Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Wednesday, January 16, 2019

Bodi ya mikopo yakusanya TZS 94.01 bilioni kati ya Julai – Desemba, 2018

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imekusanya jumla ya TZS 94.01 bilioni kutoka kwa wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu katika kipindi cha Julai – Desemba, 2018 na kuvuka lengo lake la kukusanya TZS 71.4 bilioni katika kipindi hicho.

 Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Abdul-Razaq Badru amesema jana jijini Dar es salaam kuwa makusanyo hayo yametoka kwa jumla ya wanufaika zaidi 198,659 ambao wamejiari au kuajiriwa katika sekta binafsi na umma.

 Wanufaika waliobainika na kuanza kulipa kati ya Julai – Disemba 2018
 “Katika kipindi hicho cha Julai – Desemba pia tumefanikiwa kuwabaini wanufaika wapya zaidi 12,600 ambao walikua hawajaanza kurejesha mikopo yao na sasa wameanza na hivyo kufanya wateja wanaorejesha kufikia 198,656 hivi sasa,” amesema Badru wakati akiongea na wanahabari katika ofisi za HESLB na kuongeza:

 “Makusanyo haya ya TZS 94.01 bilioni ni sawa na ongezeko la asilimia 8.7 ikilinganishwa na TZS 85.88 bilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho mwaka uliopita yaani, Julai – Disemba, 2017,” amesema.

Badru alikua akieleza hali ya ukusanyaji wa mikopo katika kipindi cha nusu mwaka wa fedha wa 2018/2019 utakaomalizika mwezi Juni mwaka huu ambao lengo kwa mwaka mzima ni kukusanya TZS 150 bilioni.

Kwa mujibu wa sheria iliyoanzisha HESLB, waajiri wanapaswa kukata asilimia 15 ya mshahara ghafi (basic salary) wa mnufaika na kuwasilisha makato hayo kwa HESLB ndani ya siku 14 baada ya tarehe ya mwisho wa mwezi wa makato.

Kujiunga na GePG
Katika mkutano huo, HESLB pia ilitangaza rasmi kujiunga na Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato yaani (Government e-Payment Gateway - GePG) na kusisitiza kuwa kuanzia sasa, malipo yote kwenda HESLB yatapokelewa kwa mfumo huo unaofuatwa na taasisi mbalimbali za Serikali.

Mwajiri au mnufaika anatakiwa kunakiri ‘Namba ya Kumbukumbu’ Control Number) iliyopo kwenye ankara (Loan Statements) zao na kufanya malipo kwa njia ya benki au simu. Maelezo ya kina yapo kwenye tovuti hii.

Namba za simu kwa wateja wenye maswali
Mkurugenzi Mtendaji amesisitiza kuwa kuanzia sasa, hakuna malipo yoyote yatakayopokelewa bila kufuata mfumo huo na kwamba wateja wenye maswali wapige kwa namba 0659 748 536; 0621 870 172; 0620 714 421; na 0621 870 173).

HESLB ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2005 ili kutekeleza majukumu makuu mawili. Mosi, kutoa mikopo ya elimu ya juu kwa wanafunzi wa kitanzania ambao ni wahitaji na pili kukusanya fedha za mikopo iliyoiva kutoka kwa wanufaika waliokopeshwa na Serikali tangu mwaka 1994/1995.

Mwisho.
Jumanne, Januari 15, 2019
tangazo
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )