Pakua App Yetu Playstore
<< BOFYA HAPA>> Kui Install

Saturday, January 5, 2019

Jux Na Mbosso Wasikilizwa Zaidi 2018.

Application ya Boomplay inafahamika kuwa chanzo kikubwa cha ukuaji wa muziki katika bara la Afrika na mnamo mwaka 2017 boomplay app iliweza kujinyakulia tuzo ya application bora ya muziki barani Afrika kupitia kipengele cha “App Afrika award” ikiwa imewafikia watu million 38 ulimwenguni kote na million 3 kwa Tanzania tu.

Kwa wapenzi wa muziki Application ya boomplay inapatikana kiuraisi ikiwa imepakuliwa katika simu za Android kama vile TECNO, Infinix na itel au unaweza kupakua kupitia google play store.
Application ya boomplay imeweza kusaidia wapenzi wa muziki kupakua/kusikiliza nyimbo mpya kwa wepesi zaidi lakini pia imeweza kulinda masilahi ya wasanii wetu kwa kuweza kutambua kiasi cha fedha msanii alichoingiza kupitia mauzo ya nyimbo katika kipindi Fulani.

Na kwa mwaka 2018 boompay imezalisha nyimbo million 833 na takribani nyimbo 30,000 zikiwa mbioni kuingia katika application ya boomplay kutoka kwa wasanii mbalimbali na kupitia takwimu za boomplay inaonyesha wasanii kama Vanessa Mdee, Nandy, Jux, Aslay, Mbosso, rayvanny, Harmonize kuwa miongoni mwa wasanii waliosikilizwa zaidi barani Afrika.

Boomplay mpaka sasa imefanikiwa kufanya kazi na makampuni mengine kama vile Universal music, Kudos, Tunicore na Africori na iko mbioni kuzindua application ya iOS.


Advertisement
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )