Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Sunday, January 27, 2019

BREAKING: Rais Magufuli atumbua Wakuu wa Wilaya wawili, ateua Majaji 21

adv1
Rais wa Tanzania, John Magufuli ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya za Tarime na Mwanga huku akiteua majaji 15 wa Mahakama Kuu na sita wa Mahakama ya Rufani.

Pia Rais Magufuli amewateua wakurugenzi 10 ili kuziba nafasi zilizoachwa wazi kwenye halmashauri za mikoa mbalimbali nchini.

Taarifa ya Rais Magufuli iliyosomwa leo Jumapili Januari 27, 2019 kwa vyombo vya habari na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imeeleza kiongozi huyo ametengua uteuzi wa wakuu wa wilaya za Tarime, Glorious Luoga na Aaron Mbogho wa Mwanga.

“Nafasi ya Luoga imechukuliwa na Charles Kabeho aliyekuwa kiongozi wa mbio mwenge mwaka jana. Wakati nafasi ya Mbogho imechukuliwa na Thomas Apson,” amesema Balozi Kijazi.

Balozi Kijazi amewataja majaji wa Mahakama ya Rufani walioteuliwa ni Dk Rehema Sameji, Dk Mary Levira, Ignas Kitusi, Winnie Korosso, Lugano Mwandambo  na Sahel Barke.

Majaji wa Mahakama Kuu ni Cyprian  Mkeha, Dustan Ndunguru, Seif  Kulita,  Dk Mtemi Kilikamajenga, Zeferine Galeba, Dk Juliana Masabo,  Mustafa Ismail,  Upendo  Madeha, Willbard  Mashauri,  Yohanne Masara,  Dk Lilian Mongella,  Fahamu  Mtulya,  John Kahyoza, Athuman Kirati na Suzan Mkapa.

Balozi Kijazi amewataja wakurugenzi wapya walioteuliwa kuwa na halmashauri zao kwenye mabano ni Isaya Mbenje (Pangani) Dk Fatuma  Mganga (Hai) Regina Bieda (Tunduma) Jonas  Malosa (Ulanga) Ali Juma Ali (Njombe) Misana Kangura (Nkasi) Diocres Rutema (Kibondo) Neto Ndilito (Mufindi) Elizabeth Gumbo (Itilima) Stephen Ndaki (Kishapu).

Majaji hao watapishwa Jumanne Januari 29, 2019 Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais John Magufuli. Pia, Ma DC na Wakurugenzi watapaswa kuhudhuria shughuli hiyo.

adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )