Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Friday, January 4, 2019

Fatma Karume: Sina Mpango Wa Kumiliki Kadi Yoyote Ya Chama Cha Siasa

adv1
Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume, amesema hana mpango wowote kwa sasa wa kumiliki kadi ya chama cha siasa nchini badala yake amedai ataendelea kutoa maoni juu ya masuala mbalimbali nchini kupitia taaluma yake ya sheria.
 
"Sijawahi kumiliki na wala sitaki kumiliki kadi ya chama chochote, kuhusu kushiriki kwenye siasa naweza kushiriki bila kuwa mwanachama wa chama chochote, kwani sasa hivi nawakosoa vizuri sana kwa hiyo naweza kutoa maoni yangu hata kama wakiniita mwanaharakati." amesema Fatma Karume.

"Kuhusu kuwa mfuasi wa chama cha siasa kwa sasa nikitaka nitafanya nisipotaka nitaacha, nitawaambia nikimiliki kadi ya chama chochote." ameongeza Fatma Karume.

Hivi karibuni akizungumzia kuonekana kwake kwenye maazimio ya vyama vya upinzani nchini Fatma Karume alisema alionekana kwenye mkutano huo baada ya  kualikwa na vyama husika kutoa elimu juu ya masuala ya katiba.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )