Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Saturday, January 12, 2019

Aliyedaiwa kuiba Sh mil saba kila dakika Asomewa Mashitaka Mapya 600

adv1
Mfanyabiashara Mohamed Yusufal aliyetajwa na Rais John Magufuli kuiba Mil.7 kwa dakika na mfanyakazi wake, Arital Paliwala wamesomewa mashtaka 600 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikiwemo kuisababishia serikali hasara ya Bilioni 14.98.

Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka yao na jopo la Mawakili wa serikalo wakiongozwa na Hashimu Ngole mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Wilbard Mashauri.

Katika mashtaka hayo yaliyosomwa kwa takribani saa mbili, washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kughushi, kuwasilisha taarifa za mwezi za mahesabu ya uongo kwa TRA, kukwepa kodi na kuisababishia serikali hasara ya sh. 14,987,707,044.58

Miongoni mwa mashtaka hayo ni kuisababishia serikali hasara, ambapo wanadaiwa kukwepa kodi ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008 hadi 2015 kupitia kampuni ya Pamplant ltd iliyokuwa inamilikiwa na mshtakiwa Yusufali ambapo mshtakiwa Paliwala alikuwa mfanyakazi wake.

Pia inadaiwa washtakiwa walitenda kosa hilo wakiwa wanatumia stakabadhi za kughushi pamoja na kutumia makampuni ya kughushi wakidai kuwa wamenunua vitu kutoka katika makampuni mbali mbali wakati wakijua baadhi ya kampuni hizo ni za kughushi huku zikiwa hazijasajiliwa Brela.

Hata hivyo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za uhujumu uchumi isipokuwa kwa kibali kutoka kwa DPP.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo umeshakamilika ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi January 24, 2019.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )