti ngoja nikutoe wasiwasi, mimi nina uwezo wa hata kuona mambo yajayo kwenye maisha yako na ninauwezo pia wa kuyabadilisha na yakawa kama vile nitakavyo”
“Ina maana wewe una uwezo kama Mungu?”
“Hahaaa, hapana, mimi sio Mungu, sio jini, sio binadamu wala sio malaika”
 
“Sasa hapo wewe ni nani?”
“Sijui, labada baba yangu ajibu swali hilo”
“Ni Jojo”
“Tuachane na mazungumzo hayo, sasa tunatakiwa kuelekea kwenye meli yenu”
“Ahaha, sasa wewe si umetuambia tukirudi kule itakuwa ni hatari sana?”
“Ndio ni hatari ila, kwa sasa sio hatari, kabla ya kurudi kumshuhulia K2, kuna sehemu ninahitaji kumpeleka baba yangu”
“Sehemu gani?”
“Hupaswi kujua, atafahamu baba yangu hiyo sehemu ambayo tunahitaji kwenda”
 
“Sawa”
“Jojo”
“Bee”
“Njoo tuzungumze”
Tukatoka katika chumba hichi na kumuacha Magreti ndani na maiti yake Osama.
“Sijaelewa ni sehemu gani ambayo unahitaji twende?”
“Ninahitaji twende ukaone ndugu upande wa mama.”
“Wapi?”
“Chini ya bahari?”
“Jojo kumbuka kwamba mimi ni binadamu na si jini, hembu niambie kitu cha kueleweka hapo”
“Usija baba yangu, muda wa kuondoka ni sasa hivi. Unaweza kuwasilana na Livna”
“Sawa”
Nikatoa simu yangu na kukuta mtandao upo sawa, nikampigia Livna simu, simu yake ikaita kwa muda kisha ikapokelewa.
 
“Dany mume wangu upo salama kweli”
“Yaa nipo salama, mpenzi wangu”
“Kwa nini umevua sura yako ya bandia, unajua kwamba ni hatari?
“Usijali mke wangu, ninakuja sasa hivi”
“Upo wapi kwani?”
“Nitakuambia nipo wapi, ila kuna kifaa ambacho Wamarekani wamekigundua jana, kifaa ambacho wanaweza kufwatilia sura ya mtu popote atakapo kwenda hembu zungumza na Logate waweze kuhakikisha kwamba wanalifwatilia hilo swala”
“Sawa, nifanya hivyo, ngoja niwaandalie meli ile kwenye fukwe”
 
“Sawa”
Nikakata samu na kurudi chumbani.
“Kila kitu kimekamilika na muda wa kuondoka sasa hivi”
“Sawa, Magreti anaonekana kuniogopa sikui kwa nini?”
“Najaribu kukuzoea Jojo ila ninashindwa”
“Utanizoea, ila ninawaomba iwe siri, hususani wewe Magreti huko tuendapo ninakuomba usimuambie mtu yoyote juu ta lile ambalo nimekuonyesha”
“Sawa nimekuelewa”
Tukatoka nje na kutaka kuingia kwenye gari tulilo kuja nalo ila Jojo akahitaji tuingie kwenye gari lake, tukafanya hivyo na yeye akawa ndio dereva. Safari ikaanza huku Jojo akiendesha kasi sana.
“Unajua kuna muda ninawachukia sana watu ambao walisababisha haya maisha”
 
“Maisha yapi?”
“Maisha waliyo kusababishia wewe baba yangu, wamekufanya uwe gaidi ikiwa wewe sio malengo yako kwenye maisha yako”
“Ni kweli mwanangu, ila nimekuwa hivyo acha iwe hivyo”
Simu yangu ikaanza kuita, nikaitoa kwenye mfuko wa suti simu yangu, nikakuta ni namba ya Livna ndio inayo nipigia.
“Ndio”
“Ni kweli tumeweza kukifwatilia, na Ester ameweza kuzuia utendaji wake wa kazi na sasa yeye ndio anakiongoza”
“Kazi nzuri shukrani sana”
“Mupo wapi?”
“Tunaitafuta Chalinze sasa hivi”
“Ok, ninaona ukaguzi barbarani ni mkubwa sana tutakuwa tunawafahamisha kila sehemu yenye road block”
 
“Sawa mpenzi”
Nikata simu huku nikimtazama Jojo, aliye nitazama kwa jicho la kuiba kisha akatabasamu.
“Baba nikuulize”
“Niulize tu”
“Kwa nini umetembea na wanawake wengi?”
Swali la Jojo likanifanya niyanyanyue macho yangu taratibu hadi kwenye kioo kidogo kilichopo mbele yangu na kumtazama Magreti kwa nyuma.
“Unaogopa kujibu kisa Magreti, usimfiche bwana. Magreti mimi baba yangu ni malaya, sasa kama unampenda jiandae kuumia tu”
Nikajikuta nikikausha kimya, hata kufungua kinywa changu ninashindwa.
“Yaani kama baba angekupata leo, wewe ungekuwa msichana wa mia moja”
“Mungu wangu”
Magreti alizungumza huku akinitazama vizuri kwa kunichukungulia usoni.
“Hivi Dany huna ukimwi kweli wewe?”
Swali la Magreti likazidi kuninyong’onyeza kiasi kwamba nikashindwa kujibu chochote na kuendelea kukaa kimya 
 
 ITAENDELEA
‘Haya sasa Dany ameumbuliwa na Jojo mwanye wa kumzaa? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )