Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 23, 2019

AISIIIII……….U KILL ME ( Sehemu ya 199 )

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA- 0657072588
ILIPOISHIA   
       
“Kama kitu gani?”   
“Risasi ni moja wapo ya kitu ambacho unaweza kukikwepa haraka iwezekanavyo. Baba sasa huu ndio wakati wa kwenda kumtoa K2 madarakani, tummalize yeye pamoja na maadui wengine wote ambao waliweza kukuletea tabu wewe sawa”
Maneno ya Jojo yakanifanya nitabasamu kwani kwa uwezo nilio nao sasa K2 na wajinga wezake watajuta kunifahamu na watajutia ni kwa nini waliweza kuniharibia maisha ikiwemo kuwaua ndugu zao ambao nimewashuhudia wakipata mateso makubwa kuzimu, mateso ambayo K2 na wezake nao pia wanastahili kuyapata kwani ni haki yao.

ENDELEA
“Nimekuelewa mwanangu, umeweza kufwatilia ni wapi K2 alipo?”
“Yupo Tannia na bado ni raisi, na kwa sasa ana amani kubwa sana akiamini kwamba kila kitu kimekwisha”
“Ninahitaji kumshuhulika haraka iwezekanavyo”
“Ila nilazima nikufundishe jinsi ya kuweza kutumia nguvu zako. Kazi itaanza kuanzia kesho asubuhi, leo unatakiwa kuweza kupata chakula cha kutosha”
Jojo alizungumza huku akiondoka eneo hili, nikamfwata kwa nyuma na tukarudi ndani. Jojo akanionyesha chumba ambacho kinatumia kama jiko.
“Baba unajua ipo siku Tannia itakuja kutoweshwa moja ya visiwa vyake?”
Jojo alizungumza huku akifungua friji kubwa lililopo katika eneo hili, nikaona vidungu viwili vilivyo jaa juisi.
“Kwa nini unazungumza hivyo?”
“Miaka mingi ijayo hilo tukio litatokea”
“Ni kisiwa gani?”
“Una uwezo wa kuona mambo ya mbali, jaribu kuwaza hicho kitu alafu utaniambia ni kisiwa gani kitapotea kweney ramani ya dunia”
“Nifikie kwa namna gani?”
“Fumba macho yako, kisha vuta hisia kali sana juu ya hilo swala”
Nikajaribu kufumba macho yangu, nikafikiria kitu alicho niambia Jojo, ila nikashindwa kabisa.
“Sioni chochote”
“Vuta hisia, juu ya hicho kitu kwa manaa ni mambo yajayo”
Nikajaribu kurudi tena nilicho kifanya awali ila sikuweza kabisa kuona kitu cha aina yoyote.
“Hakuna kitu”   
Jojo akatoa kidungu kimoja cha juisi, akamimina juisi kiasi kwenye glasi na kunikabidhi, nikapiga fumba moja la juisi hii ambayo kwa haraka nikajikuta nikitema yote.
“Jojo hii si damu?”
“Ndio baba, ni damu ya binadamu, kwa sasa una uwezo ambao itakupasa kwa kila kipindi fulani unywe damu ya binadamu mwenye nyota kama yako na hii itakufanya uweze kuishi miaka mingi na hoto zeeka wala kuwapoteza asilimia yoyote ya nguvu za mwili wako. Miaka yote utabaki kuwa binadamu”
Maneno ya Jojo yakanifanya nibaki nimemtole macho tu.
“Baba, kufanya hivyo itakusaidia kuweze kufikisha malengo ya kuifikisha Tanzaninia katika malengo makubwa duniani, unakumbuka kwamba uliambiwa kwamba ni lazima uifanye Tanzania kuwa taifa kubwa na hii ndio njia ya pekee ya kukufanikisha wewe”
Jojo alizidi kuzungumza kwa msisitizo mkubwa sana.
“Jojo ila kumbuka kwamba mimi ni binadamu na sina chembechembe yoyote ya ujini?”
“Hilo ninalielewa baba yangu, ila una nguvu kama zangu, ili kuweza kuziongoza nguvu hizo ni lazima uweze kuitumia hiyo damu. Unaniona mimi, ninazidi kuonekana mrembo na mdogo sana kwa sababu gani unajua?”
“Eheee?”
“Kwa sababu ya hiyo damu. Huwa damu hii unatakiwa kunywa kila baada ya miaka mitano”
“Mmmmm”
“Ndio nanimekitafutia hii damu kwa ajili yako baba yangu, kunywa ili uweze kuishi”
Nikashusha pumzi nyingu huku nikimtazama Jojo usoni mwake. Taratibu Jojo akaushika mkono wangu ulio shika glasi na kuanza kuipandisha taratibu mdomoni mwangu.
“Usiisikilizie baba, kunywa moja kwa moja sawa baba”
Sikujubu kitu gadi glasi inafika mdomoni mwangu, nikatamaini kuinywa ila nikaishusha glasi hii.
“Jojo siwezi kunywa hii?”
“Baba na ukiacha kunywa hii damu huwezi kuishi miaka mingi, pia na nguvu ambazo umekabidhiwa zote zitaondoka mwilini mwako na hutoweza kupambaba na maadui zako. Baba huu ni muda wa kuhakikisha kwamba unakuza jina la Hitler kwa mara nyingine duninai. Kumbuka kwamba unaitwa Dany Hitler, tafadhali baba”
Jojo alizungumza huku machozi yakimlenga lenga usoni mwake. Nikaitazama glasi yenye damu, nikayafumba macho yangu na kuanza kunywa mafumba mengi kwa mfululizo hadi juisi ikaisha.
“Safi, inabidi umalize hichi kidungu”
“Sasa hivi!!!?”
“Ndio baba”
“Ahahaa hembu acha kwanza”
Nilizungumza huku nikitoka humu jikoni, Jojo akanifwata kwa nyuma na sote kwa pamoja tukaka sebleni, Jojo akawasha tv.
“Baba”
“Mmmmm”
“Unampenda Magreti?”
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Nimekuuliza tu baba?”
“Yaa ninampenda”
“Basi leo inabidi twende tukamchukue”
“Wapi?”
“Kule kwneye ile meli ya Livna”
“Si unakumbuka siku tuliyo ondoka tuliacha matatizo gani?”
“Ninakumbuka ila kwa sasa usiogope kwa maana hawawezi kutuzuia”
“Sihitaji kumdhuru mtu”
“Hatuwezi kumdhuru mtu”
“Sawa tutaend……”
Kabla sijamaliza sentensi yangu tukaona taarifa ya habari inayo muhusu K2 jambo lililo tufanya kunyamaza kimya na kumsikiliza kitu anacho kizungumza na waandishi wa habari.
“Serikali yangu ikishirikiana na nchi ya Marekani tumweza kuangamiza ngome kubwa ya magaidi ambayo ilikuwa ni meli kubwa iliyokuwa katikati ya bahari”
Taarifa hii ikanifanya nikae vizuri kwenye sofa hili, na kukazia macho hii taarifa.
“Tumeweza kumuangamiza gaidi anayeitwa Dany. Tuna kila sababu ya kusema kwamba Tanania na dunia kwa ujumla ina amani kwani gaidi huyo amekufa, na tumefanikiwa kumuokoa mwanangu”
K2 alizungumza huku akiwa amejawa na furaha kubwa sana.
“Muheshimiwa raisi je tunaweza kuona mwili wa gaidi huyo?”
“Kwa sababu ya shambulizi hilo na sababu za kiusalama, basi kitengo maalumu kilicho endesha oparesheni hiyo kilichopo nchini Marekani kitatuonyesha mwili wa gaidi huyo akiwemo mpenzi wake Livna ambaye naye pia amekufa katika shambulizi hilo”
Nikajikuta nikinyanyuka kwa hasira sana, nikataka kupiga hatua japo moja mbele, ila Jojo kwa haraka kanishika mkono.
“Baba bado huna nguvu za kupambana na K2 kunywa damu ili nguvu zako uweze kuzihimili”
Jojo alizungumza kwa unyonge sana huku akinitazama usoni mwangu, kwa haraka nikiaelekea jikoni, nikafungua friji na kuchukua kidungu kimoja kilicho jaa damua mbayo kwa mara ya kwanza nilihisi kwamba ni juisi.
Nikaanza kunywa kwa kasi hadi nikaimaliza, Jojo akanitazama usoni mwangu huku nikiwa amejawa na tabasamu sana.
“Baba huu ni muda, sikuhitaji kukueleza juu ya hili tukio, nilihitaji ujionee wewe mwenyewe. Sasa ni muda wa kuzitumia nguvu zako”
“Tukio limetokea muda gani?”
“Limetokea usiku wa kuamkia leo”
“Nahitaji twende eneo la tukio”
“Lina ulinzi mkubwa sana”
“Twende eneo la tukio”
“Sawa ila kuna maandalizi tunatakiwa kufanya, njoo nikuonyeshe”
Tukaingia kwenye chumba kingine, chumba hichi kimejaa silaha za kila aina pamoja na mavazi ya jeshi karibia sara za majeshi ya kila nchi duniani.
“Ni muda wako sasa baba?”
Nikaanza kuzunguka kwenye chumba hichi nikitazama kila aina ya mavazi. Nikachukua mavazi ya jeshi la Marekani na kumfanya Jojo naye kuchukua mavazi kama haya. Tukavaa kwa haraka na nikachukua bastola mbili kama kawaida yangu.
“Kuna boti ipo eneo hili”
Jojo alizungumza huku tukitoka sebleni, tukatembea hatua kadhaa kuelekea kwenye fukwe hii ya bahari, nikaona boti moja ambayo ni kubwa na inaonyesha ina uwezo mkubwa wa kukimbia. Tukaingia kwenye boti hii na Jojo akaanza kuendesha kwa kasi boti hii. Kwa hasira kali ambayo imenitawala nikaanza kujihisi mwili wangu ukichemka kwa joto kali ambalo limenijia kwa muda mfupi sana.
“Baba tulizia hasira?”
Jojo alizungumza huku akinitazama usoni mwangu, kwani hapa baharini kuna upepo mkali sana ila usoni mwangu ninamwagikwa na jasho jingi sana. Mikono yagu ikaanza kunicheza pale tulipo anza kuzioa boti nyingi kwa mbali pamoja na helicopter nyingi za jeshi zikizunguka katika eneo hili. Jojo akanitazama huku akimeza fumba zito la mate.
Kitendo cha kufika eneo la meli hii inayo fuka moshi mwingi sana na ikonyesha kwamba imeshambuliwa sana, nikaanza kushambulia wanajeshi kadhaa waliopo kwenye boti ndogo. Mashambulizi  yakaanza kuibuka katika eneo hili huku wanajeshi wa Marekani na Taania wakijitahidi sana kuhakikisha kwamba wanapambana nasi ila kusema kweli uwezo wangu umeongezeka mara dufu, kwani hata mtu awe umbali gani, simkosi kwa risasi ambayo nitaidhamiria kumfikia popote juu  ya mwili wake.
‘Dany nakufaa’
Niliisikia sauti ya Magret kwenye masikio yangu.
“Baba nenda nianchie huku nje”
Jojo naye alizungumza na nina imani kwamba ameweza kusikia sauti ya Magreti. Kwa haraka nikarudikia mnyororo mkubwa wa nanga unao toka kwenye meli hii kubwa ya Livna, nikaanza kupandisha juu kwa kasi sana. Sikumaliza hata sekunde ishirini nikawa nimesha fika eneo la ndani ya hii meli.
Nikawaona wasichana wengi sana wakiwa wamekufa vibaya, wengine wamalipuliwa kwa mabomu na miili yao kupoteza baadhi ya viongo. Unyama ulio tendwa humu ndani kusema kweli unanifanya nizidi kupandwa na hasira, kila mwanajeshi ninaye kutana naye anaye jifanya kwamba anakagua maiti za wasicha hawa ili awamalizie kwa kuwapiga risasi, anakuwa halali yangu na kila ninaye mshika, basi ninahakikisha kwamba ninaking’ofoa kichwa chake kama wanavyo fanya watoto pale wanapo washika modoli yao.
Sauti ya Magreti ikazidi kuniita na kunifanya nizidi kushuka chini, ambapo tayari maji yamesha anza kuingia kwa wingi. Nikayafimba macho yangu na kuisikilizia sauti hii ni wapi inapo tokea. Kichwani mwangu nikaanza kuona vyumba vya hii meli vilivyo anza kukatiza kwa kasi kichwani mwangu hadi nikafanikiwa kugundua kwamba Magreti yupo kwenye chumba nilichokuwa ninaishi mimi na tayari maji ndani ya chumba chiho yameshaingia ndani.
Kwa haraka nikaanza kuelekea chini ya kabisa kilicho chumba hicho huku nikijitahidi kuogelea kwa kasi sana. Nikafanikiwa kufika nje ya mlango wa chumba hichi, nikajaribu kuusukuma na kukuta ukiwa umefungwa kwa ndani. Nikarudi nyuma kwa kasi kisha nikapiga kikumbo kizito mlango huu ukafunguka, nikamkuta Magreti akiwa amekaa amekaa kwenye moja ya kona ya chumba hichi huku amekumbatia tisheti yangu.
Kwa haraka nikamsogelea na kumkuta akiwa ndio anamalizikia katika kuishiwa na pumzi, kwa haraka nikaanza kumpuliza mdononi mwake, zoezi la mkujaza pumzi likafanikiwa. Magreti akafumbua macho yake, alipo nitazama akatabasamu. Kwa haraka nikamshika kwa mkono wangu wa kulia na kuanza kuogelea kuelekea juu sehemu ambayo bado haijazama ndani ya bahari.
Tukafanikiwa kuingia katika chumba cha cha mawasiliano, ambacho hakina maji kabisa. Nikakuta maiti nginyi sana za wasichana hadi watoto wadogo sana ambao ndio kwanza walikuwa wakikuzwa katika kuifanya kazi hii ya kijasusi.
“Mungu wangu”
Magret alizungumza huku machozi yakimwagia usoni mwake, na mwili wake wote umejawa na maji, nikaingia katika chumba cha pili ambacho tulikuwa tunakitumia, tukiwa na vikako vya kuwazungumza na baadhi ya viongozi duniani. Nikakuta maiti za Ester, Logate na wasichana wengine wawili.
“Hawa washenzi wamewaua hadi hawa wasichana”
Nilizungumza kwa sauti nzito iliyojaa utetemeshi mwingi sana.
“Dany”
Logate alikurupuka chini alipo lala, sote tukamtazama. Kwa nguvu Logate akanikumbatia huku machozi yakimwagika usoni mwake.
“Imekuwaje?”   
Nilimuuliza hukun ikimtazama usoni mwake.
“Wametuvamia, niliwahi kujilaza chini na kujipaka damu za Ester na mimi nikaonekana nimekufa”
Logate alinijibu huku akiwa amejawa na wasiwasi mwingi sana na majonzi mengi japo hajanijibu swali nililo muuliza.
“Dady inabidi tuondoke”
Magreti alizungumza huku akitetemeka kwa woga sana. Nikatazama moka ya laptop iliyo anguka chini, nikaiokota na kifunua, na kukuta ni nzima bado.
“Mulikuwa munafanyaje?”
“Tulikuwa tunajitahidi kupambana nao, kuna mmoja wa wasichana alivujisha signal ya sehemu tulipo ndio maana tumeshambuliwa hivi”
“Sasa unaweza kufanya chochote?”
“Ngoja”
Logate alizungumza huku akijipangusa machozi yake usoni. Akaitazama hii laptop, kisha akaanza kiminya minya batani zake.  Nikamtazama kwa umakini na nikaona nikitu gani anacho kifikiria.
“Nahitaji ku…”
“Kulipua vinu vya nyuklia nchini Marekani, sasa mabomu yao yote ya nyuklia yaelekeze kwenye miji yao mikubwa pamoja na ikulu  zao, kisha lipua vinu hivyo”
“Sawa mkuu”
Logate akayang’ata meno yake na kuanza kuminya minya batani za laptop hii kwa kasi sana. Nikachukua rimoti na kuwasha tv zote kwa bahati nzuri nikazikuta zikifanya kazi.
“Zimebaki sekunda ngapi?”
Nilimuuliza Logate huku nikitazama chaneli moja habari nchini Marekani ikitangaza juu ya jeshi lao kufanikiwa kulipua meli iliyo ficha magaidi.
“Niwekee picha za satelaiti zinazo onyesha Marekani nzima”
Kwa haraka Logate akafanya hivyo, na nikaanza kushuhudia jinsi miji mikubwa ya nchini Marekani ikilipuliwa na mabomu haya makubwa ya nyuklia ambayo wao wenyewe ndio watengenezaji. Nikaona jinsi ikulu ya Marekani nayo ilipata pigo hili ambalo wamestahili.
“Mkuu tayari, Marekani hadi ije kurudi kwenye nguvu yake ni baada ya miaka mia moja ijayo”
Logate alizungumza kwa furaha sana, nikamtazama huku nikiwa nimejawa na tabasamu.
“Niunganishe na K2”
“Sawa”
Ndani ya muda machache nikaoiona sura ya K2 kwenye Tv ya mbele yangu, uso wake baada ya kuniona mimi akastuka sana, wasiwasi mwingi ukamjaa, kigugumizi kikampata kwani ninaona jinsi kinywa chake kinavyo jaribu kuzungumza neno ila kinashindwa.
“K2 baada ya Marekani wewe ndio unafwata. Jiandae”
Nilizungumza kwa sauti nzito sana ambayo tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kuitoa kinywani mwangu. Baada ya kuzungumza maneno hayo nikaipiga ngumi tv hii na ikapasuka pasukua, nikiashiria kwamba ni muda wa kwenda kuonana na K2 uso kwa uso.
                                                                           ITAENDELEA
‘Haya sasa histori ya dunia imeandikwa, Marekani imebaki magofu na sasa ni zamu ya K2 je ni nini atakacho fanywa K2? Usikose sehemu inayo fwata ya hadi hii ya kusisimua kutoka kwa muandishi mahiri Eddazaria G.Msulwa”
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )