Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Thursday, January 3, 2019

Jeshi la Polisi Dar Lakanusha Taarifa ya Panya Road Kulitikisa Jiji Hilo Mwaka Mpya

adv1
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema Jiji hilo liko shwari na hakuna tukio lolote la uvunjifu wa amani ambalo linahusishwa na uwepo wa 'Panya road'.

Akizungumza leo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Lazaro Mambosasa amewahakikishia wananchi wa Jiji hilo kuwa hali ni shwari na hakuna tukio ambalo limetokea hasa kwenye siku ya mkesha wa mwakya mpya wa 2019.

"Tumeona moja ya gazeti likisema 'Panya road watikisa Dar'.Ukweli hakuna tukio limehusisha panya road siku ya mkesha wa mwaka mpya.Dar iko salama sana , hivyo taarifa hizo hazina ukweli wowote,"amesema Kamanda Mambosasa na kusisitiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum limejipanga kuhakikisha usalama upo wa kutosha.

Amefafanua katika siku ya mkesha wa mwaka mpya kulikuwa na makundi ya watu mbalimbali wakiwamo wanaosheherekea mwaka mpya,makundi ya watu waliotoka Kanisani na maeneo mengine, hata hivyo hakukuwa na tukio ambalo limefanywa na hao wanaodaiwa kuwa panya road kwani hakuna panya road .

"Tupo kwa ajili ya kuhakikisha hali ya usalama inakuwa salama,hivyo asitokee mtu mmoja kwa utashi wake akawatia hofu wananchi kwa kudai kuna panya road wakati hakuna," amesema Kamanda Mambosasa na kuongeza kuwa wananchi wasiwe na hofu na kuwatataka waendelee na shughuli zao kama kawaida za ujenzi wa uchumi wao na Taifa kwa ujumla kwa mwaka huu wa 2019.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )