Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Thursday, January 17, 2019

Benki tatu ( TADB, NMB, TPB) zasaini makubaliano kusaidia wakulima

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeingia makubaliano na Benki za Biashara za NMB na Benki ya Posta (TPB) lengo likiwa kuwasaidia wakulima wadogo wadogo kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo chini ya TADB. 

Makubaliano hayo yamefikiwa ili kumwezesha na kumwinua mkulima mdogo aweze kumudu kilimo chenye tija, kupunguza umaskini na kufikia malengo ya serkali ya kufikia uchumi wa kati na viwanda ifikapo 2025.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo hayo, Meneja anayesimamia Mfuko, Bw. James Mwakilima alisema Serikali imeshatoa kiasi cha shilingi bilioni 45 kwa mfuko kwaajili ya  kuwakopesha wakulima wadogo  sehemu mbalimbali hapa nchini.

“Katika kutimiza azma yake ya kujenga uchumi wa kati na viwanda, Serikali imeshatoa shilingi bilioni 45 kwa TADB kupitia  mfuko  wake wa dhamana kwa wakulima wadogo ili wakulima waweze kujikita  kwenye kilimo chenye tija.” alisema Bw. Mwakilima

 Bw. Mwakilima alitoa wito kwa wakulima nchini kuitumia vyema fursa hiyo kwa kuwa itakuwa fahari kubwa kwa Benki ya Kilimo kuona wakulima wanainuka kiuchumi na kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa kati na viwanda kwa kuwa hakuna viwanda visivyo na malighafi.

“Ni nafasi pekee kwa  wakulima wadogo hapa nchini kuitumia vyema fursa hii kwani Benki ya kilimo ni moja ya madaraja ya kumvusha mkulima kutimiza malengo yake. alisisitiza Bw. Mwakilima.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya Posta (TPB), Bw. Ramadhan Mganga alisema kuwa kupitia Mfuko huo Benki yake imefanikiwa kuwakopesha wakulima wadogo hapa nchini. Bwana Mganga alitumia nafasi hiyo  kutaja mikoa ambayo imenufaika na mikopo kuwa ni pamoja na Simiyu, Iringa na Singida.

Aliongeza kuwa katika kuhakikisha wakulima wananufaika na mikopo hiyo, Benki ya Posta imekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu kwa wakulima wadogo juu ya mazao gani walime na kwa wakati gani ili waweze kuwa na kilimo chenye tija

TADB imejipanga kuhakikisha kuwa inashirikiana na mabenki  ya biashara ili kunifanikisha azma ya serikali ya Awamu ya Tano ya kuleta mageuzimakubwa katika sekta ya kilimo ikiwemo kuwainua wakulima wadogo na kuchagiza maendeleo ya sekta ya viwanda.
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )