Je, Unatafuta Kazi au Ajira?
<< BOFYA HAPA>> Kupata Ajira Yako Leo

Wednesday, January 23, 2019

Kesi ya Mmiliki JamiiForums Kuendelea February 20

adv1

Kesi ya kuendesha mtandao ambao haujasajiliwa nchini kwa kikoa cha co. tz  inayomkabili mkurugenzi mtendaji wa Jamii Media, Maxence Melo na mwenzake Micke William imeshindwa kuendelea na ushahidi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Kesi hiyo ya jinai namba 458 ya mwaka 2016 ilipaswa kuendelea na ushahidi wa shahidi wa saba jana, lakini wakili wa upande wa mashtaka hakuwapo mahakamani.

Wakili wa Serikali, Elizabeth Mkunde alieleza kuwa wakili wa Serikali, Nassoro Katuga hakuwapo, hivyo kuomba tarehe nyingine kwa ajili kuendelea na ushahidi.

Baada ya maelezo hayo, hakimu mkazi mkuu wa Mahakama hiyo, Huruma Shahidi aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 20 itakapoendelea na ushahidi.
adv
Loading...

Advertisement
Usipitwe na Habari Yoyote. Install Mpekuzi App kwenye Simu Yako Upate Habari Zetu kwa Wepesi Zaidi

==>>... << BOFYA HAPA  Kui Install>>
Mgid
taboola apo chini
hapa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )