Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 11, 2019

Bosi wa Zamani TRA na Wenzake wapandishwa upya kizimbani na Kusomewa Mashitaka 58

adv1
Aliyewahi kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake wanne wamepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kujibu mashtaka mapya 58, yakiwemo ya utakatishaji wa fedha na kujihusisha na mtandao wa uhalifu.

Wakili wa Serikali Mkuu, Hashimu Ngole akisaidia na Pendo Makondo na Patrick Mwita, amedai leo Ijumaa Januari 11, 2018, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustina Mmbando kuwa washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka hayo katika kesi ya uhujumu uchumi namba 2/2019.

Mbali na Kitilya, washtakiwa wengine ni Shose Sinare, Sioi Solomon pamoja na wengine wapya waliounganishwa katika kesi hiyo, Bedason Shallanda na Alfred Misana.

Kabla ya kusomewa mashtaka hayo mapya 58, washtakiwa Kitilya, Sinare na Solomoni walifutiwa kesi yao ya zamani iliyokuwa na mashtaka manane chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai  ( CPA), sura ya 20  iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Walifutiwa mashtaka hayo, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuieleza Mahakama hiyo kuwa hawana nia ya kuendelea na shauri hilo.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )