Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Monday, January 7, 2019

Baba Atiwa Mbaro Kwa Kumuua Mwanae Kwa Mapanga

adv1
Hazra Mwasenga, mkazi wa Kitongoji cha Haduye Kijiji cha Iwala, Kata ya Itale wilayani Ileje, mkoani Songwe, ametiwa mbaroni kwa tuhuma za kumuua mwanawe, Subi Mwasenga (28), kwa kumkata mapanga kisha kumzika kienyeji kwa siri, akimtuhumu kuiba nyama.
 
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Joseph Mwabezya, alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki na aligundua alipotembelea maeneo ya makazi ya mzee huyo alimsalimia na kuuliza kuwa mwanawe haonekani na kuhoji tuta lililopo pembezoni mwa nyumba yake.

Alisema baada ya kuhoji, Mwasenga alimweleza kuwa lile tuta ni kaburi la mwanawe ambaye alimuua kwa kumkata na panga kwa kosa la kuiba nyama na kwenda kuiuza, wakati yeye alichinja ng’ombe mdogo kwa ajili ya kitoweo.

Alisema baada ya kumkata na mapanga mwanawe, alipoona amekufa aliamua kuchimba shimo na kumfukia kwa siri kwa kuwa alitenda kosa la kuiba nyama.

‘’Nakuomba mwenyekiti nimekueleza haya kwa kuwa wewe ni rafiki yangu, iwe siri usimwambie mtu,” alisema mwenyekiti huyo wa kijiji.

Mwabezya alisema baada ya kutoka eneo hilo alikwenda kutoa taarifa hizo polisi na kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kutokana na ukubwa wa tukio hilo, na kuwa vyombo vya usalama baada ya kufika eneo hilo walimkamata Mwaisenga.

Joseph Mkude, Mkuu wa Wilaya hiyo na Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema ni tukio la pili la kikatili kutokea ndani ya muda mfupi.

Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na kuchukua hatua, ikiwamo kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo.

“Nilifika eneo la tukio nikiwa na kamati yangu ya ulinzi na usalama na kuagiza mtuhumiwa akamatwe, na sasa yupo rumande na pia nilitumia fursa hii kutoa rai kwa wananchi kuwa makini katika kutenda ukatili, tukio hili ni la pili kutokea baada ya hivi karibuni mtoto kumuua mama yake kwa panga,’’ alisema.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )